Mizengo Pinda: Natamani Katiba ya Tanzania ibadilishwe, ili Rais Magufuli aongezewe muda zaidi

Mh Pinda anajua katoa somo na kuhusu katiba aisee maana nimepitia kauli yake midomo na sauti na hisia za usoni hongera sana mzee angalau ile kauli ya katiba ipo tight inatosha sana kueleweka
Nime copy to na ku paste
katiba ipo tight🤔🤔🤔
 
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amesema isingekuwa katiba ipo “tight” kidogo, basi angetamani kuona Rais Magufuli akiongeza miaka mingine mitano baada ya muda wake kuisha.

"Ni kwakuwa tu katiba zenyewe kidogo ziko taiti lakini kama si kwa sababu hiyo, Walahi ningesema mzee piga mingine mitano tu''

Pia Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu ameongeza kuwa:

“Ni matumaini yetu kwamba katika kipindi hiki hata kama utatugomea kabisa kuongeza kidogo, lakini utahakikisha basi umetupa kiongozi mwingine mzuri kwa kusaidiana na NEC, atakayeweza kusukuma mawazo haya na maamuzi haya magumu ambayo unayafanya”

Mzee Pinda ametoa kauli hiyo leo hii wakati wa Semina ya Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) iliyofunguliwa na Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, inayofanyika Jijini Mwanza.

Ilimradi asifukue ufisadi wenu. Unatamanije maisha ambayo ulishindwa kuyaishi wakati wa uongozi wako? Unafiki mtupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
utatugomea kabisa kuongeza kidogo, lakini utahakikisha basi umetupa kiongozi mwingine mzuri kwa kusaidiana na NEC, atakayeweza kusukuma mawazo haya na maamuzi haya magumu ambayo unayafanya”
Naomba watanzania wote, mmshauri Dr JP Magufuli aniteue mimi niwe mgombea wa CCM, na baadaye Rais waJamhuri ya muungano waTanzania, ili niendeleze hapo alipofikia ndg wananchi mnasemaje?

Sahau about avatar mtaniona kiuhalisia na kuwatangazia ndo mimi mwenye avatar hii! mkinipenda lkn
 
Yaani ni kimeo kiasi hicho? mpaka aongezewe miaka y utawala? ni kashfa kubwa sana kumuongezea Rais miaka ya uongozi, maana yake ni kama ifutavyo;.

1) Mzembe goigoi, hakutimiza Ilani za uchaguzi hata robo! kuna viraka kibao sehemu.
Rais mchapa kazi anakamilisha miaka 2 tu!

2) Kuongoza nchi si kazi ndogo, alikiri mwenyewe kwa mdomo wake, sasa mnataka afie hapo? km mtu yeye ameona Gunia ni zito, ataka umsaidie, wewe unasema fikisha tu!

3)Ya kwake yasifanikiwe ila ya nchi, na vibaraka yafanikiwe! anatakiwa kulea na kuendeleza familia yake!

4)Mbaya zaidi mnataka kumchoresha kwenye jamii za kimataifa na watanzania kwa ujumla, ili atoke kwa aibu, ogopa sana mtu anayesema uko nyuma yako!

5)Yeye hajasema anataka, hata familia yake haijasema kitu kuhusu mpango huo, nyie mnataka, siyo unafiki huo?

6)Bora atumie akili ya JK Nyerer aachie ngazi mapema akiwa bado anapendwa na watu, atatumika km mzee wa Busara, kuliko aje kuwa km GADAFFI. kimbere mbere ni kibaya sana asiwasikilize.

7)Wa-Tanzania wenye vipaji, wapo bwerere, je wamesema hawataki kuonyesha vipaji vyao? Jiwe hawezi kuwa mwema miaka yote! Binadamu anapenda mambo tofauti tofauti!

8)Dhahiri kwa akili zao fake people wanaamini Urais ni kitu mzuri, au wanamwingiza chaka maksudi, wkt mwenzao anasema ni mzigo, mpaka analala na ma-file kitandani, sasa alale nayo mpaka lini?
hao hao ndo watakuwa wa kwanza, watamgeuka siku moja,

.
 
Badala ya kuangalia ni vipi tunajenga mifumo na taasisi zenye kuweza kutupa uongozi bora endelevu bila kujali kiongozi ni nani, tunapigia chapuo na jaramba habari za kubadili mifumo na taasisi ili zimruhusu mtu mmoja kutawala zaidi.

Hii ni moja ya sababu kubwa bado tupo masikini.

Hatufikirii sera, mifumo, taasisi, dhana.

Tunafikiria watu, matukio na mambo madogomadogo.

Mtu kama Pinda huyo naye kasoma sheria, kafanya kazi usalama, kafanya kazi Ikulu, kawa mbunge, kawa mpaka Waziri Mkuu.

Lakini bado anaongea mambo kama vile mtu asiyejua misingi ya utawala bora na uongozi endelevu.

Huyo mtu wanayetaka kumuongezea muda akianguka na kufariki kesho itakuwaje?
 
Ni mwendo wa kujikomba tu hivi sasa. Madikteta hawanaga mchezo, kila mtu wanamuweka kwenye mstari.
Ukitaka kuwatawala wafanye wawe masikini ili wakutii,hawa wazee wanaogopa wanajihami wasiguswe madhambi yao ya upigaji wa nyuma,hivo wanakwenda na mdundo wa ngoma.
 
A cha kujipendekeza
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amesema isingekuwa katiba ipo “tight” kidogo, basi angetamani kuona Rais Magufuli akiongeza miaka mingine mitano baada ya muda wake kuisha.

"Ni kwakuwa tu katiba zenyewe kidogo ziko taiti lakini kama si kwa sababu hiyo, Walahi ningesema mzee piga mingine mitano tu''

Pia Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu ameongeza kuwa:

“Ni matumaini yetu kwamba katika kipindi hiki hata kama utatugomea kabisa kuongeza kidogo, lakini utahakikisha basi umetupa kiongozi mwingine mzuri kwa kusaidiana na NEC, atakayeweza kusukuma mawazo haya na maamuzi haya magumu ambayo unayafanya”

Mzee Pinda ametoa kauli hiyo leo hii wakati wa Semina ya Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) iliyofunguliwa na Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, inayofanyika Jijini Mwanza.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
We we not binadamu au nugunugu?
Pamoja na kwamba sikipendi chama cha kijani, lakini huyu mzee Kayanda Peter Pinda ni mmoja ya wazee wachache wanao jielewa na kusimamia kile wanacho kiamini.

Mzee huwa namtazama akiongea hutoa kile ambacho yeye binafsi anakiamini, tena pasipo na tashwishwi husema jambo bila kushinikizwa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku kamasi zikimvuja kwa ukali wa pilipili kwenye msosi, jamaa alimuangalia mpishi huku machozi yakimlengalenga Kama mjusi kabanwa na mlango :
"Bwana mpishi, kwakweli leo umenikosha, na kama ikikupendeza tuongeze kofi lingine la bu'pilipili!"
🎃🎃🎃 😂😂 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
NB: Kwetu, Mwamadako, mtu akisema umuongeze kofi la bu'pilipili anamaanisha uchote kiganja kizima kilichoshiba uzichochee kwenye mboga!
 
We we not binadamu au nugunugu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ili jukwaa liwe huru, sio lazima basi tufanane mawazo, fikra na mitazamo.
Hivyo ndivyo ninavyo mtazama Mizengo, na hii haijalishi hata kama amekosea lakini anasimamia kile anacho kiamini.

Note:
Kwaleo nimekuhifadhi, ila nakupa onyo siku nyingine usije ukarudia kunitukana maana hauto baki salama na jf utaikimbia.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
kutoka kwenye nchi ya viwanda mpaka nchi ya kusifu,kusujudu,kuabudu na unafki kiwango cha SGR ya kenya
 
Kwanini Pinda asiombe Katiba ibadilishwe ili Raisi aruhusiwe kufuga Nyuki Ikulu.
 
Kinachofikirisha na kuongeza maswali mengi ni kwanini hawa watu huwa wanasema mazuri tu? Je, huyu rais wetu ni kweli hana mapungufu ambayo watanzania hawa wameona na yanatakiwa kurekebishwa ili tupige hatua kubwa zaidi kiuchumi, kisiasa na kijami? Nina mashaka kula anayemwongelea Mhe. Rais aidha anatawaliwa na itikadi za kichama au mapenzi yake binafsi, vinginevyo ni vizuri tukazungumzia mazuri na mapungufu ili maboresho yafanyike.
 
Back
Top Bottom