Mizengo Pinda declares assets in anti-graft drive

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
LEONARD MWAKALEBELA,
14th January 2010


Prime Minister Mizengo Pinda declared his assets today, saying he has between 20m/- and 25m/- only in all his bank accounts. He said the saving was due to accumulated salaries, pensions and allowances.

In a question and answer session with editors held in Dar es Salaam this noon, Mr Pinda also said that he has only one private car.

"I've only one car which I got through loans given to MPs," declared the Premier.

Mr Pinda also explained that he was possessing three ‘simple' houses in Dodoma, Mpanda and Dar es Salaam.

"I've one in Dodoma which I built through loans, another one in Mpanda town which I built using my little savings and a small one in my farm. he elaborated.

According to the premier, he is planning to build another house at his home village (Kibaoni), to accommodate his delegation during his visits to the village.

"I've been staying in my grandfather's houses in all years while I'm at Kibaoni, but due to my current capacity and security concerns associated with it, I can no longer stay there. I'll build another one to accommodate us especially my delegation," said the Prime Minister.

Mr Pinda wondered why high ranking government officials were amassing wealth, while their costs were borne by the government. The prime minister was optimistic that he would make good saving now as most, if not all, of his costs were borne by the government.

"Amassing wealth for what purposes, why should you be so greedy…I don't even hold shares anywhere, maybe later on after making some good savings," he explained.

Mr Pinda said that some people would be surprised by his decision of not using the post to amass wealth.


My Take:
I would like for the Premier to go a step higher (if he hasn't done so yet) to release to the press his wealth declaration forms. Even more, President Kikwete should direct all his ministers and deputies to declare their wealth publicly to emulate the Premier.. It isn't hard or is it?
 
Mwanakijiji

Mkuu endelea kuota JK aseme mali zake? Hapo ndio utaona wanavyoruka viunzi, tunasubiri kama watajaza fomu. Hivi ni kwa nini hawajazi zile fomu wakati kuna sheria zinazowabana wafanye hivyo.
 
Nakumbuka hata Mkapa wakati anatangaza mali zake alisema ana vijumba viwili tu tena kamoja kako Masasi nyumbani kengine kako Dar pale mtaa wa Sea View.

Kama Pinda ana gari moja alilopata kwa mkopo wa wabunge ina maana kabla alikuwa hana gari?
 
- Vipi imeshafanyika facts finding kwamba maneno yake yote ni kweli? Kwani amekua mbunge kwa muda gani? Si kila mwisho wa miaka mitano ya ubunge kila mbunge hupewa gari jipya au lingine,

- I mean nina heshima sana na PM wa sasa as a person, sina uhakika sana na uongozi wake, lakini hii habari nina wasi wasi haijakaa sawa na ingawa pia siamini kwamba ni mwizi kama wale tuliowazoea.

Respect.


FMEs!
 
sidhani kama umaskini ni kitu cha kujivunia kama anavyofanya Mh hapa,au ndio ujamaa uliotukuka, lazima uwe maskini ili uonekane mtu wa watu, hata kama mshahara wako wa halali unaruhusu kuwa na mali?

pia naungana na kuhoji hivi huyu si amekua mbunge huu mwaka wa kumi sasa, hela zake anapeleka wapi?
najua hazinihusu maana akishapewa zinakua zimeshakua zake, lakini narudi kwenye tatizo lile lile la kutangaza mali kidogo ili uonekana unaishi maisha ya kawaida kumbe una zingine kibao umezificha, though sisemi kuwa PM kaficha.

Naungana na kusema kuwa kutangaza mali isiwe mwisho, kujua kama anayosema ni kweli au nia ni kuturidhisha tu!

na hapa ni wajibu kwa wanaojua kusema, maana hiyo sheria iko wazi kwamba kama unajua mali ya kiongozi ambayo hajaiorodhesha unaruhusiwa kumuumbua...so nampa PM benefit of doubt kwamba anayosema ni kweli, ila kama aneyejua zaidi huu ndio wakati wake!
 
He probably means "under his name".. it doesn't include his wife, children or other close family members.. thats why I would like to see his declarations forms.
 
He probably means "under his name".. it doesn't include his wife, children or other close family members.. thats why I would like to see his declarations forms.

kwakeli, maana kama nakumbuka vizuri zile form mpya lazima hao wote utaje mali zao pia...na pia mmezipata lini, na hata ukiuza kitu unatakiwa ukitaje, form ni nzuri, tatizo ni wanoko kwenye kuzionyesha! wakati ni haki yetu!
 
EMPLOYMENT HISTORY Company Name Position From DateTo Date
United Republic of Tanzania Prime Minister 2/9/2008
Prime Minister's Office - Regional Admin.& Local Governments.Minister20062/8/2008
Prime Minister's Office - Regional Admin.& Local Governments.Deputy Minister2000/2005
State HouseClerk to the Cabinet1996/2000
State HouseAssistant Private Secretary to the President1982/1992State HouseSecurity Officer19781982

Ministry of JusticeState Attorney1974/1978

source:http://www.parliament.go.tz/bunge/mpcv.php?vpkey=39

inaonekana Mh. Waziri Mkuu ni muumini mkuu wa ideology ya ujamaa wa kiafrika kwa kutojitajirisha kwa mgongo wa ofisi ya umma au kufanya makeke ya kuwa na magari kibao binafsi wakati wananchi waliokupa dhamana ya uongozi wanaishi kwa kutumia chini ya dola mmoja ya kimarekani kwa siku.
 
Siamini chochote asemacho kuhusu mali zake kwani hakuna namna yeyote ile ya kuthibitisha. Ingekuwa kama wanavyofanya Marekani na kufile taxes hapo kidogo tungeweza kuweka imani ktk ayasemayo
 
..lakini jamaa ana 25 milion zimekaa tu bila kazi halafu mnasema ni masikini.

..huu umasikini mnalinganisha na nani haswa?

..kuna kiongozi mmoja alifariki, tukaambiwa alikuwa na watoto 50. wote walikuwa na afya tele. hakuna hata mmoja alikuwa na utapia mlo.

..hizi kazi za serikali zinalipa kuliko mnavyofikiri. ndiyo maana wakina Ndulu wanaacha kazi WB na kurudi bongo.
 
Umilki wa mali havina uhusiano na uadilifu. Tajiri na maskini wote wanaweza kuwa viongozi waadilifu au viongozi mafirauni; uadilifu ni tabia ya mtu mwenyewe. Bloomberg ni tajiri mkubwa sana lakini sasa ni karibu miaka tisa kiwa Meya wa New York wala hajahusishwa na skendo zozote za utovu wa uadilifu.

Ingawa wanasiasa wengi wa caliber yake sasa hivi ni matajiri sana, bado siwezi kusema kuwa kwa vile Pinda hana mali sasa hivi basi ni mwadilifu, it takes more than that. Mkapa alipoanza alionyesha kuwa hakuwa na malin nyingi na kulikuwa na ushahidi wa kishushuhu kuthibitisha kuwa hakuwa na mali wakati huo. Lakini katika miaka mitano tu ya mwisho wa utawala wake, Mkapa akageuka kuwa tycoon wa kutupwa.
 
To me Mizengo Kayanza Peter Pinda sounds sincere.
The PMs' position has not intoxicated his normal and official life functions.
 
To me Mizengo Kayanza Peter Pinda sounds sincere.
The PMs' position has not intoxicated his normal and official life functions.

- Mkulu LG, heshima mbele sana, tulishaumwa na nyoka sasa tunakua na wasi wasi hata na unyasi ukipiga kelele, ni vyema tukathibitisha kwa facts na evidence in the future, maana kama amekuwa mbunge for 10 years, basi ameshapokea zile ruzuku za mwisho wa 5 years, yaani Millioni 38 Tsh, sasa zidisha mara mbili, na magari mawili ya ubunge,

- Anatakiwa kuwa na more mali than zilizotajwa, ingawa kwa maoni yangu ni kwamba he is a good man, lakini tumeumwa mno na manyoka sasa hatuamini mtu tena! siamini kwamba amesema mali zake zote sasa the question ni WHY? au anaficha nini na hasa what is the agenda hapo maana hawa wanasiasa hawakurupuki tu hivi hivi?

- Halafu politically nini faida ya Waziri Mkuu wetu kutangaza mali zake, bila kuwalazimisha Mawaziri wake au wote walioko chini yake kufuata muongozo wake?

Respect.


FMEs!
 
- Mkulu LG, heshima mbele sana, tulishaumwa na nyoka sasa tunakua na wasi wasi hata na unyasi ukipiga kelele, ni vyema tukathibitisha kwa facts na evidence in the future, maana kama amekuwa mbunge for 10 years, basi ameshapokea zile ruzuku za mwisho wa 5 years, yaani Millioni 38 Tsh, sasa zidisha mara mbili, na magari mawili ya ubunge,

- Anatakiwa kuwa na more mali than zilizotajwa, ingawa kwa maoni yangu ni kwamba he a good man, lakini tumeumwa mno na manyoka sasa hatuamini mtu tena! siamini kwamba amesema mali zake zote sasa the question ni WHY? au anaficha nini na hasa what is the agenda hapo maana hawa wanasiasa hawakurupuki tu hivi hivi?

- Halafu politically nini faida ya Waziri Mkuu wetu kutangaza mali zake, bila kuwalazimisha Mawaziri wake au wote walioko chini yake kufuata muongozo wake?

Respect.

FMEs!
That is just a clear message to his sub-ordinates. Very likely majority of them thought the forms are for the juniors. Ni kamtego hako, you wait and see the outcome. Utawasikia na wengine.
 
Nina imani na Pinda ...upande wa uadilifu...sio ajabu watu wa usalama ..walitaka tangu mwanzo mwaka 2005 awe waziri mkuu...ili kuondoa nguvu ya mtandao serikalini,kwani ni ukweli uliowazi kuwa Kikwete amelazimika kuchagua pinda baada ya things ku fall apart .....

deal la mwanzo la kikwete kuaminiwa kupewa urais lilikuwa kumbakisha SHEIN na kumpa Pinda uwaziri mkuu...

uhusiano wa kikwete ,na pinda na shein ni wa kikazi zaidi ....kwani hawa si marafiki zake wa kukaa vikao jioni...na ndio maana bado kuna malalamiko ndani ya circles kuwa JK hupata ushauri wa uendeshaji serikali kwa watu wengine wasiokuwa barazani kama Lowassa na kwa mawaziri ambao nimtandao kama sofia simba,shukuru,ghasia etc...its like baadhi ya ajenda za baraza la mawaziri hujadiliwa kwanza kweye kitchen cabinet ....kupata msimamo wa kuingilia barazani au hata kwenye vikao vya NEC na cc Mtindo ndio huo huo!!!

Upande wa pinda na shein tunakubali uadilifu wao lakini tunataka waongeze juhudi kuhakikisha serikali hayumbi!!!

Nitapenda kuona kama JK nae atatangaza mali ....katika siku za karibuni amejilimbikizia mali sana.....inawezekana kwenye campagne donations alibakiwa na pesa nyingi sana baada ya Pesa za EPA kutumika ni wazi ile michango ya marafiki zake na nje kama ule wa IRAN ...ilibakia kwenye personal account zake...ukizingatia hana wasi wasi na gharma za mwaka huu......inabidi sheria ya uchaguzi iweke hili wazi ....wagombea waweke wazi pesa zao za kampeni.......na baada ya kampeni wachapishe hesabu zao...na kwa aliyeshinda ...atakiwe kupeleka fedha zake za kampeni zilizobaki kwenye mashirika ya misaada...nadhani hata marekani wanafanya hivyo ...Obama alibakiwa na pesa nyingi na ali declare!!
 
-
- Anatakiwa kuwa na more mali than zilizotajwa, ingawa kwa maoni yangu ni kwamba he is a good man, lakini tumeumwa mno na manyoka sasa hatuamini mtu tena! siamini kwamba amesema mali zake zote sasa the question ni WHY? au anaficha nini na hasa what is the agenda hapo maana hawa wanasiasa hawakurupuki tu hivi hivi?

- Halafu politically nini faida ya Waziri Mkuu wetu kutangaza mali zake, bila kuwalazimisha Mawaziri wake au wote walioko chini yake kufuata muongozo wake?

Respect.

FMEs!


Mkuu, FMES nakubaliana kabisa nawewe, hatujui kama Kayanza alikuwa anaishi nyumba ya serikali au ya kupanga kabla ya uwaziri, lakini vilevile it seems hapa kuna a tricky situation.

Mkuu wa kaya bado hajatangaza mali zake, hivyo walio chini yake inaleta kigugumizi kidogo.

Na hatujui nani atachora mstari mchangani kwa wale ambao hawajatangaza mali zao.
 
PM, habari yako imetulia.

Ila sijui kama wataisikiliza maana kama yeye kashaweka mahekalu yake, basi si vibaya akiweka na ya watoto wake popote watakapotaka.
 
Pinda atangaza mali zake

• Asema akaunti zake zote hazizidi sh milioni 25

na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ametangaza mali zake. Aliwaambia wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jana ofisini mwake, Dar es Salaam, kuwa anamiliki nyumba tatu, na yuko katika pilikapilika za kujenga nyumba ya nne.

Pinda, ambaye ni kiongozi wa kwanza wa serikali ya awamu ya nne kutangaza mali zake hadharani, alisema kwamba ana akaunti kadhaa ambazo zikijumuishwa pamoja, zina kiasi cha pesa kisichozidi sh milioni 25.

Alisema ana nyumba moja Dodoma, ambayo aliijenga kwa mkopo wa serikali; nyingine iko nyumbani kwao Mpanda na nyingine, ambayo aliiita kijumba iko Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa nyumbani kwa baba yake, ambaye yeye alimuita babu, anayeishi Kibaoni, Wilaya ya Mpanda, hana nyumba bali chumba kimoja ambacho amekuwa akikitumia hadi alipokuwa waziri mkuu.

Alisema kuwa hakuwa na shida na chumba hicho, lakini katika mazingira ya sasa ya nafasi aliyonayo amelazimika kupaboresha.

“Sasa tunajenga pale,” alisema huku akiwatania walinzi na wasaidizi wake kwamba kama si wao, yeye asingepata shida kufikia pale kama ilivyokuwa zamani.

Pinda alitoa maelezo hayo baada ya kuulizwa kuhusu tetesi kwamba yeye ni waziri mkuu “maskini” akilinganishwa na vigogo waliomtangulia na wengine waliomo serikalini.

Katika kujivunia “umaskini” huo, Pinda alisema: “Najiona kama nina bahati, namshukuru Mungu kunifikisha hapa nilipo.”

Alisisitiza pia kuwa hana hisa katika kampuni yoyote, halafu akasema kwa utani, “inawezekana ni ujinga tu wa waziri mkuu huyu wa sasa…”

Alisema kwa nafasi aliyonayo analipwa pensheni kila mwezi, kwa sababu serikali imeweka utaratibu mzuri wa kumhudumia kwa kila kitu, hivyo anaweza kutumia mapato yake ya kila mwezi kufanyia mambo ya msingi au kuweka akiba.

“Ukisha-retire (ukishastaafu) serikali inakujali hadi kifo. What more do you want (Unataka nini zaidi)?” alisema.

Mara ya mwisho kwa kiongozi wa kitaifa kutangaza rasmi mali zake ilikuwa mwaka 1995. Wakati huo, Rais Benjamin Mkapa, katika mwanzo wa utawala wake, alitangaza kuwa ana nyumba mbili; moja Dar es Salaam, nyingine kwao Lupaso.

Alipostaafu, licha ya wananchi kudai atangaze mali alizonazo, Mkapa hakusema ana mali kiasi gani. Lakini inajulikana kuwa idadi ya nyumba zake ilikuwa imeongezeka, na alikuwa amejiingiza katika uwekezaji ambao baadhi ya wakosoaji wake wamekuwa wakiulalamikia kwa misingi ya kisiasa.

Hatua ya Pinda kutangaza mali zake ni changamoto kubwa kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye amekuwa bubu kuhusu nyumba na mali zake anazomiliki.

Kikomo cha ubunge

Katika mazungumo ya jana, Pinda alipendekeza wabunge wawekewe kikomo cha muda wao wa utumishi.

“Tuweke kipindi maalumu cha uongozi. Itakuwa suluhu (suluhisho) nzuri ya kuondokana na vijimaneno na kukamatana uchawi…Miaka 15 kwa mfano, inatosha kwa mbunge, na watu watakuwa wanajua kuwa muda wako unaisha,” alisema.

Alisisitiza kwamba Tanzania ina watu wengi wenye uwezo, na kwamba kuweka vipindi maalumu kungesaidia kujenga mazingira ya kuwaandaa wengine kupokeana nafasi za uongozi.

Alikuwa akijenga hoja kuhusu rai inayotolewa na baadhi ya wananchi kwamba wazee waachie ngazi, akasema hoja si umri bali muda ambao mtu anakuwa amekaa katika nafasi hiyo.

Hata hivyo, alionya kuwa viongozi wenyewe walio madarakani hawawezi kujipimia. Akasisitiza kuwa ni vema viongozi kuiga mfano wa hayati Rashid Mfaume Kawawa wa kuachia ngazi kwa hiari.

Katika kusisitiza hayumo miongoni mwa wanaopaswa kung’atuka sasa, alisema yeye si mzee, lakini akadokeza kwamba iwapo atapata tena fursa ya kuchaguliwa kuwa mbunge miaka 15 inamtosha.

Kasi ndogo ya serikali

Pinda alikataa kukiri kwamba utendaji wa serikali ya awamu ya nne umekuwa wa kasi ndogo.

Alisema swali hilo ni gumu kwake, kwani yeye ni msimamizi wa shughuli za serikali, na kwamba inafanya kazi kupitia Baraza la Mawaziri, na kila waziri ana majukumu ya kutekeleza.

“Kila waziri ana potifolio (wizara) yake, lazima aisimamie. Tunakwenda vizuri kiutendaji. Jitihada zimefanyika,” alisema.

Kiswahili lugha ya kufundishia

Waziri Mkuu alisisitiza umuhimu wa kutumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia ili kukuza maarifa na ujuzi wa watoto wa Kitanzania, kwa kuzingatia kuwa wanafunzi na watoto wengi hawajui Kiingereza vizuri.

“Tutumie lugha inayoeleweka. Mfano China, Ufaransa, Ujerumani na kwingineko wanatumia lugha zao kufundishia,” alisema.

Alisema ni ajabu kwamba hata sheria ndogo ndogo za halmashauri zetu, na hata sheria zinazotungwa bungeni zinaandikwa kwa Kiingereza, ilhali wanaozipitisha wanazijadili kwa Kiswahili, na wanaozitekeleza wanajua Kiswahili.

Akasisitiza: “itabidi tufike mahali tusema ‘hapana’.”

Sheria ya Uhuru wa Habari

Pinda alikataa kueleza sababu za serikali kuchelewesha muswada wa sheria ya uhuru wa habari ambao umekuwa unapigiwa kelele na wananchi kwa miaka mitatu mfululizo sasa, na ambao harakati zake zimeanza wakati wa serikali ya awamu ya tatu.

Muswada huo ambao ukipitishwa utasaidia kurekebisha na kufuta baadhi ya sheria mbaya na katili zilizopo, uko mikononi mwa serikali baada ya wadau kukataa toleo la awali ambalo serikali ilitaka kulipitisha kwa kasi. Wadau waligundua kasoro kubwa, wakaomba upitiwe na kurekebishwa upya.

Miongoni mwa sheria zinazotarajiwa kufutwa au kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na muswada huo ni Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, ambayo serikali imekuwa ikiitumia vibaya kuyafungia magazeti yanayoikosoa.

Alipoombwa ataje tarehe ya kupelekewa muswada huo bungeni ili ujadiliwe na kuwa sheria, Pinda alitoa matumaini yasiyokamilika, akisema: “Haitawezekana kwa Januari, labda Aprili. Kama tutashindwa yote sawa sawa, atakayekuja atalisukuma.”


Chanzo: Tanzania Daima
 
Pinda tunakushukuru, uking'atuka uje utujulishe umevuna kiasi gani, usifanye kama Rais mstaafu Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Sumaye ambao walitutangazia mali wakati wanaingia madarakani lakini wakatoka kimya kimya! Pia tujulishwe mali zilizoandikishwa kwa majina ambayo sio ya wahusika, isije ikawa ni janja kuonyesha mali kidogo kumbe zingine zimechomekwa kwa watu wengine (money laundering).
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom