MAKOLE
JF-Expert Member
- Feb 5, 2012
- 618
- 280
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka Watanzania na waumini wa dini zote nchini humo kudumisha amani na utulivu. Mizengo Pinda amesisitiza kuwa, Watanzania wanapaswa kukataa suala la kuiingiza nchi katika vurugu na kukataa vishawishi vitakavyosababisha uvunjifu wa amani.
Waziri Mkuu wa Tanzania amewaomba viongozi wa dini mbalimbali nchini humo kufanya juhudi za kuwafundisha waumini wao elimu inayozingatia misingi ya imani za dini zao na kukemea tabia ya wanasiasa kufanya siasa bila kutilia maanani suala la amani.
Mizengo Pinda amebainisha kwamba, Watanzania wana mchango mkubwa katika kuhakikisha nchi haiingii kwenye vurugu kwa kutokubali na kutoshawishika na vishawishi vitakavyovuruga amani ya nchi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amelaani vikali vitendo vya kinyama vya kuchinjwa maalbino kwa imani na kishirikina na kusisitiza kwamba, watu wanaofanya vitendo vya kinyama kama hivyo hawana imani na Mwenyezi Mungu na ndio maana wanajitumbuikiza katika vitendo hivyo vinavyokinzana na ubinadamu.
CHANZO: Mizengo Pinda awataka Watanzania kudumisha amani
MY TAKE: Hivi kwa kashfa ya ESCROW haoni kwamba naye ni mmoja wa wanaochochea/ wanaoweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini?