Mizengo Pinda amkaribia Nyerere kwa Uongozi Bora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mizengo Pinda amkaribia Nyerere kwa Uongozi Bora

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kanda2, Aug 16, 2009.

 1. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuwa mujibuwa utafiti anamkaribia Mwalimu Nyerere kwa uongozi bora.

  Na Leon Bahati

  MIAKA 10 tangu kifo chake,Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ameongoza kwa ubora miongoni mwa mawaziri wakuu 10 waliowahi kushika wadhifa huo nchini, akifuatiwa kwa karibu na Waziri Mkuu wa sasa, Mizengo Pinda.

  Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa miezi mitatu iliyopita na Kampuni ya Synovate ambayo zamani ilikuwa ikijulikana kama Steadman Group Tanzania, Pinda ametofautiana
  kwa pointi moja tu nyuma ya mwalimu Nyerere.

  Mwalimu Nyerere anaongoza kwa asilimia 29 na Pinda anamfuatia kwa asilimia 28 na kuwaacha wengine kwa tofauti kubwa akiwamo aliyemtagulia Edward Lowassa. Mawaziri wakuu wanaoshika mkia kwa ubora ni John Malecele, Cleopa Msuya na Joseph Warioba ambao kila mmoja amepata asilimia moja.

  Hayati Edward Sokoine, ambaye alikufa kwa ajali ya gari mwaka 1984 akiwa ana sifa kemukemu kutokana na kuongoza vita dhidi ya walanguzi na wahujumu uchumi, anashika nafasi ya tatu kwa ubora akiwa na asilimia 26.

  Baada ya Sokoine ambaye anashika nafasi ya tatu, mawaziri wakuu wengine wamepata alama za ubora chini ya asilimia 10.

  Nafasi ya nne inashikiliwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye kwa asilimia sita wakati Edward Lowassa ambaye alijiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond mwaka jana, anafungana na Mzee Rashid Kawawa na kushika nafasi ya tano kwa kuwa na asilimia nne.

  Nafasi ya tano inashikiliwa na Dk Salim Ahmed Salim ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) ambao kwa sasa unajulikana kama Umoja wa Afrika (AU).

  Utafiti huo unamuonyesha pia Pinda kama waziri mkuu anayefahamika zaidi kwa watu kuliko wengine. Katika kundi hilo, Pinda anafahamika kwa watu kwa asilimia 81, akifuatiwa na Lowassa kwa asilimia 73.

  Wanaofuatia pamoja na kiwango cha asilimia cha kufahamika ni Sumaye (60), Sokoine (45), Nyerere (37), Kawawa (34) Malecela (24), Warioba (20), Msuya (18) na Dk Salim (14).

  Meneja Msaidizi wa Synovate, Agreey Orio aliviambia vyombo vya habari hivi karibuni kuwa kwenye utafiti huo Rais Jakaya Kikwete ana ana nafasi kubwa ya kuchaguliwa tena kwenye nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao, 2010.

  Kwa upande wa rais wa Zanzibar, utafiti huo ulionyesha kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, anapewa nafasi kubwa ya kushinda.
   
 2. S

  Shamu JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni moja kati ya research za uongo na propaganda. Huo utafiti unaonesha propaganda bado zinatawala Tanzania. Nyerere ni kiongozi bora? Pinda pia? Umaskini tuliokuwa nao WTZ; unataka kuniambia kwamba Nyerere alikuwa kiongozi bora? Huo utafiti ni Uongo na propaganda tupu.
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hivi nyerere alikuwa kiongozi bora sana eeh.mimi siiti research ya uongo bali ni research ya upumbavu kuwai kuisikia ndo hii
   
 4. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,315
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Shamu,
  Hivi umaskini wa wa-Tanzania umesababishwa na Nyerere! Wakati anachukua uongozi hao waTZ walikuwa na hali gani?
   
 5. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Shamu na Kigogo vichwa vyenu vibovu!

  Huo utafiti unalinganisha waliowahi kuwa mawaziri wakuu. Nyerere ndio kinara wao, hata Pinda anapiga mzigo vizuri. Sijui nyie mnadhani nani alikuwa bora!
   
 6. Jenerali QoyoJB

  Jenerali QoyoJB JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Jamani watanzania wenzangu msidanganyike na utafiti wa steadman wa uongozi bora hizi ni data za kupikwa, hii ni njama wataalamu wanaita "ajenda seting" sasa wananchi wasioelewa watasema kumbe bado hawa watu wanakubalika kwanini tusiwapigie kura kumbe data za kupikwa.

  Mimi sibishi kuwa Pinda ni mzuri kiuongozi tatizo ni watu anaoongoza nao serikali isiyojali watu.
  Jk alivyoingia tulimwamini lakini watu aliowakuta wanamkwamisha na yeye kutoka ni ngumu tutamsaidiaje?

  Hebu angalia anawakumbatia kina Hosea, Mwanyika na Katibu mkuu wa Nishati na Madini wakati akijua walihusika na Richmond sasa tutamwamini vipi?

  Ukitakata kuokoa mti mzuri shambani usiungue na mota una fyeka nyasi za pembeni kwanza ili moto usifike kwake sasa Jk kawakumbatia mafisadi lazima ataungua nao japo tunampenda sana naye anajua hivyo. Ingekuwa mimi ningemwambia Jk fumba macho anzisha chama chako wachukue watu wazuri gombe mwakani. Nasema hivyo kwasababu Wadhamini wa CCM ni kila Lowasa naye Chenge juzi tumesikia UVCCM wamempa ukamanda kuwalea JAMANI mnangoja nini? haya minihayo tu kwa sasa endeleeni kushabikia tafiti za steadman ambazo tunajua zilipikwa.

  Subirini mwakani vumbi itakavyokuwa ni zaidi ya 1995 na Zenji ndo hivyo tena Kingunge kashamkubali Maalim Seif kuwa ni mtu mwenye msimamo, umewahi kusikia hilo kwa Kingunge miaka iliyopita? kama hujasoma alama za nyakati soma sasa CCM wenyewe wanalumbana majukwaani vikao vya chama wameona havifai.
   
 7. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu huu utafiti unatuonyesha ukilinganisha viongozi wote waliohudumu
  kwenye nafasi hiyo ya ukiranja (PM) kimsingi Nyerere na mtoto wa mkulima wako safi manake wemgine sio walikuwa wanatupeleka chaka!
   
 8. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Acha kufuru!
   
 9. M

  Magezi JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  utafiti huu ni wa kijinga. Utatuambiaje mtu tunayemuona na kumjua kwa upumbafu wake alafu useme ni bora sijui kuliko nani?? Pumbafu zenu hata hao synovate!!!
   
 10. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Mngeniambia kuwa Sokoine ndiyo anaongoza kidogo itaniingia akilini, lakini Pinda, mh! I doubt...........
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu, sidhani kama utafiti ndio tatizo. Haya ni maoni ya Watanzania, hivi ndivyo tunavyofikiria
   
 12. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  JAMANI Pinda kafanya lipi la maana hadi sasa? kama ni uadilifu basi DR.Salim A.Salim,Kawawa na Sokoine ndio waaminifu,tuliambiwa kuwa Sokoine alikufa akiwa na suti pea mbili jee Pinda ana suti pia ngapi?

  DR.Salim anaweza kufananishwa na Pinda? Pinda huyu kafanya kazi lini hadi apewe alama hizi? Mkapa kwa term yake ya kwanza alikuwa anaonekana ni muadilifu hadi pale alipofariki Mwalimu Nyerere ndio akaonesha ngozi yake halisi.Pinda hajakaa hata miaka mitatu tutamtathimini vipi? mwanafunzi hupimwa mwanzo wa kozi au mwisho wa kozi?

  kama Pinda ni kiongozi wa mfano ashughulikie maazimio ya bunge juu ya Richmond angekuwa Sokoine angefanya kazi yake.
   
 13. The Spit

  The Spit JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Huu utafiti haujatumia creteria sahii katika kupata maoni ya watu ndo maana matokeo hayana ukweli wowote na uhalisia,kwa mfano hapo mwishoni wanapomalizia kwa kuelezea kuhusu mawaziri wakuu maarufu,kwamba anaongoza Pinda,Lowasa,Sumaye.....
  hii inaonyesha kuwa hawakutumia approval rates katika utendaji na ufanisi wa utendaji waziri mkuu mhusika bali kwa kuuliza tu kuwa kati ya hao hapo nani ambaye labda mtu anamfahamu,katika hali ya kawaida vijana wengi watanzania na watanzania wengi tu hawafahamu hata kama Nyerere alishawahi kuwa waziri mkuu,Au kama sokoine au DK.Salim alishawahi kushika wadhifa huu,kwa hiyo obviously wengi watamfikria Pinda au Lowasa au Sumaye,,,na wasimfikrie heta Jemadari Hayati sokoine.Popularity should be judged in terms of job approval rates,and not who comes to your mind first which is what these people have done in their research.
  if it was based on job approval rates then it's obvious Sokoine is the winner,and not Sumaye,Pinda or Lowasa kama inavyoonyesha huo utafiti.
  So i agree with majority here that this whole research thing is totally and completely misleading!
  it's a crap!
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Aug 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kweli kabisa Kajathesi, nakuunga mkono kuwa huwezi fanya Utafiti wa viongozi hasa kiti cha Waziri mkuu ikiwa hufahamu Nyerere alifanya nini akiwa waziri Mkuu!.. Sokoine alifanya nini positive wakati wake kisha ukapima ufanisi wa watu wote hawa sii tu kutokana na utendaji wao bali pia shurba na mapambano waliyosimamia.
   
 15. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  hivi hao stedman hawajipendi mpaka wamsifie dr salim
  embu fikiria wangesema dr salim ndio bora.....
  kusema dr salim ni bora ni sawasawa na kusema bilali ni maarufu..
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Aug 16, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,660
  Likes Received: 82,446
  Trophy Points: 280
  Kwangu mimi huyu Pinda ni ZERO kabisa tangu siku aliyotamka kwamba "mafisadi ni matajiri wakubwa sana nchini mwetu, kama wakikamatwa basi nchi itawaka moto" Huyo si hafai tu kuwa Waziri Mkuu bali hata mjumbe wa nyumba kumi kumi, angalia alivyosimama Bungeni kutaka kumtetea fisadi Mkapa eti ni kiongozi safi kabisa! Pamoja na kufanya biashara akiwa Ikulu, kuhusika kwa karibu kabisa katika ununuzi wa kifisadi wa Rada, magari na helicopters za jeshi, kuiba mgodi wa Kiwira na kujiuzia kwa 10% ya thamani ya mgodi huo! Kuhusika katika kusaini mikataba ya uchimbaji wa madini yetu ambayo haina maslahi yoyote kwa nchi yetu. Yote hayo Pinda aliyafumbia macho na kumuona fisadi Mkapa kama Mr Clean!!! Halafu leo tunaambiwa eti utendaji wake unakaribiana na Mwalimu!!!! :confused:
   
 17. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Hao Synovate waweke hiyo "Poll" yao hapa halafu na sisi tujibu maswali yao na kupiga kura tuone kada ya wasomi inasimamia wapi kuhusu hao viongozi.
   
 18. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwani wewe hufahamu huo utafiti huwa unafanyika vipi? Wacha ni kueleze watafiti wanakuja na kitu chao-halafu wanasema tutafute watu wa ku-support hicho kitu. It is as simple as that. Sasa wanasema wanatafuta maoni pale lakini wanaouulizwa ni wale wale ambao watakubaliana na wazo la tafiti. Hiyo kitu kwa kwetu Afrika - wala isikugutushe ni mchezo wa karagosi usanii tu huo
   
 19. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nyerere hajapatapo kuikandia Zenj. Pinda anaonekana haipendi Zenj. Any way hatuhitaji kupendwa naye. Pinda si sawa na Nyerere. . Abadan- Asilian.
   
 20. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Heri wewe umesema ati mtu asiyeheshimu katiba awe bora mwee? Jina lenyewe tu ati syndicate, labda ya majambazi.
   
Loading...