Elections 2010 Mizengo Kayanza Peter Pinda's Profile

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
GENERAL
ID No.: 1038
Salutation: Honourable
First Name: Mizengo
Middle Name: Kayanza Peter
Last Name: Pinda
Member Type: Constituency Member
Constituent: Katavi
Political Party: CHAMA CHA MAPINDUZI
Office Location: P.O. Box 980, Dodoma
Office Phone: +255 744 301630
Direct Line Dar. #1 +255 22 2120120
Direct Line Dom #1 +255 26 2321606
Mobile +255 754 301630
Office Fax: 2112538
Office E-mail: mpinda@parliament.go.tz
Member Status: Current Member
Start Date:
End Date:
Date of Birth: 12 Aug 1948


EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
University of Dar es Salaam LLB 1971 1974 GRADUATE


EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
Prime Minister's Office - Regional Admin.& Local Governments. Minister 2006
Prime Minister's Office - Regional Admin.& Local Governments. Deputy Minister 2000 2005
State House Clerk to the Cabinet 1996 2000
State House Assistant Private Secretary to the President 1982 1992
State House Security Officer 1978 1982
Ministry of Justice State Attorney 1974 1978


Source: Parliamentary On-Line Information System (Polis)
 
Ndugu wana JF.

Nimepokea bila mshituko wala msisimko wowote kuwa Mizengo Pinda ameteuliwa kuwa PM.

Kimsingi Pinda ni muadilifu na ana haiba ya 'mtu mwenye kutenda haki'. Tatizo la Pinda ni moja tu: Ni muoga. Chaguo sahihi la mafisadi. Wanataka mtu anayeweza kulia na kutoa machozi kama mtoto mdogo bungeni. PM ambaye mafisadi wakimuamuru 'sema meremeta ni ishu ya JWTZ' akubali na aseme. Au fisadi akimtuma 'muambie Zitto Kabwe hatorudi Bungeni 2010' anasema kweli. Aibu ya TZ.

Tangu ateuliwe 2008, amedhihirisha kuwa ni muoga na kwa hiyo amewafanya WaTZ wakichukie chama chake kwa sababu siyo jasiri. Hawezi kuthubutu. Nathubutu kusema bora Lowasa kuliko Pinda. Ubaya wa Lowasa ni tabia yake ya kufanya ubia na wahujumu uchumi....Wahindi.

Kwa kifupi kuteuliwa kwa Pinda ni muendelezo wa kiduku.

Makinda TV.
Hii ni runinga. Tena runinga ya mbao. Kazi ya huyu maza ni kutafuta vifungu vya kulisha 'ban' wabunge watakao chokonoa maslahi ya waliomuweka. Aibu yetu. Aibu ya Tz.

Skizia baraza la mawaziri. Usishangae kuyakuta majina yafuatayo:

  • Makongolo Mahanga (PhD feki)
  • Zakhia Meghji (WaTz wamesahau madudu yake akiwa hazina)
  • Lawrence Masha (rafiki na kipenzi cha familia)
Kama kawaida. Mkwere anaendeleza harakati zake za usanii kwenye uongozi wa nchi. Katika Zama hizi ambapo Watanzania wanataka viongozi wanauthubutu.

Ndiyo maana mimi ni mfuasi wa Chadema kwa sababu viongozi wake wanathubutu.

Sasa tunaletewa mtu anayetumwa, tena na mafisadi, "kaseme hivi...". Kazi ipo.

Ndiyo maana nathubutu kuuliza, Pinda ni bora kuliko Dr. John Pombe Magufuli?

Nisaidieni.
 
Kuthubutu na kusimamia uthubutu mambo ambayo ni msingi kwa kiongozi yoyote anaeongoza na wananchi kichwani mwake ni hazina na tunu tuliyoikosa katika vinchi vyetu masikini Tz ikiongoza. Mtoto wa Mkulima ni kiongozi mzuri ila udhaifu wake ni "Ndio Mzee" tofauti na magufuli (a.k.a. Caterpillar) ambaye anakamua tu bila kujali we ni nani na ukiingia site yake hata kama baba ako na mama ako ni waasisi wa CCM (TANU) au Tanzania unakunywa mvinyo wa ghadhabu yake
 
john pombe magufuli yuko juu. Tatizo hakuwahi kuwepo kwenye kambi ya kikwete nadhani alikuwa kambi ya SA Salim au sumaye kama sijakosea
 
Kuthubutu na kusimamia uthubutu mambo ambayo ni msingi kwa kiongozi yoyote anaeongoza na wananchi kichwani mwake ni hazina na tunu tuliyoikosa katika vinchi vyetu masikini Tz ikiongoza. Mtoto wa Mkulima ni kiongozi mzuri ila udhaifu wake ni "Ndio Mzee" tofauti na magufuli (a.k.a. Caterpillar) ambaye anakamua tu bila kujali we ni nani na ukiingia site yake hata kama baba ako na mama ako ni waasisi wa CCM (TANU) au Tanzania unakunywa mvinyo wa ghadhabu yake

Ni kweli Magufuli ni Caterpilar la nguvu. Nakumbuka suala la magari la vibosire alivyowaumbua bila kuwaangalia usoni akiwa waziri wa ujenzi. Akiwa waziri wa ardhi na maendeleo ya makazi hata naibuu wake bi. Ritha Mlaki alimweka kwenye orodha ya watu wa kunyang'anywa viwanja kwa kutoviendeleza. Amepewa wizara ya kitoweoo tumeona alivyong'ara huko.

Kitendo cha PInda kutamka hadharani kuwa mafisadi wana nguvu sana na wakiguswa nchi itatetereka ni kauli isiyofaa kabisa kutoka kwa kiongozi mkubwa kama PM na kwa maana hiyo Pinda nafasi hiyo hakuna cha maana anachokifanya zaidi ya kukalia tu hicho kiti bure. Nakubaliana na mtoa mada kuwa ni mara mia ya Lowasa katika utendaji kuliko Pinda, tatizo la Lowasa ni mwizi na kwahilo hafai kuwa kiongozi.
 
Kuna moja imesahaulika:

Akiguswa (albino akikatwa mkono) ANALIIIIIIYA!!!! Kwangu ndo n'chompendea!!!:yield::yield::yield::yield::yield:
 
Kuna shule fulani ya sekondari sitaki kuitaja, mtu akitaka kuingia ****** inabidi aache shati nje ili asije akatoka na harufu mbaya, naamini inabidi Mh. Pinda ashauriwe aache shati nje ya CCM la sivyo atanuka
 
Akina EL na RA wanadai Pinda na mgogoro mbaya wa kiafya. Matarishi wao jana na juzi wameshinda kwenye mabaa mbalimbali hapa Dodoma wakidai "mgogoro" wa afya yake ni mkali sana.
 
Back
Top Bottom