comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Wana jf
Salaam.
Wakala wa Vipimo nchini WMA inakusudia kuanza matumizi ya stika maalumu zitakazotumika kuzitambulisha mashine na vipimo ambavyo vimehakikiwa na mamlaka hiyo.
Bi. Irene John (katikati) akiongea na wanahabari hawapo pichani
Hatua hiyo ni ili kuongeza matumizi ya teknolojia katika kuwalinda walaji na watumiaji wa huduma mbalimbali ambazo huuzwa kwa kutegemea ukubwa, uzito au ujazo fulani wa kipimo.
Kaimu Meneja Elimu, Habari na Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka hiyo Bi. Irene John ametaja vipimo vitakavyowekewa stika hizo kuwa ni pampu za kuuzia mafuta, bohari za mafuta ya jumla, mizani za barabarani, mizani za wafanyabiashara na zile za viwandani, malori ya kubebea mchanga, vifusi pamoja na kokoto bila kusahau mizani za kuuzia mazao ya wakulima.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Wakala hiyo Bi. Stella Kahwa amesema stika hizo zitakuwa zikitolewa bure pasipo malipo yoyote huku akiwataka wafanyabiashara nchini kuzingatia uadilifu kwa kutochezea vipimo wanavyotumia katika biashara yao kwani sheria ya mamlaka hiyo inatoa adhabu kali kwa wahusika wa makosa hayo.
Chanzo: EATV