Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,893
- 16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.
Eti ndugu zangu watanzania;
Upi ni wakati sahihi wa kumsomesha mtoto katika Private School kwa mzazi wa kipato cha chini? Primary Level au Secondary Level?
Ninapoongelea mzazi wa kipato cha chini kwenye muktadha huu nina maana kwamba ni yule ambaye anatamani mtoto wake asome katika Private School ila hawezi kumudu gharama za kuanzia darasa la kwanza mpaka form six. Yeye anaweza kumudu Level moja tu baaas.
Kama mtoto atasoma primary level katika Private School basi secondary level atasomea katika shule ya Serikali na vice versa.
Kuna jirani yangu nipo nae hapa anadai ni bora mtoto aanzie elimu ya msingi katika Private School ili apate msingi bora wa lugha ya kiingereza hata akienda secondary anaelewa masomo kwa ufasaha.
Classmate wangu Beautiful Nkosazana yeye alikuwa anadai eti ni bora mtoto akaanza Primary Level katika shule ya serikali ili akienda Secoary katika Private School anakuwa tayari amekomaa vema kiakili na anaweza kujimudi.
HII IMEKAA VP NDUGU ZANGU?
WEWE UNANISHAURIJE KAKA/DADA YANGU?
OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Primary msomeshe shule za kawaida, Sekondari mpeleke Private, then A-level atajipeleka mwenyewe shule za serikali baada ya kufaulu vizuri Olevel.
Shule ya msingi asome private. Ukiangalia syllabus za primary private zinacover secondary Kwa asilimia zaidi ya 70. Mtafute alie darasa la sita mpe paper za form 2, civics,geography, English, biology uone atakachotenda. Pia secondary hapambani kukariri, lugha anaijua hivyo masomo hayawi magumu sana kwake