Miura aongeza mkataba kucheza soka akiwa na miaka 54

Rukaka2020

Senior Member
Jun 20, 2020
137
632
Mchezaji wa Kijapan mwenye umri mkubwa Kazuyoshi Miura (54) anarudi tena uwanjani baada ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja na club yake ya Yokohama.

Kazuyoshi Miura atatimiza umri wa miaka 54 kamili February 26 2021 ikiwa ni siku moja kabla ya kuanza kwa msimu wa 2021 wa Ligi Kuu Japana (J-League).

Huo utakuwa ni msimu wake wa 17 akiwa na club ya Yokohama toka pale alipojiunga nayo 2005.

Mara ya mwisho Miura anafunga goli ilikuwa 2017 dhidi ya Thespakusatsu Gunma katika Ligi daraja la pili na kuandika rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa (miaka 50 na siku 14) kufunga goli katika professional League nchini Japan.

WACHEZAJI WETU SIJUI WANAKWAMA WAPI?????
Screenshot_20210112-183047_1.jpg
 
Back
Top Bottom