Miundombinu ya Barabara viwango vya lami Vijijini zinasahaulika

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,257
Ukweli ni kwamba maisha ya mjini yanategemea sana maisha ya watu wa vijijini, vijijini ndo kwenye lishe, utajiri na mali ghafi zote Muhimu kwa nchi nzima na hata nje ya nchi. :

Lakini tatizo linakuja pale barabara za mjini tu ndo zinazingatiwa haswa katika uwekaji wa Lami lakini sehemu nyingi za vijijini hakuna miundombinu ya barabara za Lami zinazowezesha usafirishaji wa malighafi, chakula pamoja na bidhaa kutoka vijijini na kwenda mijini.

Ukosefu wa miundombinu ya barabara huko vijijini imesababisha wakulima kulima kwa kiwango kidogo (small scale agriculture) badala ya kilimo kikubwa (large scale agriculture ) hivyo basi wakati mwingine kupelekea Kukosekana kwa chakula au uhaba wa chakula,

Ukosefu wa miundombinu hasa ya barabara hupelekea nguvu kazi muhimu hasa ya vijana kukimbilia mjini kutokana na ukweli kuwa miundombinu ya vijijini na mjini ni vitu viwili tofauti yani ni Kama maji na mafuta.

Kutokana na ubovu wa barabara za vijijini wengi wenye magari ya kubeba mizigo au malighafi hugoma kupeleka magari yao vijijini kutokana na kuhofia magari ya kuharibika huko, changamoto hiyo humfanya mkulima kujilimia mazao yake kiasi kwa kuogopa hasara.

Ujenzi wa miundombinu mizuri huku vijijini itawafanya hata idadi ya wamachinga mjini ikapungua pamoja vijana waliokosa ajira kukimbilia vijijini kulima kutokana na ubora wa miundombinu rafiki.

Ni wakati sasa Serikali yetu pamoja na wabunge wetu hasa wa majimbo ya vijijini kupiga kampeni ya ujenzi miundombinu ya barabara za vijiji vyote kwa kiwango cha Lami.

chncdhaHR0cDovL3dpa3JleHBvcnQuY29tL3dwLWNvbnRlbnQvdXBsb2Fkcy8yMDE2LzA4L3JvYWRzLWFmcmljYS10ZXJy...jpg
 
Barabara ya sengerema buchosa hadi nzela imekufa na JPm, manake hela za ujenzi walizijua mfugale na JPM, barabara ya Geita kahama hamnazo
 
Ukosefu wa miundombinu ndo kichocheo
Barabara ya sengerema buchosa hadi nzela imekufa na JPm, manake hela za ujenzi walizijua mfugale na JPM, barabara ya Geita kahama hamnazo

cha umaskini.
 
Back
Top Bottom