Uchaguzi 2020 Miundombinu kila mtu anaweza kujenga, ugumu wa kazi ya Urais uko hapa...

kagoshima

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,629
5,134
Habari wakuu. Ugumu wa kazi ya Urais upo katika maeneo haya yafuatayo:

1. Kuwaunganisha watu,
2. Kuwafanya majority wawe na furaha na nchi yao
3. Kuboresha uchumi wa raia maana ndio tegemeo lao kuu walipo kuchagua.
4. Usalama wa raia,
5. Huduma bora za afya, maji, elimu, umeme
6. Uhuru kwa kila raia bila ubaguzi
7. Haki kwa kila raia bila ubaguzi
6. Na mengine mengi yanayomfanya raia afurahie maisha.
Ukweli ni kwamba hayo yote yalikosekana awamu hii ya uongozi wa JPM. hii miundombinu; barabara sijui madaraja nk imekuwa ikijengwa tangu Mkapa ,Kikwete na sasa Magufuli kuonyesha kwamba hiyo sio issue sana. Ni kazi ambazo lazima zifanyike ila bonus ya kwanini watu wafurahie serikali yao IPO kwenye Yale pale juu.

Mkapa alijenga barabara nyingi sana kujaribu kuunganisha mikoa, pamoja na dimba la Mkapa. Kikwete alijenga barabara nyingi, universities, madaraja nk.

So issue sio kujenga hiki wala kile maana kila atayepewa ikulu atajenga tu?

Ugumu wa upo katika kuwatimizia mahitaji yao waliokuchagua, tufanye chaguo sahihi 2020.
 
Back
Top Bottom