Miundo mbinu ya Tanzania.

Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
681
126
Jamani kuna picha nimeiweka hapa chini nisaidieni kuibandika (mimi sijui kubandika picha JF)

Ukiangalia hiyo barabara na hayo magari kweli unaweza kuikana hata nchi yako. Hivi kweli maisha bora hata barabara za mikoani tuu tunashindwa kuweka hata changarawe? Tunazunguka kutafuta wawekezaji hivi ni mwekezaji gani atawekeza sehemu kama hizi za Kigoma japo kuna opportunities nyingi?

Hii bara bara inanikumbusha siku moja nilikuwa naenda Lindi na Mtwara tukalala Nangurukuru siku 3.
 

Attachments

  • NJILI_pics+073.jpg
    NJILI_pics+073.jpg
    16.6 KB · Views: 227
Mtoto wa Mkulima unanifurahisha sana. Kitu cha kwanza ninachokiona hapo mimi ni hali ya hao kaka zangu na wadogo zangu, magari na barabara sivizingatii sana, unajua hao ndugu zetu wako hao sana, kama kungekuwa na lolote serikali ingeanza na hao kwanza megine baadaye, najua baadhi ya watu wanaweza kusema ingeanza na barabara kwanza, kwa sababu bila barabara hakuna linaloweza kufanyika. Barabara nyingi zinazotengenezwa inakuwa nightmare,
 
Mtoto wa Mkulima unanifurahisha sana. Kitu cha kwanza ninachokiona hapo mimi ni hali ya hao kaka zangu na wadogo zangu, magari na barabara sivizingatii sana, unajua hao ndugu zetu wako hao sana, kama kungekuwa na lolote serikali ingeanza na hao kwanza megine baadaye, najua baadhi ya watu wanaweza kusema ingeanza na barabara kwanza, kwa sababu bila barabara hakuna linaloweza kufanyika. Barabara nyingi zinazotengenezwa inakuwa nightmare,

Ni sawa lakini mkuu umeona hiyo bara bara mwenyewe? usiombee yakukute wakati unasafiri mkuu.
 
Noma.
Katika kazi zangu Tanganyika vijijini, hiyo ni cha mtoto. Yaani kuna mahali barabara ni mbovu na nyembamba, hata pick ups hazipishani, achilia mabasi kama hayo pichani. Aliyefika wilayani kilindi mkoani tanga anaelewa ninachosema, ama aliyefika Ambangulu Korogwe wakati wa masika nadhani ananielewa pia.
Barabara.jpg


Hiyo ni miaka 46 ya uhuru.
*Ni maisha bora kwa kila Mtanzania
*Ni Tanzania yenye neema
*Ni Ari mpya, nguvu mpya, na kasi mpya.
 
Noma.
Katika kazi zangu Tanganyika vijijini, hiyo ni cha mtoto. Yaani kuna mahali barabara ni mbovu na nyembamba, hata pick ups hazipishani, achilia mabasi kama hayo pichani. Aliyefika wilayani kilindi mkoani tanga anaelewa ninachosema, ama aliyefika Ambangulu Korogwe wakati wa masika nadhani ananielewa pia.
Barabara.jpg


Hiyo ni miaka 46 ya uhuru.
*Ni maisha bora kwa kila Mtanzania
*Ni Tanzania yenye neema
*Ni Ari mpya, nguvu mpya, na kasi mpya.


Ni noma naona maengeleo yetu yanakuwa but negetive growth. Kweli niaka 40 ya kujitawala bado mambo yako hivi? Tunawatu, rasilimali, amani, climate nzuri tuu, STrategic geographical location nzuri except siasa safi na uongozi bora wenye vision ndio tumeukosa.
 
Halafu uliza nauli ya kutoka Dar mpaka huko yanakoelekea mabasi hayo, utachoka.
Huku hakuna mtu atapeleka marcopolo yake, huena isirudi. Yataendelea kwenda malori tu.
 
Mi nashangaa pale nilipowahi kumsikia Mramba akisema kuwa tutajenga treni za umeme, sasa sijui kama barabara tu imewashinda, mabehewa ya treni za sasa yamewashinda hata kuweka viti, je hizi kama sio ndoto za Alinacha ni nini wana JF..?? Kingine cha kusikitisha, kuna waziri ambaye mpaka sasa nakosa jibu aliupataje hali hajui lolote kuhusiana na finance issues, aliwahi kutetea kupanda kwa kodi ya mafuta akidai kuwa itatumika kutengeneza barabara kitendo cha kupelekea fuel costs kwa watanzania kushuka (suprising, and embarassing kwa mtu mkubwa kutoa multiplier effect ya ki-layman namna hiyo).

Mi nafikiri sasa kuna haja ya kumtafuta Magufuli wa pili ili awekwe kwenye wizara ya miundo mbinu, manake huyu mheshimiwa alijitahidi sana enzi za cheo chake katika wizara hii. We want people kama yeye. Hii mambo ya kuweka the so called "figure head" katika wizara badala ya active persons (hasa kwa wizara sensitive kama hizi) ni kuwatesa wananchi tu. Tulimuona Magufuli alivyokuwa anajua mpaka kilometa ambazo hazina lami na alikuwa anaweka clear mipango ya wizara na utekelezaji wake ulikuwa unawapa matumaini wananchi. I don't mean kuwa namshabikia Magufuli, no please, narecognize mtu akifanya kazi (visible stuff).
 
Halafu tusiende mbali, kwa wakazi wa Dar, nafikiri tunaona michezo na matumizi mabovu ya kodi katika utengenezaji wa barabara. We imagine barabara za ndani kama maeneno ya kijitonyama mpaka mwananyamala, kila mara nasikia wanazichonga tu. Na haipiti wiki, zimegeuka mapango tena. Sasa huu mchezo wa kuchezea pesa kwa kuchonga barabara kila siku hali wangekuwa wamejikusanya na kuweka walau lami chakavu. Sasa kama mjini tu wanashindwa kuwa serious, ije vijijini ambako wananchi wake wameshakubali matokeo ya shida za umaskini wa nchi yao..?? Manake huku mjini ndiko viongozi, au ndugu au marafiki zao wanaokaa nao kwenye vikao vya starehe wanapita kila siku, na wanaona matokeo ya kodi zinazotumika kwa matengenezo ya barabara za ndani but they keep quite. We barabara ya Shekilango ilichukua muda gani? Barabara ya Sam Nujoma imechukua muda gani? Mapango ya barabara ya Mandela (tena inayoelekea airport) ina mapango kiasi gani na cha kuchekesha ni kuwa, hao viongozi wanapokuwa wanaelekea airport huwa wanathubutu kuikwepa hiyo barabara ya mandela na kupita pugu road, ikiwa ni ishara kuwa wanafahamu mapango hayo but they seek an alternative itakayowakwepesha waki-assume kila mtanzania wa dar atakwepa mapango kwa kupita pugu road.

Ninachokimaanisha hapa, ni kuwa hawa viongozi wanathubutu kujifanya hawaoni mapango yaliyo jirani nao (huku Dar) sasa ya huko porini si ndio watajifanya hawasikii wala hawasimuliwi..?? Hawa viongozi wanahitaji kufanya kazi ya ziada kwa kweli, manake wananchi tumechoka choka.
 
@Kishazi
Hakuna atakayekushangaa kwa kumsifia Magufuli, kwani aliyoyafanya mazuri yalionekana. Ukiachilia mbali kukariri kwa kichwa kilometa za barabara kuu za Tanzania nzima, jamaa huyu aliweza kuwanyang'anya magari ya serikali wale waliokuwa wajitwalia bila aibu, mpaka wakamtishia maisha. Kwa mwingine hili suala lingekuwa gumu sana kulitekeleza. Kumbuka kuwa ni Magufuli aliyetoa amri ya kuwakata malipo makandarasi wababaishaji kule Singida, baada ya kuchelewa kumaliza barabara. Jamaa aliiweza barabara, sema tu walimpakazia zigo lisilobebeka la kuuza nyumba zetu, ndilo ambalo limemchafua sana. Otherwise ile ndoto yake ya Mtanzania kusafiri kwa taxi toka Mtwara hadi Mwanza nadhani ingekuwa imeshatimia.
Mramba bomu sana, pesa zote za barabara kakimbizia kwake Rombo, mpaka Mbunge mwenzie Lucas Selelii akalalamika wazi bungeni.
 
Hiyo barabara Mramba lami Rombo- mbona siasa tu! Hakuna chochote- wala hakuna cha lami- ni siasa tu- hizo pesa zimepelekwa Rombo lini mtu alienda huko aseme kama kuna lami- ni ahadi tu miaka 10 sasa!
 
Kabla ya kututoka Mwl alisema akifa tutamkumbuka. Wakati hule sikuweza kuelewa kwa sababu nilijua watanzania tupo wengi na tusingekaa na kumfikilia mwalimu. Lakini tangu serikali hii ya nne ilipoingia na ubabe fulani uliyoonyeshwa na serikali ya tatu ndipo nikatambua kuwa mwalimu alitambua fika kuwa aliacha watu walafi wenye kupenda sifa waliokuwa na tamaa ya kuingia ikulu pasipo kuwa na nia dhabiti ya kuendeleza taifa ili. Mwalimu aligundua ni jinsi gani tamaa ilitawala kundi kubwa la viongozi. Mwl alitambua umbumbumbu wa watanzania na ile imani ya undugu kuwa ingewapelekea kumchagua mtu asiyekuwa na sifa, mtovu wa maadili asiyeijua nchi na mwenyeupeo mdogo kuchukua dhamana ya kuendeleza Taifa hili.

Mwalimu hata wakati wa uhai wake alitamka kuwa watanzania tulipaswa kuwaogopa kama ukoma wale waliokuwa na tamaa ya kuingia ikulu kwa mapesa na mbinu nyingine chafu. Pia baba wa Taifa alisema IKULU si maala pa kukimbilia. Ikulu si maala pa mchezo. Ni maala pagumu sana. Hupati usingizi ukifikiria shida za watu wako.

Pamoja na yote aliyonena Mwl. Watanzania tumetoa nafasi kwa mtu ambaye alionyesha tamaa kubwa ktk umri mdogo wa kuichukua nchi. Na hata aliposhindwa 1995, mwaka 2005 mtu huyu alikuja kwa namna ya pekee akionyesha tamaa kubwa ya kuingia ikulu huku akiwa na kundi kubwa la marafiki wenye pesa na pia kuzungukwa na watendaji wabovu. Mtu huyu ujiosha machoni mwa watanzania na kujivua pale lawama zinapotolewa na kusukuma mzigo kwa watendaji wake. Ni ndani ya miaka 2, mh. huyo anaitangazia dunia kuwa hajui ni kwa nini nchi ambayo yeye anaiongoza ni maskini licha ya kuwa na mali lukuki. Nilifikiri ili ni swali ambalo kabla ya kuitaji kura zetu alikuwa amelipatia jibu na tayari alikwisha andaa namna ya kutatua. Kwa wakati huu ambapo mweshimiwa hajui je watanzania tutarajie nini wakati tatizo letu ni umaskini?

Ni katika bunge la budget la mwaka huu ilidhihirika kuwa serikali haikuwa imejenga barabara mpya hata km 1. Na ni miezi 5 kwa sasa tangu budget ya 2007/2008 ipite huku serikali ya nne ikisifiwa kwa kuweka kipaumbele kwenye barabara kwa kutenga mabilioni ya fedha lakini mpaka sasa tunaongea swala la kupata makandarasi, je kazi itaanza lini wakati inatambulika fika kuwa mwaka jana miundo mbinu yetu iliaribiwa na mvua kubwa? Mikakati ya budget kwa 2008/2009 imeanza huku tukishindwa kusimamia utekelezaji wa budget iliyopo. Swala la kujiuliza je, fungu lilitengwa kwa ualisia wake au ilikuwa kiini macho ili kuondoa aibu kwa serikali baada ya kubanwa na mh Zitto? Tuwe macho maana longolongo na sifa zimezidi. Tunaweza hata kupewa budget hewa ilimradi tu wajisifu.

Ni kweli miaka 46 tangu tujipatie uhuru. Leo hii kuna baadhi ya maeneo hapa Dar unakuta alama ya lami mitahani kuonyesha kuwa Mwl aliweka kipaumbele kuifanya Dar na maeneo mengine kuweza kufikika. Ilikuwa ni matarajio yetu kuona viongozi waliomfuata kutia msukumo zaidi. Lakini ukiachilia mbali mipangilio dhabiti iliyowekwa na Mzee wetu Ruksa na jitiada zake za kuomba fedha nje ambayo ndiyo haswa ilikuja kusimamiwa na Ben hakuna tena mikakati hiyo na usimamizi ulimefikia ukingoni. Upcountry kumeachwa tupu. Tambua Ben kwa kutambua kuondoka kwake ikulu basi hakuacha mipangilio bora na hata fedha akazipitishia mlango wa nyuma ili kujiandaa kuwa chinga mtaani na si rais mstaafu.

Nafikiri imefikia hatua serikali kuu kupunguziwa kabisa uwezo wa kumiliki kodi za nchi hii na badala yake kuwepo na uwiano wa mgawanyo moja kwa moja from source wa kodi, mikopo na misaada ili halmashauri ziwezeshwe kusimamia miundo mbinu wakiwa na fungu kuliko hivi sasa. Lakini pia lazima jina la mh lijumuishwe na matokeo mabovu ya serikali yake badala ya kumsifia na kufikiri mbovu ni Edu, kara na wengine. Yeye ni kichwa, alivua nguo mwenyewe kwani hakujua maji yalikuwa ni ya baridi matokeo yake anagoma kuyaoga? Thanks JF

TANZANIA INA NEHEMA TANGU ENZI INAITAJI WASIMAMIZI WAWAJIBIKAJI NA WENYE KUIONA MAANA IMEWEKWA NA MWENYEZI NA SI WALE WANAOTAKA KUITAFUTA KWA NJIA ZAO ZA KIBINADAMU.

Jamani kuna picha nimeiweka hapa chini nisaidieni kuibandika (mimi sijui kubandika picha JF)

Ukiangalia hiyo barabara na hayo magari kweli unaweza kuikana hata nchi yako. Hivi kweli maisha bora hata barabara za mikoani tuu tunashindwa kuweka hata changarawe? Tunazunguka kutafuta wawekezaji hivi ni mwekezaji gani atawekeza sehemu kama hizi za Kigoma japo kuna opportunities nyingi?

Hii bara bara inanikumbusha siku moja nilikuwa naenda Lindi na Mtwara tukalala Nangurukuru siku 3.
 
Agao Kichore,
Wakati wa Nyerere miaka ya mwanzo 1980s barabara zilikuwa zimechoka sana- afandhali hata sasa! Mashimo makubwa makubwa barabara kuu ilikuwa kawaida!
Maboresho ya barabara yalianza wakati wa mzee ruhsa, na kasi kubwa wakati wa Mkapa kwa kusimamiwa na Magufuli- hii kasi wakati wa JK inaonekana imepungua tena sana!

Maneno mengi tu- matamu na ahadi- but where is the output ktk barabara? Good thing with BWM ahadi kidogo na vitendo vingi!
 
Picha hizi zinaonyesha hali halisi ya usafiri na usafirishaji ilivyo nchini Tanzania. Kwa wale mliokulia kwe maeneo yenye kupunga upepo mzuri....eg Oysterbay..ni ngumu kwenu kuelewa picha kama hii kuwa imepatikana Tanzania. Sisi tunaoyajua vizuri tunaona ni mambo ya kawaida. Ukweli uko pale pale kwamba barabara yeyote bila lami, mvua ikinyesha hakieleweki. Na si tu kwamba usafiri unakwama bali hata maisha ya watu kuwa hatarini. Ukiangalia hizi picha na magari yalivyokaa unashindwa kuamini kwamba kweli dereva aliamua kujitosa kwenye tope hilo hata kama abiria waliterememka.
Kuna haja ya serikali kuangalia sana katika upande barabara. Tusisahau kwamba maaendeleo ya nchi yetu yanatokana na resources zinazopatikana huko vijijini. Sasa hali kama ni hii tutafika kweli. Ndugu zangu hasa wewe uliyeleta picha hizi, nakushukuru sana, maana tunaona hali halisi ya miundo mbinu yetu. Wizara hii imeongezwa ili kuboresha hali, lakini ukweli naona barabara za mjini ndio bado zinapewa kipaumbele. Wazalendo kazi ipo.
 
Hatuwezi kumsifia magufuli bila ya kumlaumu kwa kuuza nyumba za serikali.Kwa mtu mwenye uchungu na mali za Watanzania ni kufuru aliyoifanya Pombe Magufuli ya kuuza maekari ya Viwanja pamoja na majumba yake hasa yale ya Oysterbay na Msasani kwa bei ya kupeana.Kwa hilo hata kama alishauriwa vibaya angeomba Ushauri zaidi.
Jamani hilo la mramba kupeleka hela Rombo sioni kama ni la msingi kwa kuwa rombo ni sehemu ya tanzania ambayo pia inahitaji maendeleo.Hatuna majimbo tanzania, maendeleo ya sehemu moja ya nchi ni ya watanzania wote.Huwezi kupeleka maendeleo sehemu zote kwa wakati mmonja kama ndoto Ya JK.Barabara ya Rombo inajengwa na sasa imeshaanza na kwa kasi ya ajabu.Pole sana kwa kupewa ripoti ya barabara ya rombo kwa kuwa inaelekea hutaki warombo wapate lami.
 
Hiyo barabara Mramba lami Rombo- mbona siasa tu! Hakuna chochote- wala hakuna cha lami- ni siasa tu- hizo pesa zimepelekwa Rombo lini mtu alienda huko aseme kama kuna lami- ni ahadi tu miaka 10 sasa!

Ok, sasa kama hali ni hiyo, kwa nini mbunge Lucas Selelii alikuwa akimlalamikia waziwazi Mramba bungeni kuwa kajipendelea jimboni kwake? Na ni kwa nini wabunge wa sisiemu walimuunga mkono Selelii palepale?
Tunaomba jibu.
 
Ok, sasa kama hali ni hiyo, kwa nini mbunge Lucas Selelii alikuwa akimlalamikia waziwazi Mramba bungeni kuwa kajipendelea jimboni kwake? Na ni kwa nini wabunge wa sisiemu walimuunga mkono Selelii palepale?
Tunaomba jibu.

IDIMI,
Ni ahadi tu za CCM kama ahadi zingine! Kwa nini hadi sasa hakuna barabara na Wabunge walimuunga Mkono pale pale sijui- ni barabara chache sana zinazoongelewa kiukweli ukweli huwekwa lami- huenda serikali haina pesa!
May be tuvute mda!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom