Miundo mbinu ghali isifunguliwe bila ya watu kupewa elimu pana juu ya matumizi na utunzaji

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Niliwahi kushuhudia kituko kimoja miaka ile wakati uwanja wa taifa ukiwa bado mpya. Jamaa wakati wa mapumziko ya mechi alikwenda kujisaidia haja ndogo kwenye sinki la maji, wakati sehemu za kujisaidia zipo, na hajazuiwa kuzitumia!. Kitendo kile kilikera watu wengi na ilikuwa ni bahati nzuri kwa yule jamaa, kwani polisi waliwahi kumuokoa ili asipate kipigo kutoka kwa mashabiki wenye hasira.

Juzi juzi tu baada ya daraja la Mwalimu Nyerere kufunguliwa, dereva wa lori lenye mzigo wa zaidi ya tani 10 kataka kukatiza, na akakamatwa, anaulizwa kwanini anataka kupita na mzigo mzito ambao unaweza kuchangia katika kuua daraja lenyewe, akasema alikuwa hajui ni mipaka halisi ya wingi wa tani za mzigo ambao iwapo gari litazidisha basi halitakuwa na haki ya kulitumia daraja lile.

Wazungu wanasema ignorance is not an excuse, na ujinga huo huo wa mtu ndio unaoweza kumfanya akakutwa na hatia mahakamani.

Ushauri wangu kwa serikali, kabla miundo mbinu ya gharama haijaanza kutumiwa, ipo haja ya kutumia TV, vipindi vya radio na hata vipeperushi vya njiani, vyenye kuelezea matumizi ya miundo mbinu. Ipo haja ya kuongeza jitihada za uelimishaji wa jamii nzima ili ujinga usitumike kama kisingizio cha miundo mbinu kuharabiwa mapema.

Mdogo mdogo lakini ipo siku tutafika.
 
Watanzania hatusomi magazeti,vitabu,vipeperushi wala kutazama Tv ukimkuta mtu ana smartphone basi yeye na Instagram sasa sijui utatupatia wapi utupe elimu pengine uandae show ya diamond vs kiba hapo unaweza kutueleza jambo
 
Hilo haliepukiki kbs! kama tunataka miundombino idumu lazima tuelimishe watu vya kutosha kbs
 
Back
Top Bottom