Miujiza ya Mungu kwa Tundu Lissu, COVID-19 na Siasa za Tanzania yetu

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,989
22,521
Wanajamvi,

Kwanza kabisa, niseme kama COVID-19 ingekuwa mbaya Tanzania, Lissu asingepata huu umati wa ajabu wenye Watanzania wenye hamasa ambayo sidhani kama nimeshawahi kuiona kwenye siasa za Tanzania. Hili ni la kumshukuru Mungu! Amejibu maombi kwa namna ya ajabu kabisa!

Amejibu maombi kwa namna ya ajabu, sambamba na kufanya muujiza mkuu kwa maisha ya Lissu. Hili, ni pamoja na kwamba maombi ya kumuombea ndugu Lissu ili Mungu amuepushe na mauti iliyokuwa ikimkabili, yalizuiliwa na serikali ambayo juzi tu rais amepewa “tuzo ya corona”🤦🏾‍♂️ Hili hata yeye mwenyewe “alijihisi”, akasema “tuzo hii ni ya Mungu”.

Lissu nimemsikia akizungumza yote yaliyotokea baada ya kutaka kuuwawa kwa kumiminiwa risasi 16 mwilini! Lakini sijamsikia akigusia hili la wananchi kuzuiwa kumuombea! Kwa wengi wenye imani, limetushangaza sana! Makanisa haya haya, yamesahau? Kwa sababu hata dini zenyewe zinatutaka tuwaombee wote! Hata wale waliotukosea! Lakini kwenye hili la kushambuliwa kwa Lissu, hayo makanisa yalikuwa kimya! Na juzi yakaibuka na issue ya “Amani”, lakini hawataki haki! Ndiyo maana dhuluma na kila aina ya uchafu na wachawi wamejaa kwenye nyumba za ibada!

Sasa kwenye siasa za Tanzania, ulianza muujiza wa Lissu, kisha wa Corona, halafu sasa ni siasa za Tanzania! Kwa wale ambao watakuwa wameshasoma maandishi yangu humu, nilisema kitambo kabisa kuwa “siku Tundu Lissu akitua nchini, basi siasa za Tanzania zinabadilika papo hapo”.

Kinachotokea sasa ni muujiza mwingine! Mungu akitupa uzima, hii thread mtaniambia kama Lissu haendi Ikulu. Najuwa wengi watabeza! Lakini “time will tell”, tena siyo muda mrefu! Nimeona hamasa ya vijana wa Tanzania, wakike kwa wakiume! Wababa watu wazima, wazee, na wamama wengine wamebeba watoto migongoni wakihatarisha usalama wao na watoto wao! Wakiwa na hamasa ya kumona tu na kumsikia Lissu! Kwenye video clip moja, nimeona wakiimba kwa hamasa ya hali ya juu sana! Wakisema “Hatuogopi bunduki”. Sijui kama ni kule Mbozi ambapo OCD alitaka kuwazuia wananchi kwenda kumuona Lissu! Baadaye akagwaya kwa “nguvu ya umma”.

Kwa wale viongozi wa dini, nadhani wapokee ushauri wa Dkt. Bagonza, kwamba “Amani ni tunda la Haki”

Kwa wale wanaobeza, naomba watambuwe kuwa, salama ya Taifa letu, ipo kwenye “uchaguzi huru na wa haki”.

Niishie hapa kwa sasa, nikiamini kwamba, wale wote watakaoinuka kinyume na nguvu za haki ya Mungu wa miujiza, wataangamia!
 
Ambacho hujaweza kugundua katika kufuatilia kwako ni kwamba, tangu Lissu ameanza kusikika, hajawahi kusikika akitaja mambo ya Mungi latika maongezi na harakati zake, lakini this time tangu amerudi, haijapita siku kila aendapo ipite bila kusikika akimtaja Mungu.
 
Tundu Lissu namsikia akizungumzia yote aliyofanyiwa na serikali ili kuendelea kumuhujumu ikishirikiana na wasiojulikana, Job Ndugai et al! Lakini sijamsikia akizungumzia la wananchi kunyimwa kumuombea!

Hata la kuzuia asichangiwe damu, kwa watanzania, linawaumiza sambamba na kunyimwa kumuombea! Watumishi wa Mungu wamekuwa Mungu hata wahukumu na kuona ni sahihi?🤦🏾‍♂️

Mh Lissu asiaahau kuzungumzia hili, kwamba “Mungu si Athumani”, Kwani yeye ndiye aliyetenda muujiza kabla hata serikali haijazuia wananchi kumuombea Tundu Lissu! Ubinadamu uko wapi?
 
Nimemsikia sana! Lakini sijamsikia akizungumzia hilo la serikali kuzuia asiombewe! Labda ni kwasababu hakuwepo, na hafahamu ni kwa namna gani wananchi waliguswa na jambo hili!

Nakumbuka kuna vijana walipigwa sana na kuwekwa ndani kwasababu ya kuvaa T-shirts zenye kusema “Pray for Lissu”, haya makanisa hayakumuombea, bali wananchi kila mmoja kwa imani yake.

Na muujiza wa kweli ukatendeka, halafu tena muujiza wa corona ili kumuwezesha kuwafikia wananchi bila taabu! Mungu ni mwema kabisa!
 
Nimemsikia sana! Lakini sijamsikia akizungumzia hilo la serikali kuzuia asiombewe! Labda ni kwasababu hakuwepo, na hafahamu ni kwa namna gani wananchi waliguswa na jambo hili! Nakumbuka kuna vijana walipigwa sana na kuwekwa ndani kwasababu ya kuvaa T-shirts zenye kusema “Pray for Lissu”, haya makanisa hayakumuombea, bali wananchi kila mmoja kwa imani yake. Na muujiza wa kweli ukatendeka, halafu tena muujiza wa corona ili kumuwezesha kuwafikia wananchi bila taabu! Mungu ni mwema kabisa!
Hilo aliliongelea pia.
 
Mara zote Mungu huwasimamia wale waliotaabika pindi aliyewatesa akineemeka kwa raha zake, wanaccm wanampa taarifa za ndani ya CCM kampeni zikianza rasmi ataongea vyote ikiwemo njama ya kaijage wa Tumeccm ya uchaguzi kutaka kuengua jina lake kwa njia haramu za kishetani.
 
Hii ni kali!😳
 
Duh!

Naona makamanda washaanza kukubali kuwa COVID-19 si hatari kama tulivyoaminishwa 🤣🤣🤣
 
Duh!

Naona makamanda washaanza kukubali kuwa COVID-19 si hatari kama tulivyoaminishwa 🤣🤣🤣
Sidhani kama umeelewa muktadha wa hoja. Nadhani umesahau Magu alienda kuji ficha kwa muda! Yeye mwenyewe alisema wananchi waombe tu! Aliepuka kama kawaida yake.

So I was talking about a miracle. And more to come. Kwani hata rais si alisikilizia kwanza? Alipoona Poa ndo akaibuka na yeye! Lakini kwasababu alitaja “Mungu”, wale “wajasiria dini”, wakadandia.
 
Tundu Lissu namsikia akizungumzia yote aliyofanyiwa na serikali ili kuendelea kumuhujumu ikishirikiana na wasiojulikana, Job Ndugai et al! Lakini sijamsikia akizungumzia la wananchi kunyimwa kumuombea!

Hata la kuzuia asichangiwe damu, kwa watanzania, linawaumiza sambamba na kunyimwa kumuombea! Watumishi wa Mungu wamekuwa Mungu hata wahukumu na kuona ni sahihi?🤦🏾‍♂️

Mh Lissu asiaahau kuzungumzia hili, kwamba “Mungu si Athumani”, Kwani yeye ndiye aliyetenda muujiza kabla hata serikali haijazuia wananchi kumuombea Tundu Lissu! Ubinadamu uko wapi?
Binadamu tunatofautiana uwezo wa kufirikiri kwasababu tulio wengi niwavivu wa kufikiri 'We differ in thinking capacity because we do not excercise much of our brains'
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom