Miujiza hiyoo Jamani Ehhh

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,041
Miujiza


pix.gif

Na Imelda Mtema
Katika hali iliyotafsiriwa kama miujiza, kijana mmoja aitwaye Ramadhan Masta, amegeuza jeneza kuwa makazi yake ya kudumu kwa kwa kile alichosema kwamba hana sehemu ya kuishi kwa sasa...


pix.gif

Masta anaishi katika jeneza hilo, aliloliweka juu ya mawe eneo la Kipawa, Ilala, jijini Dar es Salaam, sehemu ambayo ilikuwa na makazi ya watu kabla ya bomoa bomoa iliyowahamisha kupisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Juzi, Jumanne, Mwandishi Wetu akiwa anapita eneo hilo alishuhudia kijana huyo akitoka ndani ya jeneza hilo, ndipo aliposhawishika kusogea eneo la tukio ili kujionea.

Awali, Paparazi Wetu alianza kuhisi kijana huyo hakuwa na akili nzuri, lakini alipopokewa na salamu ya: “sister mambo vipi? Karibu home...” ndipo akagundua kwamba mshkaji alikuwa mzima wa kila idara.

Amani lilipata bahati ya kufanya naye mahojiano, ambapo alisema kwamba, amelazimika kugeuza jeneza hilo makazi baada ya nyumba yake ya urithi kubomolewa na serikali.

“Sina mahala pa kuishi, unajua sisi hatuna mali. Siyo matajiri, urithi pekee ambao niliachiwa na wazee wangu ni nyumba ambayo ilikuwa ikinisaidia vijisenti vya kuendesha maisha yangu, lakini imebomolewa.


“Mbaya zaidi, fidia niliyopewa haitoshi kabisa kujenga nyumba nyingine, nikaona bora nijipumzishe hapa,” alisema Masta akionesha umakini.

Akaongeza: “Nina amani sana niwapo ndani ya jeneza, kwani najua hakuna kitu chochote kitakachonidhuru, nitakaaa hapa hadi rais Jakaya Kikwete atakapopita anione.”

Alipoulizwa kuhusu sehemu aliyotengeneza jeneza hilo, Ramadhan alisema alilichukua katika msikiti wa eneo hilo wakati bomoa-bomoa ikiendelea.

“Nililichukua msikitini, akili yangu ilifanya kazi fasta sana, nilipoliona nikajua dili. Nikafikiria kuhamishia makazi yangu humo,” alisema kijana huyo ambaye ni mchangamfu.


Aidha, kwasasa Ramadhan anajipatia mkate wake wa kila siku kwa kuuza mabaki ya milango, mabati na samani nyingine alizokusanya katika eneo hilo.

Baadhi ya watu ambao wanafanya naye kazi hiyo, walimwambia Mwandishi Wetu kwamba, rafiki yao hana matatizo ya akili ila ameamua kuishi katika jeneza hilo kwasababu makazi yake yalibomolewa.

“Hajawahi kujuta hata siku moja kuishi ndani ya jeneza. Ana furaha kama kawaida na maisha yanakwenda. Mwenyewe anasema yupo sehemu salama,” kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Luna alisema.

Mwingine alisema: “Nahisi yupo sahihi kufanya hivyo, hata kama watamlazimisha aondoke, aende wapi sasa wakati nyumba yake wamebomoa na pesa waliyompa haitoshi? Acha mwana aendelee kusongesha laifu.”

Hivi karibuni eneo la Kipawa, jijini Dar es Salaam lilivunjwa ikiwa ni agizo la serikali kwa ajili ya wakazi hao kupisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
 
Mungu akusaidie kaka uondokane na maisha ya kuishi kwenye jeneza ili hali bado uko hai.
 
hana jipya huyu, ni comedian tu...kwanza anapoingia kwenye hilo jeneza anacheeeka, hadi anaondoa mvuto wa shida aliyonayo!
 
Ama kweli dunia ina mambo maana jeneza kuliona tu moyo wangu hustuka seuza kuwa kibaraza afterthen kaliokota masjid likiwa lishasafiriji abiria wa kumyaga duh pole jah man
 
Waarabe wana msemo wao mmoja unaosema hivi "al junuun funuun" yaani uwandazimi una mafungu mengi, si lazima mtu avae nguo chafu ndio aitwe kichaa, hata anaofanya huyo mtoto pia ni ukichaa
 
Hiyo bangi anayovuta aache mara moja,hapo bado atatembea bila nguo muda si mrefu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom