elivina shambuni
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 461
- 295
KAMA unatumia mtungi wa gesi ya kupikia nyumbani kwako, basi fahamu kwamba mtungi huo umeundwa nje ya nchi. Lakini muda si mrefu, mitungi ya aina hiyo itaanza kutengenezwa Tanzania na gharama zake zinatarajiwa kuwa nafuu kuliko ilivyo sasa.
Akizungumza katika Maonesho ya Viwanda Mkoani Pwani, Meneja Masoko wa kampuni ya Lake Gas ambayo ni kampuni tanzu ya Lake Group, Ramadhani Siasa alisema kampuni yao inatarajia kuanza uzalishaji wa mitungi ya gesi mwezi Desemba mwaka huu. “Kwa sasa mitungi ya gesi za majumbani zinazotumiwa na makampuni mbalimbali inatoka nje.
Sisi tutaanza uzalishaji na hayo makampuni yatakuja kununua kwetu na kupaka rangi zao,” alisema Siasa. Maonesho ya Viwanda mkoani Pwani yaliyofunguliwa Oktoba 17 na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, yanatarajiwa kufungwa kesho na Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda. Watu wanaotembelea maonesho haya wamekuwa wakijionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na viwanda mkoani Pwani na kupata nafasi ya kujinunulia baadhi ya bidhaa hizo kwa bei rahisi.
Chanzo: Habarileo