Mitume, Manabii, Wachungaji, Makasisi na .. Neneni juu ya hili.

mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,379
3,826
Kuna watu wanajiita mitume, manabii na wahubiri maarufu hapa nchini.

Nawaomba mnisaidie kwani ninakabiliwa na utata katika hili. Kwamba natakiwa niitii mamlaka kwani imewekwa na mungu. Hadi sasa naitii malaka yaani raisi wangu na serikali kwa ujumla. Sasa mbona lawama zinazidi kuhusu hii mamlaka? Eti inahusika na hili na lile.

Cijui Uli.. ah! nachoka mimi. SASA TUAMBIENI NYIE MNAOSIKIA MIMONGONO YA ALIYE JUU. Je, mamlaka hii imewekwa na Huyo mumhubiriye?

Je, huyo anasemaje kuhusu hiki chombo chake? Kimeasi, kimelewa madaraka, kinahaha, au akili zimezidi, ama kiko sawa bado na kwamba kelele za pembeni ni za Wafilisti tu?
 
Japo umeuliza wachungaji lakini nadhani yeyote anaweza kuwa na cha kusema kwa suala hili. Kanuni ni moja tu: Mti mwema utautambua kwa matunda yake. Mti mwema huzaa matunda mema na mti mwovu huzaa matunda maovu (Rej. Mt.7:15-20).
 
Umenena aisee. Ngoja nianze kutafakari hayo matunda ya hii mamlka
 
Unawauliza matapeli! Subiri wakishapiga hela Jumapili watakujibu!
 
Yeyote anaweza kujibu hata mimi naweza kujibu. Mfalme Sauli wa Agano la kale alikuwa chaguo la Mungu lakini aliasi na akaendesha serikali dhalimu. Mungu anasisitiza kutii mamlaka hata sasa. Hii haina maana kwamba isishauriwe, kukemewa, na kusahihishwa. Hii ilitokea wakati wa Agano la kale kama Nabii nadhani alivyomkemea Mfalme Daudi. Je serikali yetu imeasi kwa Mungu?
 
hapo niliwataja hao watu tu lakini yeyote aweza kujibu. basi umetoa jukumu muhimu kwamba tunawajibu wa kuikosoa na kuishauri mamlaka na kwamba bado ni halal basi na yenyewe isikie ushaurii. asante
 
Serikali yetu imekosa uhalali mbele za Mungu! Ni kama utawala wa Sauli. Japo alikuwa mpakwa mafuta, lakini hakupewa kibali kwa Bwana na aliishia kupinduliwa ili mpakwa mafuta aliyekuwa na Kibali mbele za Mungu kupata nafasi. Nadhani huu ndio wakati alioufanya bwana ili tukombolewe.
 
Mtu anajiita mtume na nabii! Jina zito sana ndg yangu hawa ni wafanyabiashara ya dini!!
 
Back
Top Bottom