Mitumba inapozuiwa bila kuwa na misingi ya kujenga viwanda

Abel 2015

Senior Member
Sep 5, 2015
112
55
Hivi unapozuia mitumba isiingie nchini wakati huna kiwanda hata kimoja cha kutengeneza nguo uko sahihi kweli?

Wananchi wa vijijini wamezoea kuvaa nguo za bei nafuu sh 1000 wateweza kweli kushona nguo za batiki?

Nadhani magufuli angeanzisha kwanza viwanda vya nguo ndipo azuie mitumba..
 
Tanzania ya secondary production ni hadithi za alinacha hayo mambo yanataka low costs of production policies kwanza and a sizeable market to foster growth. Eti wata export goods badala ya malighafi who is going to do your marketing planning in those countries or how do you compete in prodoction costs kwa uhalisia wa kuzalisha Tanzania.

Hivi unadhani mtu anaefuata malighafi Tanzania anajali kama anaweza zalishia hapa au kikubwa kwakwe ni business analysis wapi kwake bora kwenye costs and policy stability.

Viwanda ni hivi tu vya nishati na tertiary sectors. Secondary production hadithi zaidi ya kutaka kuwaongezea watanzania ugumu wa maisha kupitia hii mitazamo ya kukurupika kwa uhalisia wa mapato hafifu kati ya wengi wetu kama sakata la kuzuia sukari.
 
As ye grow so shall ye weep.
Namaanishi kupata demokrasia ya kweli lazima tupitie machungu.
Lazima tabaka la wakulima na wafanyakazi liseme sasa basi.
 
Kujenga viwanda ni ndoto ya mchana! Sasa wanataka kuzuia mitumba! Hawataweza miaka 3 ni ndoto za mchana! Watuache na mitumba yetu wakimbize miundombinu na maendeleo tunayosubiri! Kwani tukivaa mitumba tunapungua nini sisi nchi masikini? Watuache! Hawana jipya!
 
Mimi sina tatizo na kupiga marufuku Mitumba. Swali la kujiuliza hivi Nani aliwafanya Watanzania kuanza kuvaa Mitumba ?

Mitumba ilianza kuingizwa nchini na watu wa Makanisa kwa ajili ya kuwavisha nguo watoto yatima that was many years ago!

Enzi za Mwalimu imports ya nguo ikawa ni luxury na viwanda vilivyoimbiwa sana nyimbo viliendeshwa na watu walioteuliwa na Mwalimu pasipo kuwaona uwezo.

Matokeo yake tunayajua ni kwamba viwanda vilishindwa kuzalisha nguo kwanza wakulima wa pamba hawakulipwa pesa za pamba waliyouza wakakata tamaa na matokeo tunayafahamu! Yote haya yamefanywa na CCM.

Katika miaka ya themanini kuagiza nguo ikawa bado ni anasa kwa kuwekewa kodi kubwa. As a quick fix Marehemu Sokoine akaruhusu watu waagize Mitumba na imekuwepo for over 30 years.

If the situation on the ground has changed then CCM bila aibu wala utafuti wa kina wameamua kupiga marufuku Mitumba kufuatana na itifaki ya Soko la Jumuia ya Afrika Mashariki.

It's fine the big question is je yanefanyika maandalizi au ni Kama walivyokurupuka kuhusu Sukari na mambo mengine mengi kwenye awamu hii ya 5?
 
Hivi Unapozuia Mitumba Isiingie Nchini Wakati Huna Kiwanda Hata Kimoja Cha Kutengeneza Nguo Uko Sahihi Kweli? Wananchi Wa Vijijini Wamezoea Kuvaa Nguo Za Bei Nafuu Sh 1000 Wateweza Kweli Kushona Nguo Za Batiki? Nadhani Magufuli Angeanzisha Kwanza Viwanda Vya Nguo Ndipo Azuie Mitumba..
Alafu mnasema maskini ndio wanufaikaji wakubwa wa serikali hii!!
ngoja iishe miaka 5 yake tuwe tumesulubika vya kutosha. Na akileta ukurunzinza mbona tutanyoka...asante Mkwere.
 
Kujenga viwanda ni ndoto ya mchana! Sasa wanataka kuzuia mitumba! Hawataweza miaka 3 ni ndoto za mchana! Watuache na mitumba yetu wakimbize miundombinu na maendeleo tunayosubiri! Kwani tukivaa mitumba tunapungua nini sisi nchi masikini? Watuache! Hawana jipya!
Viwanda vya nguo vipo sunflag.A to Z arusha..Urafiki dar vinatosha kuwavalisha watanzania wote
 
Hii ni nchi maskini baba Jesca asikurupuke atujafika levels za kukataza mitumba imetosha kiki sasa anaenda kuharibu kabisa.
 
Aliyeruhusu mitumba kuingia rasmi alikuwa ni Salim Ahmed Salim baada ya ile safari ya Mtwara ambako wananchi walimpokea wakiwa uchi.

Hivi kweli nchi inashindwa kushona nguo za kuvaa. Mbona miaka ya 70 kurudi nyuma ilikuwa ni aibu sana kuvaa kafa ulaya? Kinachotakiwa kufuata ni serikali kupandisha nguo mpya tunazoagiza kutoka nje. Kama kweli Watanzania hawaagiza cherehani na vitambaa ili kuanza kushona nguo basi nitaamini ni watu wa ajabu kabisa.
 
CCM haijawahi kuwa 'consistency' kwenye sera zake. Ilani moja sio muendelezo wa inayofuatia. Na ndio maana kila rais anakuja na lake.

Miaka mitano ni midogo sana kwa nchi kama Tanzania kuwa na viwanda anvyovifikiria. Na ishu sio viwanda, je, hizo bidhaa zitaweza kushindana na zinazotoka nchi nyingine?

Binafsi nashauri Magufuli ajenge zaidi miundombinu mengine aiachie sekta binafsi.
 
Aanzishe kiwanda cha kutengeneza mitumba? Ningekuelewa kama ungesema kuwa watanzania wangeshauriwa kugawa nguo walizozichoka/mitumba kwa watu wa hali ya chini sababu huo utamaduni kwasasa hatuna, unakuta mtu anakaa na nguo hazivai mpaka zinaliwa na panya
 
Back
Top Bottom