Mitt Romney amepiga kura pamoja na chama pinzani cha Demokract kumuondoa Rais wake madarakani

Bess

JF-Expert Member
Oct 4, 2016
542
649
Senator Mitt Romney, ambaye pia alikuwa mgombea Urais wa Marekani mwaka 2012 akichuana na Barack Obama amefanya tukio la ajabu sana kwa historia ya siasa za Marekani, baada ya kupiga kura pamoja na chama pinzani cha Demokract kumuondoa Rais wake madarakani.

Mitt Romney anasingizia kusimamia Imani yake na sio sheria na utaratibu wa chama chake. Ni swali jepesi anaulizwa, kabla ya kuwa mwanachama ulikuwa na Imani tofauti?

Kinachoendelea sasa hivi ni kampeni ya kumuondoa huyu jamaa kwenye chama, amesikika Trumph akisema kikao atakachokaa lazima kifanye maamuzi juu ya hatua ya mwenzao kuwageuka. Misingi ya demokrasia ya vyama vingi mnabishana na kuumizana ndani ya vikao vya chama, mkitoka nje mnakuwa kitu kimoja

Ndugu yetu Membe pia, naye anachuana vikali kupinga sera za mwenyekiti wa chama chake, na ama kujaribu kutaka kuchukua fomu pamoja na mwenyekiti wa chama huku akijua sheria na utaratibu wa chama anachoita chake.

Kumbe Mzee wetu Membe mama mmoja na Mitt Romney
 
Nasikia jana aliulizwa ile acount ya twite unayojimwafai ni yako? Si kaikana bwana! Anasema hana acount ya social media yoyote ile.
 
Wakati uliopita watu hawakuchukua fomu? Yaani mnampaisha kama vile akichukua lazima atashinda, si kura ndo huamua? Jk hawakuchukua, bm je? Mwinyi? Utaratibu ulielekeza watu wasichukue fomu hadi mtu amalize miaka kumi au walichukua ila aliyepo madarakani alishinda?
 
Hao ndio Wamarekani wanaojitanabaisha kuwa Wanademokrasia wa kweli.
 
Back
Top Bottom