Nataka kununua kwa mtu Mitsubishi Pajero, anayeifahamu vizuri

KANYEGELO

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
2,149
4,752
Jamani naomba msaada kwa nayeifahamu vizuri, anisaidie nataka kuinunua kwa mtu. Imetengenezwa 1993 model ni pajero ni manual ina mile 285243 ulaji wake wa mafuta ukoje ...naomba nisaidiwe ...nione kama nauwezo nalo au niachane nalo

1575101977989.jpeg
 
Jamani naomba msaada kwa nayeifahamu vizuri...anisaidie nataka kuinunua kwa mtu ni ,imetengenezwa 1993 model ni pajero ni manual ina mile 285243 ulaji wake wa mafuta ukoje ...naomba nisaidiwe ...nione kama nauwezo nalo au niachane naloView attachment 1277456
Hiyo gari unaweza kuidharau kwa udogo wake lakini ni gari yenye nguvu mno hasa ukiipata yenye turbo.

Kingine km siyo issue kuna gari zina 50k km lakini unakuta ishakuwa taaban na nyingine km wanashusha vile vile, tunachozingatiaga ni utimamu wa engine na gear box.

Kwani unaweza kukutana na gari km 300k lakini engine mpyaa kushinda ya 80k km
 
Nzuri hii chukua haina shida ni ngumu sana. Ujitahidi tu kuweka mafuta ya puma, total, victoria na Engine tu. Maana wale ndio wanauza mafuta premium. Hawa oilcom, sijui nani nani wakwepe kama ukoma.

Sababu ni kwamba hii gari inatumia mfumo wa GDI yaani Gasoline Direct Injection. Mafuta ambayo sio premium huwa yanatengeneza deposits za carbon katika combustion chamber tofauti na hayo ya premium ambayo huwa na additives.

Lakini kwa kujiimarisha zaidi ukiwa unaweka mafuta full tank tanguliza additives za kusafisha carbon deposits katika engine ambayo huwekwa katika tank la mafuta. Total wanazo ukiwaona watakusaidia kukupatia.
 
Back
Top Bottom