Mitsubishi outlander ina burudani gani?

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
67,033
173,713
Wazee kuna hii chuma ya Mitsubishi Motors naona imeanza kuingia mtaani kwa ukali sema experience nilionayo kwa hawa jamaa toka enzi za Pajero mpaka RVR chuma zao zilikuwa nyanya sana japo zina engine zenye nguvu sana.

Cut the story short hio gari nazungumzia ni "Mitsubishi Outlander" naona imetokea kupendwa flani na wabongo wenzangu na idadi yake kitaa inazidi kuongezeka siku hadi siku.

Wenye nayo au ambao mshawahi kuikwea Je, ina maajabu gani hio chuma maana mi kuna moja ya injinia jirani yangu wakati anapandisha mavifaa yake huku anakula ngoma niliona ina inbuit subwoofer kwenye buti kwa kuwa mie ni chizi mziki ikanivutia sana.

images (8).jpeg
 
Sijawahi kupanda zaidi ya kuziona barabaran Ila Kwa kifupi sikuhizi wabongo hawaogopi kununua Magari tofauti na Toyota.
Ni ubishi Tu maisha wengine wanaona Bora waendeshe MIPIRA yenye majina ya kibabe ingawa wanakuwa wameshamiliki Toyota na kuzichoka...
Mimi na wewe ni muda wa kubadilika huu sio miaka yote tunaendesha Toyota tu
 
Sijawahi kupanda zaidi ya kuziona barabaran Ila Kwa kifupi sikuhizi wabongo hawaogopi kununua Magari tofauti na Toyota.
Ni ubishi Tu maisha wengine wanaona Bora waendeshe MIPIRA yenye majina ya kibabe ingawa wanakuwa wameshamiliki Toyota na kuzichoka...
Mimi na wewe ni muda wa kubadilika huu sio miaka yote tunaendesha Toyota tu
Na wengi wenye MIPIRA ya kibabe hua kwny parking zao wana Toyota kama back up,kwa hio ile TI yetu ifanye kama back up mzee baba.
 
Tatizo la JF siku hizi watu hawatoi mirejesho...
Hapa nilitegemea watu waliowahi kuendesha au kumiliki au hata mafundi watoe mawili matatu kuhusu hii gari,

Mazuri yake nj yapi na mabaya yake...

Kakini ninachoamini magari yote ya Kijapani yanayoanzia mwaka 2005 kupanda juu, yanalingana ubora wake na yana ushindani mkubwa kwwnye technology haswa ulaji wa mafuta...

Changamoto kubwa iliyobaki sasa hivi ni spea tu japo kama una Mawe mazito unajilipua kitu roho inataka..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ni gari moja nzuri na luxury nlikua nayo kwa mda mfupi nikiwa katika mizunguko yang y hapa na pale kwakweli kwa nlivokuwa na endesha kwa takribani miezi kama miwili sjaona kasoro ya ilo gari bali mbwembwe walizozieke ndo zilizidi kunivutia na kunishawishi Zaidi kuendelea ina camera Zaidi ya 6 ukiwa nalo kugonga ni ngumu san af apo ndo mziki usipime ni wakutosha kam uko club kwa kweli wamejitahidi japo ni automatic transimision ni gari moja nzuri
 
Back
Top Bottom