ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 1,941
- 3,860
Stiglers Gorge (Mto rufiji)
CHANGAMOTO YA WAKULIMA
Mito hii ina maji mengi SANA sema maji mengi yanatumika kulimia mpunga, Mto Ruaha Mkuu umekaushwa na wanyakyusa wanaolima MCHELE huku nyanda za juu kusini. Serikali lazma iwahamishie chini WAKULIMA hawa, vinginevo maji maji stiglers hayatatosha
- inalishwa na maji ya kwenye mito kutoka mikoa mingi kama Njombe,Pwani, Mbeya, Morogoro na Iringa.
- Kuna mito mikubwa mitatu inayomwaga maji stiglers ambayo ni Kilombero, Luwegu na Ruaha Mkuu
- Mto Ruaha Mkuu ni tawi mama la Mto Rufiji(stiglers) , Mto huu Unaanzia milima ya kipengere makete Njombe na kupitia Mbeya sehemu inaitwa mbarali na unapita Iringa halaf dodoma katikati ya bwawa kubwa la mtera halaf unaenda Morogoro unapita katikati ya bwawa kubwa la kidatu halafu unakwenda kuungana na mto kilombero na Luwegu kutengeneza Mto Rufiji(stiglers)
- Mito inayomwaga maji katika mto Ruaha Mkuu ni Lukosi, Yovi,kitete,sanje,Ruaha mdogo,kisigo,mbarali,kimani,chimala,umrobo,mkoji,kubwa,mlomboji,ipatagwa,mama, na mswiswi(KAMA WAKULIMA WA MCHELE HUKU MBEYA WATAPUNGUZWA MTO HUU UTAKUWA NA MAJI MENGI SANA NA PIA STIGLERS) Inapaswa wakulima waamie kulima chini au downstream yaani baada ya maji kutoka stiglers sio kabla Hayajaingia
- Mto mwingine mkubwa unaopeleka maji stiglers ni Mto kilombero,limto hili ni likubwa linatokea baada ya kuunganika mito mingi midogo midogo kutoka milima ya udzungwa na mahenge na kupita bonde la ulanga, pia maji ya Mto kihansi yakishazalisha umeme yanamwagwa kilombero. Japo pia huku Kuna walima MCHELE wanaopunguza Flow
- Mto mwingine mkubwa kabisa unaomwaga maji stiglers ni Mto Luwegu, una maji MENGI SANA,
- Licha ya hiyo mito mikubwa mitatu pia Kuna mito midogo midogo kutoka mkoa wa Pwani inamwaga maji stiglers.
CHANGAMOTO YA WAKULIMA
Mito hii ina maji mengi SANA sema maji mengi yanatumika kulimia mpunga, Mto Ruaha Mkuu umekaushwa na wanyakyusa wanaolima MCHELE huku nyanda za juu kusini. Serikali lazma iwahamishie chini WAKULIMA hawa, vinginevo maji maji stiglers hayatatosha