Mitihani ya Kidato cha sita nchini kuanza rasmi Juni 29, 2020. Wanafunzi wa bweni watakiwa kuripoti shule Mei 30

1590149458336.png


WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imetangaza mitihani ya kidato cha sita nchini itaanza Juni, 29 na kukamilika Julai 16, mwaka huu.Akizungumza leo na Waziri wa elimu, Prof. Joyce Ndalichako, amesema wanafunzi ambao ni wa bweni wanatakiwa kuanza kuripoti Mei 30, mwaka huu ili ifikapo Juni mosi waanze masomo.

Ameliagiza Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kusambaza mitihani hiyo mara moja, lakini pia kuhakikikisha matokeo yanatoka kabla ya Agosti 30, mwaka huu. "Tunataka wanafunzi watakaofanya vizuri wapate muda wa kutuma maombi vyuo vikuu bila kuathiriwa na muda," amesema.

Kuhusu, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Vyuo Vikuu amesema tayari bodi hiyo ina fedha kiasi cha Sh.Bilioni 122.8 kwa ajili ya wanafunzi wenye sifa ya kupata mikopo hiyo. "Kinachotakiwa ni vyuo kuwasilisha nyaraka muhimu na hadi Mei 28, mwaka huu nyaraka hizo ziwe zimewasilishwa Bodi ya Mikopo ili itoe fedha hizo mara tu wanafunzi wanapofika vyuoni," amesema.
 
29 June mbona wamepeleka mbali sana, walitakiwa kutangaza wiki 2 tu kutoka sasa ili tuingie chuo mapema kabla mwaka kuisha
 
Kwa chuo wamezingua. kwamba anataka kusema. Chuo kifungue wa kumi as usual. Huu ni uhuni.
 
Baraza la Mitihani la Taifa NECTA wametoa ratiba ya mtihani wa kidato cha 6 kwa mwaka 2020 kama inavyoneshwa kwenye kiambatanisho hapa. Tunawatakia mtihani mwema na Mungu awalinde dhidi ya virusi vya Corona
 

Attachments

  • FORM_VI_2020_june (1).pdf
    235.7 KB · Views: 1
Huyu mama ni prof wa ajabu duniani. Ameibuka sijui kutokea wapi muda huu.wanafunxi hata kumalizia sillabus ilikuwa bado .na tangu corona uanze haijawahi kusema chochote kwenye sekta ya elimu.
Embu weka akiba ya maneno na tumia lugha ya kistaarabu, wewe ni mwalimu? je syllabus ilitakiwa kumalizika lini? kwahiyo mwalimu anatakiwa kumaliza syllabus miezi miwili kabla ya mitihani? alafu usichojua kaa kimya, ukiandika usichokijua unadhihirisha uwezo wako wa kufikiri jinsi ulivyo.
 
Embu weka akiba ya maneno na tumia lugha ya kistaarabu, wewe ni mwalimu? je syllabus ilitakiwa kumalizika lini? kwahiyo mwalimu anatakiwa kumaliza syllabus miezi miwili kabla ya mitihani? alafu usichojua kaa kimya, ukiandika usichokijua unadhihirisha uwezo wako wa kufikiri jinsi ulivyo.
Yan ni hv Hawa madgo kwanza wanafaida wameachiwa gap kubwa mno la kufny revision ,2 month ..na sylabuss lazm imalizwe. Before Pepa na shule zlifungwa tarehe za april mwanzoni na mtihani ulkuwa ufnyike may mwanzoni ,kwa maana hyoo lazima madogo walkuwa wamejiandaa vya kutoshaa ,,cha ajabu huku mtaani naona madgo wamejisahau daily kuzunguka kuwinda tunda wale/waliwe kimasihala..

Dogo lngu hapa juzi ndo naona kashika daftri na tunamsihi always apige book ...so what next wasipojipanga vzuri kwa mudaa huu uliobaki wanaweza kuharibu kazi vibaya maana wengi wao walibweteka na likizo ya corona..
 
Back
Top Bottom