Mitihani ya Kidato cha sita nchini kuanza rasmi Juni 29, 2020. Wanafunzi wa bweni watakiwa kuripoti shule Mei 30

Cicadulina

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
961
2,345
"Mitihani ya kidato cha sita itaanza rasmi tarehe 29 Juni na itafanyika hadi tarehe 16 Julai 2020, mitihani hiyo ya kidato cha sita itaenda sambamba na mitihani ya ualimu"-Joyce Ndalichako - Waziri wa Elimu Tanzania.

"Tumeliagiza Baraza la Mitihani la Tanzania kuhakikisha kwamba mitihani hii inapokamilika, ni lazima matokeo yake yatoke kabla ya Tarehe 31 Agosti,2020, ili tuweze kuendana na maelekezo ya Mhe. Rais kwamba wanafunzi hawa waweze kujiunga na vyuo vikuu kama ambavyo imepangwa".Waziri Ndalichako.
------
















Wizara ya Elimu imewataka wanafunzi wa kidato cha sita wale wa shule za bweni kuanza kuripoti shuleni mei 30 mwaka huu.

Waziri wa Elimu nchini amezungumza na kusema "Wanafunzi wa kidato cha sita watafungua tarehe 01/06/2020 na wanafunzi watakuwepo shuleni wakijisomea na kufanya maandalizi ya mitihani mpaka tarehe 28/06/2020"

"Mitihani ya kidato cha sita itaanza rasmi tarehe 29 Juni na itafanyika hadi tarehe 16 Julai 2020, mitihani hiyo ya kidato cha sita itaenda sambamba na mitihani ya ualimu"

"Tumeliagiza Baraza la Mitihani la Tanzania kuhakikisha kwamba mitihani hii inapokamilika, ni lazima matokeo yake yatoke kabla ya Tarehe 31 Agosti,2020, ili tuweze kuendana na maelekezo ya Mhe. Rais kwamba wanafunzi hawa waweze kujiunga na vyuo vikuu "

"Tunaviagiza vyuo kufanya maandalizi muhimu,ili viweze kufunguliwa 01/06/2020, na tunazielekeza mamlaka za vyuo vikuu kuweka utaratibu ambao watahakikisha kwamba masomo yanaendeshwa katika mfumo ambao utakuwa ni wa kufidia pia ule muda ambao wanafunzi walipoteza"

"Ningependa kuwahakikishia Watanzania kwamba fedha kwaajili ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu wa juu kwaajili ya kulipa muhula wa tatu tayari serikali ilikwishatoa, ziko Bodi ya mikopo".
 

Attachments

  • TAARIFA UFUNGUZI SHULE NA VYUO.pdf
    822.8 KB · Views: 1
Huyu mama ni prof wa ajabu duniani. Ameibuka sijui kutokea wapi muda huu.wanafunxi hata kumalizia sillabus ilikuwa bado .na tangu corona uanze haijawahi kusema chochote kwenye sekta ya elimu.
Wanaweza tungiwa mitihani fulani ya wastani ili kuhakikisha wengi wali-cover maeneo hayo ( topic za mwanzo).

Baadhi ya topics za mwisho mwisho zinaweza zisiwepo kwenye maswali ya mitihani, japo hizi ni hisia zangu tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom