Mitihani ya form 6-PCB: Ndiyo maana ufaulu unakuwa mkubwa

Nimekuwa nijiuliza kulikoni PCB mtu anafaulu na AAB, BBB, ABB and the like. Kumbe ni mitihani level ya kidato cha PILI na kidogo cha NNE
Angalia biology -2020: Maswali ya form 2... kidogo form 4!
Ww unaongea Hvyo wakati A za Bios Zipo 6 ,hakuna mschana wa PCB aliyepata One ya NNE and Above ,Ungeufanya Then uongeee
 
Ni kweli kabisa mitihani ya siku hizi ni rahisi mno hii inachangiwa na hofu ya kisiasa yaani baraza la taifa la mitihani linajitahidi sana kuonekana ufaulu unapanda mwaka hadi mwaka.

Kuna vijana wanafaulu let say english ana A lakini akifika chuoni hadi unajiuliza huyu alipataje A ya english maana ni mweupe hadi aibu.
 
Ni kweli kabisa mitihani ya siku hizi ni rahisi mno hii inachangiwa na hofu ya kisiasa yaani baraza la taifa la mitihani linajitahidi sana kuonekana ufaulu unapanda mwaka hadi mwaka.

Kuna vijana wanafaulu let say english ana A lakini akifika chuoni hadi unajiuliza huyu alipataje A ya english maana ni mweupe hadi aibu.
Kwa hiyo huo mtihani aliopost jamaa ni mrahisi????
 
Huu mtihani nimeupenda maana umegusa maeneo mengi ambayo wanafunzi wanajifunza A level. Ukipata A ya huu mtihani maana yake biology unaijua vizuri na unaweza kupangilia points vizuri.

Mfano swali la 7 hapo la respiration nimependa lilivyoulizwa hasa kipengele C maana hata chuo linaulizwa hivyohivyo na majibu yake hayatofautiani sana.

Topics za biology olevel ni sawa tu na a level ila a level inaingia ndani sana. animal cell inavyochorwa O level ni tofauti sana na A level kuanzia composition mpaka mwonekano. kwa asiyejua akiona form 6 kaulizwa achore animal cell atadhani ni swali jepesi la form 1.
 
Kuwekewa Swali la Classification angalau mtu asitoke na Sifurii wao wameona ni mtihani wa form one...!! Wamesahau hata mtihani wa Hesabu wa form four huanza na algebra na kujumlishaa sasa ngoja usonge kidogooo show kalii Hapo ndo utajua hujuii..
 
Hamna paper hapo chief, tutakuja tupate watu wepesi sana huko mbeleni ambao kimsingi watashindwa majukumu yao
 
Kumbukeni pia mazingira ya sasa yamerahisisha upatikanaji wa maarifa.
Zamani hata kupata tu vitabu,summary,ama mwalimu wa tuition ukiwa nyumbani ilikuwa vigumu sana.

Sasa hivi mtu anaenda kidato cha tano kaisha soma physics yote a advance kamaliza.Anafanya marudio tu
Yes zamani ndio ulikuwa mwendo... siyo AAA, BBB, BBA etc kama sasa hivi
 
Kimsingi biology haijawahi kuwa ngumu.
Weka pepa ya phy au che nyepesi.
Af watu wanapenda kuheshimu kama zao hata kama hawana impact yeyote kwenye society.
Kwan nyie wasomi wazamani mmefanya nn ambacho wa sasa hawawezi fanya?
 
A za biology huwa hazifikagi 30. Hakijabadilika kitu mwaka huu... Na kuhusu huo mtihani acha kupotosha kwa kusema ni kidato cha pili na nne. Aliyesoma Biology level yeyote hapo ataelewa ninachokiongea
Mtihani sio wa kidato cha pili au nne ila NI RAHISI SANA.
 
Hebu tufanyie hiyo section then tutajua kama kweli ni mrahisi
NB: Usitumie google
 
Back
Top Bottom