Mitihani darasa la saba 'yapotea' Dar; kutokana na kupotea kwa ofisa aliyekuwa akisambaza mtihani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mitihani darasa la saba 'yapotea' Dar; kutokana na kupotea kwa ofisa aliyekuwa akisambaza mtihani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Sep 21, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  20 SEPTEMBER 2012


  Na Masau Bwire

  MTIHANI wa taifa ya kuhitimu elimu ya msingi jana ulianza kwa dosari jijini Dar es Salaam, kwa kuchelewa kuanza kufanyika muda uliopangwa kutokana na kupotea kwa ofisa aliyekuwa akisambaza mtihani huo.


  Dosari iliyojitokeza jana katika Shule za Msingi Ndumbwi na Mbezi Juu, zilizopo Manispaa ya Kinondoni ambapo mtihani ulichelewa kuanza kwa zaidi ya saa 3. Katika shule hizo mitihani ilianza kufanyika saa 5: 15 na nyingine saa 5:45 badala ya saa saa 2:00 kamili asubuhi

  Mkuu wa msafara aliyekuwa akisambaza mtihani huo katika shule hizo, Bw. Jonasi Peter, ambaye ni Mratibu Elimu Kata ya Mikocheni, alidai hakuwa anajua mahali shule hizo zilipo, hali iliyomfanya apotee njia na kufika shuleni hapo akiwa amechelewa baada ya kuuliza kwa wenyeji wa maeneo hayo.

  Akieleza sababu za mtihani huo kuchelewa kufikishwa katika shule hizo, mbele ya Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo Bw. Philipo Mulugo, aliyefika katika shule hizo baada ya kupigiwa simu na Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Ndumbwi, Bi. Joyce Nyamwela, kumweleza tatizo hilo, Ofisa Elimu wa Manispaa hiyo Bw. Hassan Kalinga, alisema tatizo hilo limesababishwa na uzembe wa Mratibu Elimu Kata hiyo.

  Bw. Kalinga alimweleza Waziri Mulugo kwamba, alichokifanya mkuu huyo wa msafara kuchelewesha mtihani kufika katika shule hizo ni uzembe, kwani alitakiwa atembelee eneo lake kabla ya siku ya mtihani ili azifahamu shule zake lakini yeye kwa uzembe alishindwa kufanya hivyo na kusababisha yote hayo yaliyotokea.

  Baada ya maelezo hayo ya Ofisa Elimu, Waziri Mulugo alimwagiza asimamie utaratibu wa chakula kwa wanafunzi hao shuleni hapo na kuzuia wanafunzi kutoka eneo la shule na simu zote za walimu zikusanywe ili kuepuka mawasiliano na shule nyingine.

  Aidha Waziri Mulugo alisema, Mratibu huyo mara baada ya mtihani wa mwisho kumalizika atatakiwa kueleza sababu zilizomfanya acheleweshe mitihani hiyo na kwa nini asichukuliwe hatua kwa uzembe alioufanya, uliolenga kuvuruga usimamizi wa mitihani.

  Mtihani katika shule ya Ndumbwi ulifikishwa saa 5 na kuanza saa 5.15 asubuhi wakati katika shule ya Mbezi Juu ulifika saa 5.30 na kuanza saa 5. 45.

  Waziri Mulugo jana alizitembelea shule kadhaa katika Manispaa ya Kinondoni na Temeke kuangalia jinsi ulivyokuwa ukifanyika.

  Shule alizozitembelea katika Manispaa ya Kinondoni ni Victoria, Makumbusho, Kijitonyama, Kijitonyama Kisiwani, Mwangaza, Ndumbwi na Hazina ambayo ni shule isiyo
  ya Serikali.

  Katika Manispaa ya Temeke Waziri Mulugo alizitembelea shule za Mivinjeni, Wailes na Likwati ambapo leo amepanga kuzitembelea shule katika Manispaa ya Ilala na Temeke eneo la Kigamboni.


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Uzembe, huyo OFISA watoto wake wanasoma PRIVATE School... Hajali watoto wanaosoma SHULE ZA SERIKALI
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tanzania siku zote hatuishi vioja; mtu mzima tena afisa wa serikali aliyeaminiwa na kukabidhiwa majukumu nyeti, kama kwenda kuwapima watoto wetu kiakili ili kujulikane yupi wa kuendelea na masomo sekondari ipi, atapotea?????????
   
 4. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  achukuliwe hatua za kinidhamu haraka sana!huwezi kupangiwa kupeleka mitihani sehemu halafu usianze kwanza kulitembelea eneo husika kabla ya siku ya mtihani!
   
 5. C

  CHOMA Senior Member

  #5
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kupotea kwa Mratibu Elimu Kata huyo kunatokana na USIRI wa taratibu za uendeshaji wa Mitihani hiyo kwa sababu Afisa huyo hufahamu eneo lake la utendaji kazi alfajiri ya siku ya mtihani.Hivi Naibu Waziri halijui hilo.Hembu kabla hawajatoa maagizo yao wafuatilie kwa karibu taratibu zote za uendeshaji wa Mitihani hiyo.Bado kuna changamoto nyingi za uendeshaji wa Mitihani hiyo ambayo nafikiri Wizara husika na Baraza la Mitihani hawazijui.Kamwe changamoto hizo haziwezi kumalizwa kwa kutolewa maagizo kwenye vyombo vya habari.
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kwa serikali dhaifu na legelege yote hayo yanawezekana!!! Ndiyo maana hakuna kujali kazi maana hata walio juu hawajali sana!!!
   
Loading...