Miti ya Barabara ya Sam Nujoma kwishnei! ndiyo tumeliwa?

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,372
2,374
Nimepita leo Sam Nujoma road na kuona ile miti iliyopandikizwa fasta wakati wa World Economic Forum kule Mlimani city ipo hoi imekauka na mingine kudondoka.Jamani who is behind huu ubadhirifu coz nasikia walitumia mamilioni kuiweka pale, je hawakuseek ushauri sahihi kutoka kwa wataalamu au ni matunzo?bora hata wangeweka minazi artificial iwake wakeusiku tujue moja
 
Mthinichekeshe mie jamani! Ila aibu kweli kweli. Kuna jamaa aliwahi kunisimulia stori kuwa enzi za "Mwalim"u akiwa anatembelea vijiji vya ujamaa, kuna kijiji kilitengeneza shamba kwa ajili ya maonyesho ya kilimo katik avijiji vy aujmaa. Kuliwa na mahindi yamestawi vizuuuuuuuuuuuri. Wakati amemaliza ziara yake aliomba apite tena kwenye lile shamba maana aivutiwa sana; ha ha ha guess what alivyopita mara ya pili mahindi yote yamenyauka maana yalipandikizwa faster masaa machache kabla ya "Mwalimu" kuwasili kwa ajili ya maonyesho tu ili "Mwalimu" aondoke na impression nzuri ya kijiji chao. How is this different from the Sam Nujoma palm trees? Lol!
 
Wewe si mgeni na nchi yetu,watu hawataki kuwajibika ipasavyo,tunachojua ni ufisadi na fitina tu!!
 
USHAURI WA BURE KWA WAHUSIKA "NG'OENI HIYO MITI YOTE SASA"............Inaongezea uchafu wa jiji ambalo tayari ni chafu kupitiliza.
 
Nimepita jana nimeaangalia ile miti nimechoka maana imekuwa kama uchafu sasa ni bora itolewe ijulikane moja tu
 
Ni kweli kabisa lakini si walipata maujiko kwa Wageni wale. Basi hiyo ndiyo tabia ya Wanafiki na walafi
 
Nilipata kusikia gharama ya ile miti nilichoka hoi.
iligharimu mamilioni ya pesa.
 
Hayo ndo matunda ya viongozi wa bovu wa CCM.....yaani kila mahala ni kuchemsha tu.....Siku zote walikuwa wapi wasipande miti ikakua ikastawi na kadhalika...mpaka waje wazingu? Mimi nazani kwa staili hii hatutafika tunakotaka........Au wangetafuta wataalamu labda ingesaidia kujua aina ya miti ya kupanda......Lakini !!!!!!!!!!!inamaana hata kuweka watu wakumwagilia imeshindikana?
USHAURI WA BURE KWA WAHUSIKA wa hii ishu ni bora sasa waingoe ambayo imekauka maana kwa kweli ukipita na kuitazama utakubaliana na mimi kuwa inaongeza uchafu wa jiji .
 
hii ni mojawapo ya kazi za Mbunge wa jimbo Bw. Mnyika
kha!!!

Mwisho tutaambiwa hata kuchimba choo tandale kwa bwana sefu ni kazi ya mnyika

basi tufute halmashauri, tufungue ofisi inaitwa mnyika... tu-manufacture vimnyika kama mia visambae jimbo vifanye kazi
 
Nyie vipi mnahangaika na miti ,ndio tatizo lenu mliozaliwa muhimbili mkakulia ilala! We uliona wapi mti mkubwa vile ukapandikizwa .......tatizo lenu hamjui vipaumbele! Kipaumbele chetu sasa ni kutibu vidonda vya uchaguzi 2010.......kuna watu walijifanya ni chaguo la mungu! Wakati mungu alishachagua mtu wake 2005!
 
Walitangaza mti mmoja 700,000.00 na waliahidi kupanda mpaka ubungo, kweli tuna viongozi wazuri wanaofikiria leo na sio kesho.

Hivi mtu aliyetoa proposal ya ununuzi wa hiyo miti ni nani na aliyeidhinisha malipo alifikiri kitu gani na walioona miti imepandwa ghafla wakati wananenda kwenye mkutano pale ni akina nani hawa wote wanatakiwa kuwajibika na hasara za mradi huu.
 
world economic forum ni kama baba wa ile miti baada ya kuisha kwa mkutano ule ni sawa mwenye mali anapokufa, na mara nyingi viongozi wetu huwa hawatumii njia ile katika misafara, na cha zaidi serikali haikuweka watu wa kuifatilia ile miti, na ukizingatia jua letu linajulikana linavyochoma miti ile isingeweza kustawi.
 
Halafu tunakataa kuwa elimu bure haiwezekani! Kumbe hela zipo jinsi ya kutumia tu ndio tatizo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom