Mitego iliyoandaliwa kuiua CHADEMA itashindwa ikiwa CHADEMA itazingatia haya

Membensamba

Senior Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
157
Likes
0
Points
33

Membensamba

Senior Member
Joined Nov 4, 2010
157 0 33
Mwanzoni nilidokeza mikakati inayoandaliwa kuimaliza cdm miaka mitano ijayo kuwa ni pamoja na kuwatumi "virusi" waliotumwa maalum kwa kazi hiyo ndani ya cdm. Virusi hao ni mapandikizi maalum. Wengine walitumwa kutokea ccm tangu mwanzo wa kuanzishwa kwa vyama vingi ili waudhoofishe upinzani. Lakini wengine wamenunuliwa wakiwa huko huko cdm.

Kwa faida ya baadhi wale wasioelewa au kuamini kuwa huwa ccm inaweka mapandikizi, niwakumbushe yule mwanamke mwanasiasa mkongwe (jina unalijua) aliyetokea TVT (sasa TBC) miaka michache iliyopita akaeleza kwa kirefu jinsi Mwl Nyerere alivyomtuma akiwa na Kambona kwenda kuwa mwanachama cha upinzani (zamani za awali za vyama vingi) kwa lengo la kuwasoma na kudhoofisha upinzani. Na jinsi Mwl alivyomshauri aende akamtukane kwenye press ili wapinzani waamini kuwa kweli katoka TANU, na jinsi alivyofanikisha kazi hiyo. Tumeshuhudia watu waliokuwa mashuhuri kwenye vyama vya upinzani wakifanya yanayokijenga ccm na kudhoofisha upinzani tangu 1995. Na sasa nawaambia, wako mamluki wengi tu cdm, wengine wamenunuliwa wakiwa humo humo na wengine wametumwa rasmi. Wote hawa ni virusi-watu, wana kazi ya ku-corrupt mfumo wa cdm ili kukidhoofisha na hatimaye kukiua kabisa.

Lakini antivirus zipo, tena kali. Moja ni hii: CDM inawapasa kutilia mkazo (concentrate) kwenye mambo yanayo waelimisha watu na kuwaamsha kuelekea mabadiliko ya katiba na uundwaji wa tume huru ya uchaguzi. Hii inapaswa iende sambamba na kuwasiliana na serikali kuhusu hilo. Kufanya hivyo kutaondoa mtazamo wao kwenye mambo madogo yasiyo na maana na kuwaweka kwenye mkazo wa mambo ya kukijenga chama na mustakabali wa demokrasia nchini. Ikumbukwe kuwa silaha moja kubwa ya ccm ni kuwafanya cdm kugawanyika kwa kuwasababishia malumbano au kupingamana kwa mambo madogo madogo ili kionekane kuwa hakina mwelekeo. Kwa cdm kutilia mkazo maswala (issues) badala ya tofauti ndogo ndogo watajenga umoja wa viongozi, wanachama na wafuasi, jambo litakaowafanya wale "virusi" wakose njia ya kuwagawanya.

Jambo la pili la kufanya ni kufanya utafiti na uchambuzi yakinifu kuu ya mazingira yaliyopo ya kisiasa, kwa lengo la kutengeneza mikakati ya kisanysi ya kujenga mtandao mpana wa kichama nchi nzima, kuanzia ngazi ya shina. Hii ni pampoja na kubuni mpango mkakatiti wenye malengo ya muda mrefu kuelekea mabadiliko ya kweli nchini na maendeleo ya taifa. CDM isipuuze mtandao wa ccm. Ni lazima kuwepo na structure inayo-counter hiyo yao la sivyo kuingusha ni vigumu. Wakiwa "busy" na huku kukijenga chama kutakuwa hakuna nafasi ya "virusi" kufanya kazi.

La tatu ni kujenga na kuzingatia kanuni za utawala. Ni lazima chama kijenge utamaduni wa mshikamano, uwajibikaji wa pamoja, mwelekeo mmoja, na nidhamu ya hali ya juu. Mambo hayo yawe sehemu ya masharti ya kuwa mwanachama na kiongozi, na mtu akikiuka uwepo utaratibu wa kumsaidia na hata kumwondoa uanachama na/au uongozi ulio wazi. Kisha viongozi wayasimamie pasipo kumwonea haya mtu yoyote. Naamimi mambo haya yakizingatiwa cdm itakuwa invincible.
 

len

Member
Joined
Nov 9, 2010
Messages
98
Likes
2
Points
15

len

Member
Joined Nov 9, 2010
98 2 15
Nakubali kabisa, CDM ielekeze guvu zaidi ktaika kujijenga kwa kufungua matawi nchi nzima. Pia wanapaswa kuwa very creative katika kujiimarisha bila kusahau kutoa elimu kwa watanzania. Waendelee kupigania katiba mapya, nec iliyo huru zaid
 

Jatropha

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2009
Messages
1,152
Likes
144
Points
160

Jatropha

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2009
1,152 144 160
kupitia ruzuku watakayopata waanzishe shirika la habari la kutoa magazeti, redi na tv, ili isamabae nchi nzima wawashirikishe wapenzi wao kwa njia ya kununua shares lakinimkuw ana kiwango maalum.
 

RealMan

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Messages
2,355
Likes
174
Points
160

RealMan

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2010
2,355 174 160
Umesomeka vizuri hasa kwa swala la kuwa na mtandao mpaka mashinani. Tuunganishe nguvu kuanzia sasa ili 2014 tunaanza na serikali za mitaa kama warm up, ikifika 2015 itakuwa kama tunamsukuma mlevi vile!
 

Forum statistics

Threads 1,203,212
Members 456,663
Posts 28,104,838