Uchaguzi 2020 Mitazamo kinzani kwenye uchaguzi huu

Wamkopeka

Senior Member
Apr 2, 2012
136
308
Kwa muujibu wa tume ya uchaguzi wapiga kura walioko kwenye daftari la mpiga kura ni zaidi ya 29m.

Katika wapiga kura hao 29m wana mitazamo tofauti juu ya wagombea urais wa Tanzania.

Kuna wale wanaomsapoti rais aliyepo na kumuona kwamba anastahili kuendelea kwa kipindi kingine. Kigezo kikubwa ikiwa ni uchapa kazi wake, kwamba katika kipindi cha uongozi wake maendeleo makubwa yamepatikana ambayo kwa miaka mingi ilikuwa kama ndoto.Ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara,umeme,reli,majengo ya shule, hospitali na zahanati , miundombinu ya maji pamoja kuhuisha shirika la ndege kwa kununua ndege mpya.

Pia wanadai kwamba amejenga nidhamu ya kazi kwa watendaji wa serikali ambao hapo kabla walikuwa wamejawa na kiburi na kujiona miungu watu.

Vilevile wanadai ni mtu asiyevumilia uzembe na ubadhilifu wa mali ya umma na ndio maana hasiiti kumtumbua mtu papo kwa papo.

Kwa wale wanaompinga mtazamo wao umejikita zaidi katika kukosoa mtindo wa uongozi wa rais aliyepo.

Pamoja nambo yote niliyoyataja hapo juu kuwa ni mazuri kwa maana ya kuwa ni maendeleo, lakini wanasema ni maendeleo yasiyogusa maisha ya watu moja kwa moja na ndio maana hali ya maisha mtaani imekuwa ngumu sana.Licha ya kelele nyingi lakini rais ameendelea kuziba masikio, hivyo kuonekana si rais anayejali sana maisha ya watu.

Pia wanadai katika kipindi cha uongozi wake watu wameishi kwa hofu kubwa sana, Ukionekana una mtizamo hasi juu ya uongozi wa rais basi wewe ujue uko kwenye hatari, wakitolea mfano wa madhira yaliyowapata wale wote walioonekana kumkosoa rais, baadhi ya Maaskofu,Masheh,kina Mdude, Ben Saanane, Tundulisu,Azory Gwanda,Lueno,Kanguye nk.

Ni katika kipindi chake ambapo demokrasia imetikiswa kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa, kwa kuanzia na chaguzi za marudio, ambapo zilipelekea mpaka kifo cha Aquilina. Uchafuzi ulifanyika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na sasa kwenye huu uchaguzi mkuu vyote vina akisi aina ya rais tuliyenaye.

Hawa wanahitimisha kwa kusema uhuru wa watanzania umeminywa kwa gharama ya maendeleo,kuanzia mtaani mpaka bungeni.
Kwao wanaona ni bora kukosekane maendeleo lakini uhuru wao wa kutoa maoni juu ya rais wao, na juu ya nchi yao ubaki palepale.
Demokrasia ichukue nafasi yake ili watu wawe na uhuru wa kuchagua viongozi wanaowataka na si kulazimishiwa viongozi.

Kwangu mimi naona kila upande una hoja hivyo ni vema sasa kwenye uchaguzi huu watu watumie hii fursa kupiga kura ili kuchagua aina ya utawala wanaoutaka.

Kikubwa haki itendeke, anayeshinda ashinde kwa haki. Kusifanyike hila, ghiliba wala udanganyifu wowote. Tanzania ni nchi yetu sote, Rais aliyepo akishinda kwa haki kwa kupata kura nyingi basi wale ambao hawakubaliani na style ya utawala wake wamvumilie wajipange kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Halikadhalika wapinzani wakishinda basi kusiwepo figisu zozote wapewe ushindi wao kwa haki. Nao tutawapima kwa kipindi cha miaka mitano kama tukiona hatupendezwi na utawala wao basi kwenye uchaguzi utakaofuata tutawaondoa.

Ili tuweze kuvuka salama kwenye uchaguzi huu, wagombea wanatakiwa wajishushe, pasiwepo na mgombea wa kujiona yeye tu ndiye anastahili kuwa rais wetu. Kikubwa maamuzi ya wananchi yaheshimiwe ili tuendelee kuijenga tanzania yetu kwa amani.
 
Naona wewe ni mpinzani kabisa. Mshabiki au mwanachama wa CCM yuko kinyume na neno HAKI hasa katika uchaguzi huu. Lissu, Mbowe, Lema na kundi lao ndio wanasema tunataka uchaguzi huru na haki. Kura zikipigawa kwa haki, zikahesabiwa kwa haki, mshindi akatangazwa kwa haki bila figusu wala mizengwe, wao wanasema watahesabu uchaguzi huo kuwa huru na halali. Vinginevyo, hapatatosha.


Mwana CCM hawezi kutamka hivyo kwa kuwa hadi sasa haki haijaonekana kutendeka kwa hii enguaengua ndani ya chama na nje ya chama. Hakuna haki.

Walichapisha fomu moja ya mgombea uraisi ndani ya chama wakati walikuwepo wengi waliotaka kugombea na JPM. Wanajua kuwa goli la mkono kwa CCM halikwepeki hivyo msamiati wa neno haki ni mgumu vinywani mwao. Nakupongeza kwa kuwa mwanademokrasia halisi. Uko tayari kuona haki ikitendeka!!!!!
 
Tunduma leo Magufuli kasema hata kama yupo kuomba kura lakini baada ya uchaguzi tutsmbue kuwa yeye ndiye Rais...no more
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom