Mitazamo kinzani kuhusu tumbua ya Rais Samia Suluhu

Achanakia

Member
Jan 28, 2021
70
125
Mitazamo Kinzani kuhusu Tumbua ya Mh. Rais

Kuna kundi limejitokeza kupinga utenguzi anaoufanya Mh.Rais kwa baadhi ya watu wakizihusisha tenguzi hizo kuharibu legacy ya Magufuli.

Ukweli tabia hii inatia hasira, na ni dharau kubwa kwa mama yetu ambayo kivyovyote vile haikubaliki.

Moja ya watu ambao wahafidhina hawa wamejitokeza kuwatetea ni Kakoko wa Bandari, Bashiru na sasa Sabaya.

Kuhusu Kakoko kutumbuliwa kwake wanakuhusisha na mradi wa bandari ya Bagamoyo, kwamba Kakoko ni kikwazo kwani yeye mtazamo wake kuhusu mradi huo ni sawa na msimamo wa Magufuli.

Kuhusu Bashiru, vile vile wanasema hatakiwi kwa vile tu ni mtu ambaye anaziishi fikra, mtazamo na msimamo wa Magufuli kuhusu Tanzania na raslimali zake.

Vilevile wanadai kutumbuliwa sabaya kumetokana na kelele za wapinzani bila kuzingatia utendaji wake thabiti. Wanatolea mfano kwamba Sabaya kakomesha mtandao wa wezi wa magari mkoani Arusha na Kilimanjaro.

Amefanikiwa kurudisha eneo la Waislam lililokuwa limeporwa na wajanja, pia kurudisha ardhi kwa wananchi iliyokuwa imechukuliwa na wenye nguvu wachache na kuwakodishia wananchi kwa bei kubwa.

Lakini sabaya huyu ndiye aliyesaidia ccm kushinda kiti cha ubunge na halmashauri ya Hai jambo ambalo lisingewezekana kufanywa na mtu mwingine.

Hivyo wanahitimisha kwa kusema tuhuma zote kumhusu Sabaya ni za uongo na zinaenezwa na wapinzani tu.

Kwao vitendo vya wazi, zikiwemo video za cctv camera zinazoonyesha vitendo vya kijambazi vilivyofanywa na Sabaya. Ushuhuda unaotolewa na wafanya biashara namna walivyokuwa wananyang'anywa pesa, kuvamiwa kwenye biashara zao, kuharibiwa mali zao au kutishiwa walipoonyesha kwenda kinyume na matakwa yake, Watu waliokatwa masikio, kupigwa misumari, na kutiwa ukemavu wa viungo, wengine kukimbia miji yao ilibkuyanusuru maisha yao.

Wanasema madai yote hayo ni kelele za wapinzani tu na wala hayana msingi wowote. Inauma sana na hii inaonyesha namna ambavyo watu tumekosa utu dhidi ya binadamu wenzetu kwa vile tu tunatofautiana itikadi za kisiasa.

Inauma na inakera zaidi kufikiri Rais hana taarifa sahihi juu mienendo ya watumbuliwa. Kinachokera zaidi watu hawa hawa walikuwa mstari wa mbele kushangilia na hata kumpongeza Magufuli alipokuwa anawatumbua watu, tena wakati mwingine bila hata kuzingatia sheria tena kwa kuwatweza utu wao.

Mara kwamara alikuwa akisema yeye ana taarifa nyingi kuwahusu watu anaowatumbua na wasifiaji hawa walikuwa wanaamini kila walichokuwa wanaambiwa na Magufuli, lakini sasa wanashindwa kumuamini Mama yetu kama kwamba ofisi ya urais imebadilika, na kwamba mama hawezi kuwa na taarifa za anaowatumbua.

Haipendezi kabisa watu waache unafiki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom