Mitazamo hasi ya Wananchi: Wahusika fanyeni yafuatayo

infinite_

Senior Member
Sep 10, 2013
127
125
Kutokana na hali iliyopo sasa; baadhi ya Vijana/Wananchi wameonekana kuwa na mitazamo hasi kwa namna moja au nyingine dhidi ya Serikali; naombeni fanyeni tafiti kabla hamjapinga.

Hali hii inatokana na sababu mbalimbali zikiwemo kubwa na chache zifuatazo:

1. Kutokuwepo kwa ajira kwenye Public/Private sectors kitu ambacho vijana/wananchi wengi wanaona kana kwamba Serikali yao haipo kwa ajili ya wananchi na kuishia kuwa na mitazamo hasi na kusema vibaya mitandaoni au kwenye jamii zao.

2. Kutokuwepo kwa Proper Circulation of Money pamoja na major sources of money in circulation; Kitu hiki kinawafanya kila raia kuanza kulalamika kutokana na ugumu wa maisha na kukosekana kwa mzunguko wa pesa. Please tusilete visingizio kwamba Watanzania wote walikuwa ni wapiga dili; hali ni mbaya sana sana.

3. Kauri mbalimbali zinazoendelea kutolewa na viongozi mbalimbali nchini; Kitu ambacho kinakuwa perceived kwamba ni kauri hasi kwa wananchi na wapiga kura.

4. Kushindikana kutekeleza kikamilifu kwa bajeti iliyopo sasa pamoja na Miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

5. etc

Kipi kifanyike kuondoa mitazamo hasi ya wananchi iliyopo sasa?

1. Serikali ifungue ajira haraka iwezekanavyo na kuanza kuajiri. Tukiendelea kufungia ajira na hali ya wananchi ilivyokuwa ngumu financially kwa sasa tunatengeneza Bomu (The effects/Consequences of unemployment on our society) ambalo siku moja wananchi hawa wakifika on their maximum limits (Loss of trust in administration and the government which may lead to political instability) basi ujue wataweza kuandamana au kuondoa hali ya Usalama ndani ya nchi yetu sababu they will have nothing to lose or fear na siku zote ogopeni wananchi wa namna hiyo (Wahusika please fanyeni Prediction analysis/Predictive analytics on this overall issue).

1.2. Sioni sababu ya kupoteza mabilioni ya pesa kuwasomesha vijana wetu vyuoni pesa ambayo ni ya Serikali alafu vijana hawa hawa wanaishia kukaa mtaani bila ya kutumia elimu yao tuliyo wasomesha; tukisema tu Fanyeni kazi; Je wafanye kazi gani wakati Consumer spending haipo kabisa kutokana na kukosekana kwa pesa??!

2. Wale washauri wa Serikali kitengo cha Uchumi mnabidi muweke counter measures za ku-stabilise uchumi wetu haraka iwezekanavyo na muweze kushauri wahusika on time ili hali ya sasa ibadilike na wananchi waweze kuona unafuhu wa maisha na kuondoa fikra hasi iliyopo towards their Government. Kumbukeni pesa kwa sasa hakuna kabisa na wakati huo huo ugumu wa maisha nao ndio unazidi kuongezeka.

3. Washauri na waandishi wa hotuba za Viongozi mbalimbali waweze kutoa ushauri mzuri kwa wahusika kuhusu kauri zao wanazozitoa kwa wananchi na jamii nzima ikiwezekana kauri hizi zipungue, zisiwepo kabisa au labda niulize kwani ni lazima kuongea in that tone??; Kumbukeni kuna maisha baada ya Sasa na kumbukeni kuna uchaguzi mbeleni hivyo kauri mnazotoa sasa zinaweza kugeuka miba hapo mbeleni na msisahau wananchi hawa hawa ndio ufanya kuchagua viongozi. Kauri na matendo mnayofanya utengeneza tabaka ndani ya jamii na hapo hapo utengeneza makundi ndani ya vyama vyenu vya siasa na makundi hayo baadae yanaweza kutumika kuleta ushindani mkubwa kwenye uchaguzi kwa namna moja au nyingine na kuweza kuwatoa kwenye uongozi kupitia hizo chaguzi.

4.1. Mabalozi wetu wa Tanzania kokote walipo duniani waweze kutumia hekima na busara ya Kidiplomasia kuweza kuongea na nchi wahisani na kurudisha hali iliyokuwepo hapo mwanzo na kama kuna makosa au vigezo vya aina yoyote ambavyo tumewekewa na baadhi ya nchi marafiki basi tutumie ushawishi wetu wa Kidiplomasia na kuweza kuwavuta (to negotiate) nchi wahisani waweze kutusaidia 110% kama mwanzo lakini tukiishia kusema eti nchi yetu ni tajiri tu na tunabaki kuendelea kukopa ovyo ovyo wakati hatuna sources of income za kutosha kulipa hayo madeni basi ni sawa na Kazi bure na tunaliangamiza hili Taifa. Kukopa sio vibaya lakini kukopa ukiwa na uchumi mzuri na sources of income nyingi (kodi, n.k.) hapo ni sawa lakini kwa sasa makampuni mengi yanafungwa na kuachisha wafanyakazi hiyo kodi utakusanyaje?? hatuna FDI nyingi kokote pale duniani, kiwango cha watalii kinapungua sasa tunapata wapi pesa ya kulipa hayo madeni?? Kupitia Tanesco, TTCL, nk peke yake tu??! Hapana Diplomacy and other counter measures zinabidi zitumike kusimamia our national interests ipasavyo.

4.2. Viongozi waliopita wote, Sio lazima mpaka muombwe ushauri mnabidi muoneshe uzalendo wenu kwa Taifa la Tanzania na kuomba kuonana na Mh. Rais na kama mna plans za kusaidia Taifa la Tanzania kwa namna moja au nyingine basi tunawaomba msaidiane na Mh. Rais na ikiwezekana mtumike as Prominent figures sambamba na mabalozi wetu kushawishi nchi wahisani kuendelea kusaidia Taifa letu kwa kiwango kama cha zamani na pia kuwavuta wawekezaji zaidi. Tutoe ushirikiano kuweza kusaidia Taifa letu la Tanzania.

4.3. Viongozi waandamizi wa ile idara yetu ya Tanzania mnabidi na nyie mfanye assessment kwenye matukio na hali iliyopo sasa ni mbaya mbaya mbaya saaaana; natumaini mmeshaifanya hiyo assessment na mnasikiliza na kusoma reports za vijana wenu na mnaona hali halisi; Please chukueni counter measures ipasavyo kama ABC zinavyosema. Mkizembea kwenye hili wote tunajua ubaya wake baadae. Endapo kama Busara zikikwama msishindwe kuomba busara kwa walio watangulia cause wengi bado wapo hai.
Mwisho, sikilizeni sana reports za vijana wenu ziwe nzuri au ziwe mbaya na tukifanya hivyo basi mtafanikiwa kuiweka sawa Tanzania yetu na wananchi kuondoa/kupunguza mitazamo hasi.

5. Mambo yapo mengi ila hayo ni machache katika mengi. Fanyeni kuyatatua kwa manufaa ya Tanzania na Watanzania.

Mwisho: Wahusika msikasirike kukosolewa ata kidogo ata siku moja bali pokeeni ushauri ili muweze kufanikiwa zaidi ila mkitaka kusifiwa tu basi tunaelekea pabaya. Binafsi nina umia sana sana nikiona mambo hayaendi ipasavyo na nikisikia maoni ya wananchi wakilalamika na kuwa na mitazamo hasi mingi; by the way mmesikia tafiti ya SDSN inasema Tanzania ni nchi ya 153 kati ya 155 raia wake hawana furaha??!

----------------------------------------

Binafsi sina chama chochote cha siasa hivyo Pls wadau toeni comments zenye tija na sio comments zenye kubeba misimamo ya vyama vyenu, chuki au kutumia kauri mbaya sababu
tunataka kujenga na SIO kubomoa. Asante
 
Uchelewi kuambiwa wewe ni mpiga dili na muuza ngada uliyekuwa unaishi kwa fedha za dili.

Japo ulichoeleza kina ukweli. Na hii serekali ya viwonder ni kama imefeli. Ukitaka kuamini imefeli jaribu kutazama budget yake ya kwanza tu imeshindwa kutekeleza na ata mipanga yao wameshinďwa kuitekeleza mwishoe wameishia kuwa watu wa matukio na kick.
 
A very nice thread.
Binafsi naamini yote uliyosema mwanzo yametokana na kukosekana kwa VISION ya serikali yetu ya awamu ya tano.

With lack of a clear vision then huwezi kuwa na mission. And with lack of a proper mission then obviously hutafanikiwa.
Serikali ya awamu hii hawana vision. Bora hata wangekuja na theoretical vision kama ile ya awamu iliyopita ya KILIMO KWANZA tungewaelewa but the problem is leo hii hatujui tunaelekea wapi.

Tumeambiwa Tanzania ya viwanda well thats just a prospect tunafikaje huko? Kwa mtazamo wa haraka haraka badala ya kuwa na matumaini ya viwanda tumegeuka kuwa Tanzania ya VI~WONDER. Watu wameanza kukata tamaa mapema sana.

Bado ni asubuhi sana lakini matumaini yameshuka very drastically. Lets keep an eye tuone mwisho utavyokuwa coz alwayz the end justifies the means.
 
Umejitahidi kushauri....ila mie mbona naona ajira zinatangazwa kila siku? Taasisi mbalimbali za serikali zimekuwa zikitangaza ajira na kuajiri. Taasisi binafsi pia.

Kitu cha kufanya tumuunge mkono Rais Magufuli katika sera yake ya Tanzania ya Viwanda. Tumeona faida za viwanda huko Mtwara kiwanda cha Dangote kimeajiri watu wengi. Tunaona Bakhressa viwanda vyake pia vimetoa ajira kwa vijana wengi.

Jambo la kukubali ni kwamba Serikali haiwezi kuajiri wahitimu wote pia haiwezi kuacha kusomesha wananchi wake eti kwa kigezo kuwa hakuna ajira....

Lazima tufike pahala kama mzazi ukizaa ujue watoto wako hatima yao ya maisha inaweza kuwaje (walau kuhakikisha maisha yao yanakuwa predictable)

Tukiwa watu wa kulalamika na kujenga vijana wetu wakawa watu wa kulalamika badala ya kuchukua hatua wao wenyewe kujikwamua na tatizo la ajira basi wao ndio watakuwa wenye hasara na sio Serikali. Serikali haitawaletea chakula na kuwalisha mwaka mzima....tuhimizane kufanya kazi. Kujenga nchi sio kazi ndogo na lazima tuumie na tuache 'deko'.
 
Kwa mwaka huu mzima umesikia data au kauli kutoka kwa serekali kuwa imetoa ajira kiasi gani?

Acheni kudanganya watu ajira tunazoziona ni ajira za makada wa ccm tu ambazo ni executive appointee. Lakini hizi za mafungu hakuna hajira iliyowai kutolewa toka huyu aingie madarakani.

Utawala huu umeshindwa kutoa ajira, umefeli kimkakati na kimpango, imekuwa tanzania ya viwonder na matukio pamoja na kick.

Ata ile lugha ya sitawaangusha, mniombee, mimi rais wa wamasikini hakuna tena wamebaki kukimbizana kufungia mitandao ya kijamii na magazeti utafikiri ndio kazi tuliyowatuma kufanya.
 
achene uongo pesa ziko nyingi mtaani ukiona huna pesa ujue zilikuwa si zako ni mpiga dili

Kweli nimeamini wewe ni laki si pesa...

Pls jaribu kuomba macho ya kuona mbali...Usipinge tu kila kitu ili mradi uweze kumtumikia kafiri na kupata...

Jaribu kuweka Tanzania kwanza.
 
Umejitahidi kushauri....ila mie mbona naona ajira zinatangazwa kila siku? Taasisi mbalimbali za serikali zimekuwa zikitangaza ajira na kuajiri. Taasisi binafsi pia.

Kitu cha kufanya tumuunge mkono Rais Magufuli katika sera yake ya Tanzania ya Viwanda. Tumeona faida za viwanda huko Mtwara kiwanda cha Dangote kimeajiri watu wengi. Tunaona Bakhressa viwanda vyake pia vimetoa ajira kwa vijana wengi.

Jambo la kukubali ni kwamba Serikali haiwezi kuajiri wahitimu wote pia haiwezi kuacha kusomesha wananchi wake eti kwa kigezo kuwa hakuna ajira....

Lazima tufike pahala kama mzazi ukizaa ujue watoto wako hatima yao ya maisha inaweza kuwaje (walau kuhakikisha maisha yao yanakuwa predictable)

Tukiwa watu wa kulalamika na kujenga vijana wetu wakawa watu wa kulalamika badala ya kuchukua hatua wao wenyewe kujikwamua na tatizo la ajira basi wao ndio watakuwa wenye hasara na sio Serikali. Serikali haitawaletea chakula na kuwalisha mwaka mzima....tuhimizane kufanya kazi. Kujenga nchi sio kazi ndogo na lazima tuumie na tuache 'deko'.

Dangote ni legacy ya Kikwete...

Baada ya hapo naomba nitajie viwanda ata 20 vipya...Naomba nitajie kazi mpya zilizo tangazwa na Serikali.

Nafahamu Serikali haiwezi kuajiri vijana wote; lakini mbona makampuni binafsi mengine mengi yanazidi kufungwa na wafanyakazi wake kuachishwa kazi??! Ndio mnasema yalikuwa ya wapiga dili??

Biashara watu wanafanya na wanapenda kufanya lakini hali ya Sasa ya kutokuwepo kwa pesa mikononi mwa wananchi kimepunguza kiwango cha Consumer spending hali inayofanya kuwa vigumu kufanya biashara au kazi yoyote binafsi.

Hakuna anae lalamika ndio maana tumeshauri na Kazi yetu ni kushauri tu; la sivyo ningeendelea kukaa kimya tu.

Omba Mungu akupatie macho ili uweze kuona hali iliyopo sasa na Mitazamo hasi ya wananchi...Naipenda sana Tanzania na ndio maana tunashauri. Mkifuata ushauri sawa; Mkisema tuwasifie tu ndio kipimo cha uzalendo pia sawa ila kumbukeni Tanzania inapotea.

Siasa tuweke pembeni na tuiweke Tanzania kwanza kwa manufaa ya Watanzania na kizazi kijacho.
 
Ushauri wako mzuri hasa swala la ajira ni janga, hali ya uchumi kwa sasa si mzuri mzunguko wa hela umekuwa mdogo watu wanafunga biashara, vtu kupanda bei, hafu awamu hii inapenda tu kusifiwa haisikilizi wananchi wao wanajiona wamefika, sioni tatizo kwa malalamiko ya wananchi kutendewa kazi, instead ya kusingizia madawa.
Raisi naye anaropoka bila break bila kujali hali ya wananchi hilo linamgharibu maana wananchi twamuona ana tatizo kubwa, akiendelea hivi sijui hali itakuwa je!?
 
Umejitahidi kushauri....ila mie mbona naona ajira zinatangazwa kila siku? Taasisi mbalimbali za serikali zimekuwa zikitangaza ajira na kuajiri. Taasisi binafsi pia.

Kitu cha kufanya tumuunge mkono Rais Magufuli katika sera yake ya Tanzania ya Viwanda. Tumeona faida za viwanda huko Mtwara kiwanda cha Dangote kimeajiri watu wengi. Tunaona Bakhressa viwanda vyake pia vimetoa ajira kwa vijana wengi.

Jambo la kukubali ni kwamba Serikali haiwezi kuajiri wahitimu wote pia haiwezi kuacha kusomesha wananchi wake eti kwa kigezo kuwa hakuna ajira....

Lazima tufike pahala kama mzazi ukizaa ujue watoto wako hatima yao ya maisha inaweza kuwaje (walau kuhakikisha maisha yao yanakuwa predictable)

Tukiwa watu wa kulalamika na kujenga vijana wetu wakawa watu wa kulalamika badala ya kuchukua hatua wao wenyewe kujikwamua na tatizo la ajira basi wao ndio watakuwa wenye hasara na sio Serikali. Serikali haitawaletea chakula na kuwalisha mwaka mzima....tuhimizane kufanya kazi. Kujenga nchi sio kazi ndogo na lazima tuumie na tuache 'deko'.
 
Huyu mtu atakuf.......a lini jamani nchi iongozwe na mtengeneza ajira .yaaaani jamaaa limekaaa tu linafanya kazi ya kuunguruma na kukoromea watu .
 
Back
Top Bottom