Uchaguzi 2020 Mitano ya Magufuli, Serikali imeshughulikia kero mbalimbali za wananchi

Mathayo Fungo

JF-Expert Member
Nov 13, 2018
319
510
Na Debora C. Kiyuga ✍🏽

Mitano ya Magufuli, Serikali imeshughulikia kero mbalimbali za wananchi, hususan wakulima, wavuvi, wafugaji, wafanyabiashara, wafanyakazi, wajasiliamali na bila kusahau migogoro ya ardhi.

Mitano ya Magufuli, kwa upande wa wakulima, wavuvi, wafugaji na wafanyabiashara; Serikali imefuta takriban tozo 114 zilizokuwa zikikwamisha shughuli zao.

Mitano ya Magufuli, kwa upande wa wafanyakazi Serikali ilitoa fursa ya kuajiri watumishi wapya wenye sifa wapatao 74,173 na ajira zingine bado zinaendelea. Vilevile, iliwapandisha vyeo watumishi 306,917 na kulipa madeni ya watumishi ya mishahara na yasiyo ya mishahara yenye thamani ya shilingi bilioni 472.6

Mitano ya Magufuli, Serikali imepunguza kodi ya mapato kutoka asilimia 11 hadi asilimia 9 na kulipa deni la shilingi trilioni 1.2 ambapo ilikuwa ikidaiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii; na hivyo kuwezesha wastaafu kuendelea kulipwa mafao yao.

Mitano ya Magufuli, kwa upande wa wajasiliamali wadogo, wakiwemo machinga, mama lishe, waendesha bodaboda na bajaji, Serikali imejitahidi kuwawekea utaratibu mzuri wa kuendesha shughuli bila ya kubughudhiwa kwa kuwapatia vitambulisho maalum vilivyotolewa kwa gharama nafuu.

Mwaka jana (2019) jumla ya wajasiliamali wadogo 1,591,085 walipatiwa vitambulisho na hivyo kuwafanya waondokane na usumbufu uliokuwepo zamani kabla ya utaratibu huo kuanza ambapo wajasiliamali wadogo walikuwa wakibugudhiwa sana na mgambo, ikiwemo kunyang’anywa mali zao.

Mitano ya Magufuli, Serikali imetunga Sheria yenye kuzitaka halmashauri zote kutenga asilimia 10 ya mapato yao kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa wanawake (asilimia 4), vijana (asilimia 4) na wenye ulemavu (asilimia 2), ambapo hadi mwezi Machi, kiasi cha shilingi bilioni 93.2 kilikuwa kimetolewa.

Mitano ya Magufuli kwa upande wa migogoro ya ardhi baadhi ya hatua ambazo serikali ilichukua ni kuanzisha Ofisi za Ardhi kwenye Mikoa yote, ambapo sasa huduma zote za upangaji, upimaji, umilikishaji, utathmini pamoja na usajili wa hati, nyaraka, ramani na michoro zinapatikana hali ambayo imeongeza kasi ya urasimishaji makazi ya wananchi na pia utoaji hati.

Mitano ya Magufuli, Jumla ya maeneo ya viwanja yaliyorasimishwa yamefika 764,158 na Serikali imetoa hatimiliki za kimila 515,474. Aidha Serikali imefanya uamuzi wa kuvirasimisha vijiji 920 kati ya 975 vilivyokuwa kwenye maeneo ya hifadhi.

#Magufulimitanotena
 
Waambie warudishe FAO la kujitoa

Magufuli aliondoa FAO la kujitoa

CCM acheni ulaghai, mnapora Pesa za wafanyakazi wanyonge

Bring back Fao la kujitoa
 
Mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano kwa kiasi kikubwa si endelevu...na kama sera na mwelekeo haujabadilishwa basi tutegee hali ngumu ya maisha.

Hali halisi iko hivi.
1. Serikali ina aina kuu mbili za mapato. Mapato ya kodi yanayokusanywa na TRA na mapato yasiyo ya kodi ambayo yana kusanywa na vyombo mbalimbali kama halmashauri, wakala na mamlaka ya serikali. Lakini ukweli ni kwamba fedha hizo zote zilikuwa zinakusanywa ila hazikuwa zina jumuishwa katika mapato ya kodi kama hivi sasa.

Wakati JPM anaingia madarakani alihamisha au kunyang'anya vyanzo vingi vya mapato ya kodi na kuvipeleka TRA. Hali hii ilifanya TRA ionekane inakusanya zaidi kuliko awamu ya kikwete kutoka 800bil hadi 1.x tr

Hali hii imeziacha halmashauri, wakala na mamlaka bila kuwa na fedha za kujiendesha na kuendesha miradi yao midogo midogo. Hivyo kufanya pesa kupotea mtaani.

2. JPM alipoingia madarakani, alifanya crack down ya nguvu kwa wafanyabiashara kwa kuwalazimisha walipe kitu walichokiita malimbikizo ya kodi. Hapa pia fedha nyingi zilikusanywa na kuonyesha mapato yameongezeka. Lakini chanzo hiki cha mapato sasa hivi hakipo tena kilikuwa cha muda tu. Ndo maana sasa hivi TRA hawatangazi mapato ya mwezi. Kwa sababu yanashuka.

3. Halmashauri, wakala, mamlaka na mashirika ya umma yalikuwa na utaratibu wa kuwekeza kiasi fulani cha fedha zao wanazo zalisha kupitia bond, fixed account, Tbills n.k. JPM akasema serikali inafanya biashara na fedha zake akachukua vyedha zote zilizo kuwa zimewekezwa huko.

Hatua hizi tatu zilimfanya JPM awe na kiburi na kujiona nchi ina fedha nyingi mno. Ndo akaanza kusema kuwa hii nchi ni tajiri na inaweza kuwa donor country. Akatumia fedha hizo kufanya miradi yake mikubwa, kununua ndege n.k. Lakini pia chanzo hiki kilikuwa cha muda tu. Hizo fedha hazipo tena.

4. Serikali ikaanzisha utaratibu wa kupunguza matumizi na kuanza kutumia vitu kama force account na wakala wake kutekeleza miradi. Kitu ambacho hawakijui ni kwamba hatua hii pia inaipunguzia serikali kodi. Kwa mfano contractor anapo quote mradi anaweka na kodi za serikali, VAT na mwisho wa siko atalipa coorperate tax. So quote yake itaonekana iko juu. Unapotumia force account hizi fedha hauziweka. Utaonekana umetumia fedha kidogo lakini ujue hakuna kitakacho rudi serikalini.

5. Kwa sababu JPM aliona anafedha nyingi pia akakopa sana. Sasa hivi deni si himilivu tena na uwezo wa kukopa zaidi hatuna.

6. Korosho ilileta hasara. Kutumia jeshi ambao wanalipwa fedha nyingi kama per diem na posho kwenye operation ya korosho ilisababisha watumia fedha nyingi kuliko zilizokusanywa baada ya kuuza.

Matokeo yake.
1. Biashara nyingi zimefungwa hivyo hawakusanyi kodi. Chache zilizopo zinapumlia mashine.

2. Miradi mingi iliyoanzishwa inafanya na makandarasi wa nje, na material zinanunuliwa kutoka nje. Hivyo fedha nyingi zinaenda nje na mzunguko wa fedha ndani unakua kidogo. Hali ya maisha ya watu inakuwa ngumu.
3. Mashirika, wakala na taasisi nyingine za fedha ambazo investment zake ziliporwa sasa zinaanza kuwa tegemezi. Wanategemea serikali kuu ili wajiendeshe...wakati huo huo kodi imepungua sana.

Hitimisho.
Katika kipindi cha pili cha JPM hali ngumu sana. Naweza kusema hataweza kuanzisha mradi mpya na hata iliyopo itaanza kusua sua.

Inabidi apate wachumi wazuri wafanye economic adjustments ya nguvu.

Sent from my CPH1937 using JamiiForums mobile app
 
Hizi ngonjera hizi peleka lumumba. Huku kwetu Nanyamba, Kalelankurunkuru, Imalabhupina, Kazaroho na Mwendakulima hatuzitaki.
 
Magufuli aliondoa FAO la kujitoa

Ni kupora haki za wanyonge

Anakuja kujaza Mabango barabarani ili watu wadanganyika...tutakula Mabango?

Shame on you ccm na mataga

Mnategemea kuiba Kura ...
 
Amekosa kinari kwa Mungu na kwa Watanzania wengi Kuwa Rais wa Tanzania kutokana na matendo yake ya ajabu ajabu.

Kwaheri CCM.
Kwaheri MAGUFURI.
Kwaheri umasikini kwaheri ukoloni.
 
Back
Top Bottom