Unajuwa JPM katika mambo alikuwa dhaifu alikuwa hana break hata siri za intelligence alikuwa anaropoka tu sio kwa nia mbaya ila hakujuwa kuweka kifuani kitu. Kama unakumbuka sijui wakati wa kupokea report ya madini akasema huyu mwenzetu hana hatia kwa maana ni jasusi au siku alipokwenda Airport kukagua machine akamwambia yule Mama hivi wewe hujiulizi kwanini nimekuja kukagua hii machine? unajuwa Rais taasisi kubwa na anapata info nyingi sana daily ila mzee hakuwa na kifua za kuweka siri ndio maana ilikuwa rahisi sana kujuwa anafanya nini maana alikuwa na majibu ya hapo kwa hapo alikuwa na nia safi tu au hulka ya mtu kuna watu hawajui kuweka siri anaweza asilale mpaka aseme ndio usingizi unakuja. Mama sio muongeaji sana na kaweka team mpya ndio maana jamaa kahamia ugomvi wa Simba na Yanga kawa chawa na yeye apate kuishi.sijaelewa alikuwa anapataje siri wakati wa JPM ,Sasa hivi unaona kabisa na yeye pia anategemea connection