Mitandao ya simu ipige faida ya internet kwa mara ya mwisho. Elon Musk kuleta internet ya Starlink Tanzania

Ninawasiwasi na gharama, nadhani itakuwa juu zaid ya mitandao tunayotumia kwasasa hapa Tz
 
Hapa mimi nnamambo mawili yanayonitishia juu ya hili:

1. Umuhimu wa data/internet upo juu kuliko huduma zingine zote zinazotolewa na mitandao ya simu, kwasababu shughuli zote ambazo awali zilikua zinategemea mitandao ya simu zinaweza kukamilishwa na internet na aplikesheni; kwa mawasiliano(Sauti na Ujumbe mfupi kuna aplikesheni kama whatsapp na zinginezo) na hata huduma zingine kama za kibenki, malipo ya serikali nk.... vyote vinahitaji tu uwepo wa internet.

2. Mtawanyo wa internet kwa watanzania bado ni kwa asilimia chache na umejikita zaidi sehemu za mijini huku nchi yetu ikiwa ina watu wengi maeneo ya vijijini. Iwapo mtandao ukaletwa kwa njia ya satelitte na ukawa na kasi, mtandao huo utawahakikishia wa Tanzania uwepo wa mtandao na mawasiliano popote walipo.

Haya maduku duku mawili kama mazingira ya soko huru yatazingatiwa na kwasababu ya kero za mitandao hii kwa saahizi(tozo na beo ghali za vifurushi kwa sasa) sioni jinsi ambavyo makampuni haya yataweza kupona.
 
Ushabiki mbaya mambo sio marahisi kama watu wanavyodhani
Siyo ushabiki mkuu. Hebu niambie lengo gani Elon Musk aliliweka na hakulifikia? Mimi siyo shabiki wa Elon lakini ninachojua yule mwamba hajawahi kuweka lengo na akashindwa kulifikia licha ya changamoto mbalimbali
 
Bado tuna tatizo la kutoelewa bei ya bidhaa na uhalisia
Sasa hivi starlink ni gharama kwa sababu anatumia madishi pia watumiaji wachache. Ila mwakani hata tumia madishi mkuu. Huduma ya internet ataitoa kama wanavyofanya Netflix
 
Musk kuuza kwa individual sizani aisee na ndiyo maana hapo mwenyewe umesema “baadhi ya kampuni” naamini itakuwa B2B
Alisema huduma yake itakuwa na nguvu kubwa kiasi kwamba hakuna dead zone. Kwamba internet itapatikana sehemu zote duniani as long as umejiunga. Kwamba, hata uwe bondeni huko utaweza kuperuzi, tofauti na sasa hivi
 
Yule ana akili lakin anapenda kick sana na mambo sio marahis kama watu wanavyochukulia
Mkuu hivi unajua kuwa watu waliofanikiwa kutuma vyombo kwenye Sayari Ya Mars ni Marekani, China na Elon Musk? Hebu niambie mkuu Elon Musk ametuma kama mtu binafsi na wakati wengi ni Nchi ndiyo zimetuma. Huoni uwezo wa Elon Musk?
 
hili la starlink tushalizungumzia sana starlink sasa hivi ipo kwenye majaribio nchi kadhaa za Africa kama Nigeria na Msumbiji

ada ya mwezi ni $99 (around 240,000) kwa kifurushi cha kawaida na premium ni dola 500 ambayo roughly ni 1.2m

hio ni satelite internet ambayo ina speed mbovu tu hasa latency, inauzwa laki 2 na 40 kwa mwezi, huwezi cheza games vizuri na vitu vingi ambavyo una live stream havitakua vizuri

fiber, 4g na 5g zote zina speed nzuri kuliko starlink, TTCL kuanzia 55,000, voda 5G kuanzia 120,000, zuku kuanzia 69,000 etc ni much better.

starlink waachie watu wa vijijini mkuu wenye pesa, haitaondoa mtandao wowote ule wa Tanzania.
Mkuu kuna mageuzi yoyote uliyowahi kushuhudia, kusoma au kusikia yalitokea tu ghafla na kuwa bora? Mkuu hiyo simu unayotumia hapo sasa hivi ni simu bora kuliko simu uliyotumia mwaka 2015. Hata hivyo wewe mwenyewe unajua ukweli kuwa, ukichukua simu uliyokuwa unaitumia mwaka 2015 halafu uweke applications za sasa hivi simu yako haitakubali kuweka hizo applications, hata kama itakubali haitaweza kurun hizo applications. Naishia hapa, ila nadhani umeelewa namanisha nini hapa
 
Hapo hatujajua bei itakuwaje. Ingawa yule lazima ataleta ushindani mkubwa
Karibu 200,000+ per month in Europe- na inategemea na eneo, ila speed yake ni kubwa sana- Kyiv ind.
Ni nzuri sana makampuni, lakini kwa household ni mtihani upande wa gharama. Na inasaidia sana internet kwenye remote areas.
 
Nyinyi mnataka internet ya Elon Musk iwe na kasi kubwa wakati ndiyo kwanza ina anza kutumika? Kama kuna makampuni yanatumia Starlink basi tambua kuwa internet ya starlink ina kasi kubwa. Makampuni yasingeweza kuinstall starlink kama kasi yake ni mbovu
 
Karibu 200,000+ per month in Europe- na inategemea na eneo, ila speed yake ni kubwa sana- Kyiv ind.
Ni nzuri sana makampuni, lakini kwa household ni mtihani upande wa gharama. Na inasaidia sana internet kwenye remote areas.
Mkuu hiyo gharama ni kubwa kwa sababu ndiyo kwanza ana anza. Baada ya muda itapungua mkuu. Kama mtu ananunua king'amuzi kwa 160000 - 250000, na kulipia kila mwezi, mtu huyo hatashindwa kulipia gharama ya internet.
 
hili la starlink tushalizungumzia sana starlink sasa hivi ipo kwenye majaribio nchi kadhaa za Africa kama Nigeria na Msumbiji

ada ya mwezi ni $99 (around 240,000) kwa kifurushi cha kawaida na premium ni dola 500 ambayo roughly ni 1.2m

hio ni satelite internet ambayo ina speed mbovu tu hasa latency, inauzwa laki 2 na 40 kwa mwezi, huwezi cheza games vizuri na vitu vingi ambavyo una live stream havitakua vizuri

fiber, 4g na 5g zote zina speed nzuri kuliko starlink, TTCL kuanzia 55,000, voda 5G kuanzia 120,000, zuku kuanzia 69,000 etc ni much better.

starlink waachie watu wa vijijini mkuu wenye pesa, haitaondoa mtandao wowote ule wa Tanzania.
Kuna makala Kyiv independent wali-publish mwezi uliopita ikihusisha subject experts mbalimbali, wanasema speed yake ni kubwa sana na ni very secure, na ndo inasaidia critical infrastructures zote Ukraine hasa military kwenye ku-coordinate mashambulizi kupitia advanced systems mbalimbali.
 
Huwezi kukaa mars week nzima ukatoboa.

Idea zake ni theoretical sana, life in mars.
Eti duniani kuna siku haitakua salama
Jamaa anacheza na akili zetu
Mkuu tambua kuwa wagunduzi wote wakubwa walionekana ni too theoretical walipoanza safari yao. Ila baadae wote waliosema ni too theoretical walinyamaza kwa aibu. Pia wote waliogundua vitu vikubwa walionekana kama watu walio changanyikiwa
 
Mkuu hiyo gharama ni kubwa kwa sababu ndiyo kwanza ana anza. Baada ya muda itapungua mkuu. Kama mtu ananunua king'amuzi kwa 160000 - 250000, na kulipia kila mwezi, mtu huyo hatashindwa kulipia gharama ya internet.
Ni very expensive.

Ukraine info.

Starlink monthly subscription fee $60

"However, Ukrainians do not rush to jump on the bandwagon because Starlink is expensive. Ukraine has one of the cheapest internets in the world – about $7.40 for a monthly package (in the U.S. it costs $55, in Canada – $68, in the U.K. – $39)."
 
Kuna makala Kyiv independent wali-publish mwezi uliopita ikihusisha subject experts mbalimbali, wanasema speed yake ni kubwa sana na ni very secure, na ndo inasaidia critical infrastructures zote Ukraine hasa military kwenye ku-coordinate mashambulizi kupitia advanced systems mbalimbali.
Mkuu nashukuru sana kwa kulitolea ufafanuzi hili. Wengi wapo negative sana mkuu
 
Back
Top Bottom