Uchaguzi 2020 Mitandao ya kijamii Tanzania yawa restricted. YouTube, WhatsApp, Twitter, JamiiForums na Telegram zimeguswa - Oktoba 27, 2020

Screen ST1.jpeg


Twitch kajumuishwa katika kundi! Aisee hii ni Serikali, CCM au CCP?
 
Wamefanya Kitu sahihi sana mana wamewapa raia wa kitanzania hususani mimi na wew ili tuweze kupitia ilani ya kila chama pamoja na será zao ili tukafanye maamuz yalio sahihi, tátizo Sio viongoz wajinga tatz n wajinga wanao chagua viongoz wajinga. Sio swala lá kueka mjadala wakuu hiii n kwa Léo tu kesho Mamb yatakua sawa
 
Wamefanya Kitu sahihi sana mana wamewapa raia wa kitanzania hususani mimi na wew ili tuweze kupitia ilani ya kila chama pamoja na será zao ili tukafanye maamuz yalio sahihi, tátizo Sio viongoz wajinga tatz n wajinga wanao chagua viongoz wajinga. Sio swala lá kueka mjadala wakuu hiii n kwa Léo tu kesho Mamb yatakua sawa
Watu wakishachaguliwa unadhani hizo ilani wanaziheshimu tena?
Wanadonoa mawili matatu halafu wanaanza kuwinda kura za msimu ujao.
 
Moderators hamtendi haki kuunganisha posts. Hili la kufikiri kwa niaba yetu members wenu sio sahihi. Mnaviza na kufifisha fikra zetu. Acheni tabia hii. Kama post haina wachangiaji inajiondoa yenyewe.

Moja ya mambo yaliyosababisha nikawakimbia kwa muda mrefu ni hilo la kuunganisha mawazo na maoni ya wachangiaji wenu humu.
 
Najaribu kuingia YouTube lakini inagoma, kama nusu saa iliyopita nilikuwa naipata.

Kuna yeyote anapata tatizo kama langu?

Natumia Mtandao wa Tigo

PIA SOMA
= >
Wanaandaa mazingira ya wizi.
 
Tulianza kifungia magazeti

Tukafunga radio na channel za mtandaoni online tv tusizozipenda

Tukakataza tv na radio kutangaza habari yoyote ambayo haijafanyiwa uhakiki na serikali

Tukalazimisha tbc irushe matangazo ya aina moja tu masaa 24

Tukahamia kwa tv na radio binafsi zisirushe matangazo ya wapinzani

Mtaani kukawa nyomi kwenye mikutano ya siasa hadi kanda ya ziwa wakasema Ni yeye 2020

Tukasema hatutaki kura za mitandao ila mwisho tukaprove hatutakiwi

Tumezima mitandao yote watu wasitume taarifa ya kinachoendelea. Tukanyima mawakala wasiingie na simu kwenye vituo lakini pia tukazuia group sms

Lengo ni Nini? Nikuliweka taifa gizani kihabari, nikukwepa fedhea.

Je, mnaamini sanduku la kura likishindwa nafsi zitakuwa na amani na ninyi? Mlikataa uchaguzi wa serikali za mitaa lakini mliowapitisha huko wote hakuna lolote walilofanya kusaidia uchaguzi mkuu, hivyohivyo pia hata mkipata wabunge wote hawataweza kuwasaidia maana ukweli awawasaidiii wananchi wanasaidia familia na chama.
 
Najaribu kuingia YouTube lakini inagoma, kama nusu saa iliyopita nilikuwa naipata.

Kuna yeyote anapata tatizo kama langu?

Natumia Mtandao wa Tigo

PIA SOMA
= >
Hata mm mpaka nimeshangaa. Haifunguki fb WhatsApp SMS wala picha haziendi
 
Back
Top Bottom