Mitandao ya kijamii siku hizi imekuwa chanzo kikubwa cha stress na msongo wa mawazo kwa vijana

Youngblood

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
18,919
54,990
Wakuu habari zenu, leo kidogo tuzungumzie kuhusu hili la mitandao ya kijamii.

Siku hizi maisha yamegeuka sana, ni ngumu sana kudeal na stress na msongo wa mawazo hasa pale unapokuwa unapitia kipindi kigumu katika maisha.

~Umeachana na mpenzi wako uliyempenda sana, kesho unamuona facebook, instagram or WhatsApp anakula maisha na mpenzi mpya tena aliyekuzidi viwango.

~Unaperuzi facebook mara unakutana na picha za jamaa uliowaacha shule tena wale vilaza kabisa wanakula good time, wakati huo wewe upo tu nyumbani kwa shemeji na vyeti vyako vya chuo havina kazi.

~Hujabahatika kupata mtoto, unapita mitandaoni watu wanapost picha za birthday za watoto wao, huku upande wako mawifi wanakusakama kila kukicha kwamba unakula tu na kujaza choo.

~Au unapitia chats kwenye group unakutana na mapicha wenzako wote uliosoma nao wanaolewa huku wewe upo nyumbani umezalishwa huna mbele wala nyuma.

~Ni ngumu sana kukutana na hizo mambo ukapotezea, lazima zitakuathiri kwa kiasi flani na mara nyingi husababisha watu kupata hali ya upweke, mfadhaiko, wivu uliopindukia au kumfanya mtu awe depressed na mara chache watu huishia kujiua kabisa.
 
Mkuu umenigusa sana nikionaga watu na watoto nahisi kama wao ni special sana aisee..
Unachokisema ni kweli wakati mwingine unamu unfollow mtu maana anachangia hoja kubwa ya kukunyanyasa kifikra bila yeye kujua
Kuna watu yani since day 1 wao mambo yao hayajawahi kupinda ..bora Jf hatuonani aisee
 
Mkuu umenigusa sana nikionaga watu na watoto nahisi kama wao ni special sana aisee..
Unachokisema ni kweli wakati mwingine unamu unfollow mtu maana anachangia hoja kubwa ya kukunyanyasa kifikra bila yeye kujua
Kuna watu yani since day 1 wao mambo yao hayajawahi kupinda ..bora Jf hatuonani aisee
Tuko wengi kwakwel

Ila yote n life tu Bora uhai sasa
 
Mie nafurahia sana hizo nyakati, najifunza vitu na kunipa ari ya kutimiza ndoto zangu.

Ikiwa wao wanaigiza, mie nafanya kweli, ila sijawahi kufadhaika au kuchukia mtu kisa mambo ya mtandao au maisha anayoishi amenizidi. Nachukulia kama changamoto tu.
 
Poleni sana...

Usiamini kile unachoona au kusikia kutoka kwenye mitandao ya jamii ni cha kuamini...



Cc: mahondaw
 
Ni kweli kabisa...Ila kitu cha muhimu, maisha yanayooneshwa kwenye Facebook siyo halisi... Kwanini nasema siyo halisi..? Siyo halisi kwasababu watu wanaonesha side moja ya maisha yao...yani ule upande wa raha, na kula bata...lakini maisha hayapo hivyo...kuna upande mwingine...kuna magonjwa, misuko suko, njaa, kiu, masumbuko,, mabalaa...hivi watu hawataki kuvionesha...
 
Back
Top Bottom