Mitandao inasaidia; Nimeokota hand-bag yenye pesa kabla ya mateja / vibaka na kumrudishia aliyeidondosha kupitia Instagram

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
18,857
2,000
Najua wengi mtaniona mjinga lakini niwaambie tu kwamba maumivu ya mtu unaemwibia, unaemdhurumu, n.k huwa yanaziba baraka zako. huwezi kujifariji kwamba umeokota wallet ambayo ina kitambulisho chenye taarifa za kumpata huyo mtu na ukapuuzia kumtafuta kwa kisingizio cha "cha kuokota si cha kuiba mwenye mali ni..."
Siku nyingine uwe makini vinginevyo utaunganishwa kwenye kesi ya hatari sana.
 

Kwekitui

JF-Expert Member
Oct 29, 2017
892
1,000
MUHIMU: Tahadhari inabidi zichukuliwe, Wema wako unaweza kuku gharimu! kabla hujachukua uamuzi wa kumrejeshea mtu vitu vyake ni lazima upate taarifa zake (ni mzima?, kapata tukio lipi?, nk) lasivyo unaweza kuingia mtegoni au kuhusishwa na kesi.. kama huna taarifa ni bora utafute njia ya kukirudisha ulichokiokota kisiri siri bila kuacha alama wala kujulikana au ikibidi uvipeleka polisi japo hawaaminiki, Binafsi niliridhishwa na ushirikiano wa upande wa pili hivyo sikuwa na wasiwasi .

Leo hii wakati nimeamka kufanya mazoezi asubuhi, nilikikuta kipochi cha mkononi (hand bag) kwenye njia ambayo huwa nafanya jogging, Nilichunguza mazingira vizuri na nikakifungua, nilikuta noti 132 za elf 10 pamoja na noti nyingine chache, flash, na kitambulisho.

Well, nikaibeba, nikaendelea na mazoezi yangu. Nilipofika nyumbani niliingia facebook na kumtafuta huyo mtu nikamkosa, niliingia twitter nilimkosa, Bahati ilioje niliingia Instagram nikamkuta kwa picha ile ile kama ya kwenye kitambulisho. hakika ilikuwa ni bahati kwa aliidondosha maana ingeokotwa na teja au kibaka ingekuwa ni historia.

nilimtumia meseji kwa account yangu ya pili (akaunti rapa) aniambie kama kuna shida imempata na anitumie verificaton picture (hapa nilimwambia anitumie picha kashika kikombe ili nijiridhishe ni yeye na sio picha za galley au za kudownload), baada ya lisaa hivi wakati nikiwa nakunywa chai nilipokea meseji yake ambayo alilenga moja kwa moja kwa shida iliyompata kuhusu kupoteza hio hand bag, kuhusu picha alisita mara ya kwanza ila nilipomwambia bila picha sitoi ushirikiano, ilibidi apige picha kashikilia kikombe)

Basi nilimwambia aondoe shaka, ninayo hio wallet, Nilimwambia aje kupitia wallet yake chumba cha mapokezi sehemu napofanyia kazi kwasababu mimi huwa sipo ofisi kuu muda mwingi (niliscreen shot hizo chats na kuzitunza online zije kuwa msaada likitokea la kutokea)

alikaja kuichukua wallet yake saa nne lakini huwezi amini kanisubiri mpaka nimerudi saa nane mchana huku akiwa haamini amini kwamba niliiwahi hio wallet badala ya Teja au kibaka.

Najua wengi mtaniona mjinga lakini niwaambie tu kwamba maumivu ya mtu unaemwibia, unaemdhurumu, n.k huwa yanaziba baraka zako. huwezi kujifariji kwamba umeokota wallet ambayo ina kitambulisho chenye taarifa za kumpata huyo mtu na ukapuuzia kumtafuta kwa kisingizio cha "cha kuokota si cha kuiba mwenye mali ni..."

Anadai hio hand bag yawekezaka aliidondosha bila kujua akiwa kwenye chombo cha usafiri, Kanibembeleza sana kunipa kiasi flani kama shukrani lakini nilikataa, aliendelea kunibembeleza sana mpaka nikaanza kuona wazi wazi kukataa kwangu ni kama kunamuumiza hivi kwa kuona namdharau, ikabidi kishingo upande nichukue kiasi kidogo sana ili kumpooza roho.

Teknolojia inasaidia sana
132x10 ongeza na 000
Sio pesa nyingi kushinda utu
 

ankol

JF-Expert Member
Aug 21, 2012
1,409
2,000
Niliwahi kuokota wallet ya jamaa nikigombea daldala maeneo ya shule ya uhuru. Nilifika home nikakutana na mavitambulisho kibao pamoja na pesa elfu hamsini hivi.
Dah nilimwonea sana huruma mshkaji kwa jinsi ya maelezo nilokutana kwenye business card inaonyesha anafanya kazi ya udereva kwa wahindi
Kasheshe likaanza nitawezaje kumrudishia mavitambulisho yake pamoja na driving license.
Nikakiuliza baada ya wiki hivi nikampigia simu tukutane kariakoo nikampea alinishukuru sana japokua pesa nilishaitumia.
 

reymage

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,504
2,000
Ila haya mambo nahisi yanaendeshwa pasi na weledi, hivi kweli mtu aue then akae na simu mumpigie apokwe awaelekeze hadi alipo mkamdake!! It doesnt make sense, sema tu wenye mamlaka huwa hawataki kujiongeza kufanya upelelezi na ukute hata huo weledi wa kufanya upelelezi hawana.
Askari wabongo wanatafuta wa kumfia tu!
 

reymage

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,504
2,000
Hawajitumi yaani kuna kaka mmoja nae ilishamtokea mtaani kwetu mda km 15 yrs imepita zilikutwa picha eneo la ujambazi za kwake bahati njema siku ya tukio alilazwa temeke hospital alikua ana wiki nzima tukio linatokea yuko Hosp siku anaruhusiwa kesho yake anakamatwa yaani ilikua patashika sema ndo aliponea hapo!la sivyo angekua jela mbona mpk Leo!
 

Habun

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
73,034
2,000
Hawajitumi yaani kuna kaka mmoja nae ilishamtokea mtaani kwetu mda km 15 yrs imepita zilikutwa picha eneo la ujambazi za kwake bahati njema siku ya tukio alilazwa temeke hospital alikua ana wiki nzima tukio linatokea yuko Hosp siku anaruhusiwa kesho yake anakamatwa yaani ilikua patashika sema ndo aliponea hapo!la sivyo angekua jela mbona mpk Leo!
Aiseeeh! Wengi wanatumikia vifungo sio vyao kwa uzembe wa watu tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom