Mitandao inasaidia; Nimeokota hand-bag yenye pesa kabla ya mateja / vibaka na kumrudishia aliyeidondosha kupitia Instagram

Hornet

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
23,928
2,000
Umejenga msingi mzuri wa kuwaliza watu jf pindi utakapokuja na biashara ya tuma nikutumie mzigo.

Mkuu Kama una roho mbaya siyo watu wote wapo hivyo

Kuna watu wema kibao

Jana nimemuhudumia mteja wa online huko hata simfahamu nikapiga hesabu ikapungua laki Moja Yule mteja nikamtumia mzigo wake na akapokea akalipa baada ya nusu saa akanipigia akaniambia tu nimekosea hesabu
Nakurushia kiasi kilichobakia.


Nadhani ingekuwa ni wewe wala usingerudisha
 

reymage

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,504
2,000
kwenye uislam ukiokota kitu unatakiwa umtafute mwenyewe au utangaze.
Kwa hyo zote hizo ukishindwa kumuona hyo Mali NI yako.
Sasa Mimi nisingetangaza Wala kumtafuta.
My dad huu unaenda mwezi wa pili au wa 3ana pochi ya mtu ina pesa sijui za nchi gani hukoo anakuambia situmii mpk nimpate mwenyewe aliokota maeneo ya Regency nimemuambia anipe nitangazekachomoa!!!

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
12,682
2,000
Leo hii wakati nimeamka kufanya mazoezi asubuhi, nilikikuta kipochi cha mkononi (hand bag) kwenye njia ambayo huwa nafanya jogging, Nilichunguza mazingira vizuri na nikakifungua, nilikuta noti 132 za elf 10 pamoja na noti nyingine chache, flash, na kitambulisho.
Mimi sina demu, kwahiyo haya mambo ya handbags wala siyafahamu...

Hivi handbags si ndo zile wadada huwa wanashika mkononi au kuning'iniza begani?!

Kama ndivyo, how come tena mtu anadondosha handbag bila kufahamu, tena njiani?

Ingekuwa kwenye daladala, wala nisingeshangaa!!

Ni kwamba alikuwa anajisaidia, kwahiyo akaiweka chini na kuisahau hapo hapo, au?!

Kuhusu kuonekana mjinga kisa umerudisha, kwangu mimi HAPANA, manake katu nami nisingeweza kuzuia wakati nafahamu kabisa kuna uwezekano wa mwenyewe kupatikana!!

Na lau kama lingeniingia shetani la kunifanya nisimrudishie hiyo pesa, I swear hilo jinamizi lingeendelea kunitafuna maisha yangu yote yaliyosalia hapa duniani!!
 

Habun

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
73,034
2,000
Kuna shemeji yangu aliokota simu 2013 amekaa nayo asubiri atakayepiga smu ampe maelekezo jinsi ya kuipata!! Ilikua asubuhi kufika saa kumi jioni ikapigwa simu akatoa maelekezo waende ofisini kwake smu aliokota asubuhi wkt anaenda kazini!!mwaka 2017.

Akahukumiwa kunyongwa Hadi kufa Hadi Leo Yuko gerezani !!bahati nzuri ameitwa kwenye kikao Cha rufaa ya hukumu yake tareh 23 mwezi huu anasikiliza rufaa yako ,naamini Mungu atawaongoza majaji wampe haki yake.

Ile smu kumbe ilikua ya mjeshi kapigwa Hadi kafa na vibaka wkt wanakimbia ndio wakaidondosha na yeye akapita hapo akaiona na kuiokota
Ila haya mambo nahisi yanaendeshwa pasi na weledi, hivi kweli mtu aue then akae na simu mumpigie apokee awaelekeze hadi alipo mkamdake!! It doesnt make sense, sema tu wenye mamlaka huwa hawataki kujiongeza kufanya upelelezi na ukute hata huo weledi wa kufanya upelelezi hawana.
 

Rodwell mTZ

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
792
1,000
Angek
Kuna siku utapewa kesi ya mauaji au ubakaji ndio utajua hujui,huyo mtu angekuwa kauawa sasa hivi ungekuwa segerea,usirudie ujinga huo
AngekuWa ameuwawa asingetuma picha inayoonyesha ameshika kikombe,hebu soma vizuri hiyo nada.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom