Mitandao inasaidia; Nimeokota hand-bag yenye pesa kabla ya mateja / vibaka na kumrudishia aliyeidondosha kupitia Instagram

Wema unasaidia sana! Kuna siku mother mmoja alituma pesa kimakosa ikaja kwangu! Ni zamani kidogo kipindi hicho hakuna option yakurudisha muamala wa pesa!

Basi yule maza akapiga simu kwangu,akiniomba nirudishe ile pesa kakosea,zilikua za matibabu! Kweli nikarudisha zile pesa! Akashukuru sana, matibabu ya mgojwa wake yakenda vizuri na mgojwa wake akapona,basi kuna siku akaniita kwake,nikaenda tukafahamiana vizuri mno! Kumbe yule mother ni Director of HR wa Taasisi moja ya serikali! Wakaja wakatangaza kazi,alikua wa kwanza kuniambia kama nina mtu ana vigezo ampe kazi! Kweli sister aliomba na kazi akapata,sasa hivi sister na yeye ni mnene mnene kidogo kwenye hiyo taasisi! Mother kastafu mwaka Jana! Ila kamwacha sister sehemu nzuri sana! Na tushakua ndugu kabisa!
Mungu na azidi kukutendea.
 
MUHIMU: Tahadhari inabidi zichukuliwe, Wema wako unaweza kuku gharimu! kabla hujachukua uamuzi wa kumrejeshea mtu vitu vyake ni lazima upate taarifa zake (ni mzima?, kapata tukio lipi?, nk) lasivyo unaweza kuingia mtegoni au kuhusishwa na kesi.. kama huna taarifa ni bora utafute njia ya kukirudisha ulichokiokota kisiri siri bila kuacha alama wala kujulikana au ikibidi uvipeleka polisi japo hawaaminiki, Binafsi niliridhishwa na ushirikiano wa upande wa pili hivyo sikuwa na wasiwasi . Leo hii wakati nimeamka kufanya mazoezi asubuhi, nilikikuta kipochi cha mkononi (hand bag) kwenye njia ambayo huwa nafanya jogging, Nilichunguza mazingira vizuri na nikakifungua, nilikuta noti 132 za elf 10 pamoja na noti nyingine chache, flash, na kitambulisho. Well, nikaibeba, nikaendelea na mazoezi yangu. Nilipofika nyumbani niliingia facebook na kumtafuta huyo mtu nikamkosa, niliingia twitter nilimkosa, Bahati ilioje niliingia Instagram nikamkuta kwa picha ile ile kama ya kwenye kitambulisho. hakika ilikuwa ni bahati kwa aliidondosha maana ingeokotwa na teja au kibaka ingekuwa ni historia. nilimtumia meseji kwa account yangu ya pili (akaunti rapa) aniambie kama kuna shida imempata na anitumie verificaton picture (hapa nilimwambia anitumie picha kashika kikombe ili nijiridhishe ni yeye na sio picha za galley au za kudownload), baada ya lisaa hivi wakati nikiwa nakunywa chai nilipokea meseji yake ambayo alilenga moja kwa moja kwa shida iliyompata kuhusu kupoteza hio hand bag, kuhusu picha alisita mara ya kwanza ila nilipomwambia bila picha sitoi ushirikiano, ilibidi apige picha kashikilia kikombe) Basi nilimwambia aondoe shaka, ninayo hio wallet, Nilimwambia aje kupitia wallet yake chumba cha mapokezi sehemu napofanyia kazi kwasababu mimi huwa sipo ofisi kuu muda mwingi (niliscreen shot hizo chats na kuzitunza online zije kuwa msaada likitokea la kutokea) alikaja kuichukua wallet yake saa nne lakini huwezi amini kanisubiri mpaka nimerudi saa nane mchana huku akiwa haamini amini kwamba niliiwahi hio wallet badala ya Teja au kibaka. Najua wengi mtaniona mjinga lakini niwaambie tu kwamba maumivu ya mtu unaemwibia, unaemdhurumu, n.k huwa yanaziba baraka zako. huwezi kujifariji kwamba umeokota wallet ambayo ina kitambulisho chenye taarifa za kumpata huyo mtu na ukapuuzia kumtafuta kwa kisingizio cha "cha kuokota si cha kuiba mwenye mali ni ....." Anadai hio hand bag yawekezaka aliidondosha bila kujua akiwa kwenye chombo cha usafiri, Kanibembeleza sana kunipa kiasi flani kama shukrani lakini nilikataa, aliendelea kunibembeleza sana mpaka nikaanza kuona wazi wazi kukataa kwangu ni kama kunamuumiza hivi kwa kuona namdharau, ikabidi kishingo upande nichukue kiasi kidogo sana ili kumpooza roho. Teknolojia inasaidia sana

WA-IMG-20211111-774d431e.jpg
 
MUHIMU: Tahadhari inabidi zichukuliwe, Wema wako unaweza kuku gharimu! kabla hujachukua uamuzi wa kumrejeshea mtu vitu vyake ni lazima upate taarifa zake (ni mzima?, kapata tukio lipi?, nk) lasivyo unaweza kuingia mtegoni au kuhusishwa na kesi.. kama huna taarifa ni bora utafute njia ya kukirudisha ulichokiokota kisiri siri bila kuacha alama wala kujulikana au ikibidi uvipeleka polisi japo hawaaminiki, Binafsi niliridhishwa na ushirikiano wa upande wa pili hivyo sikuwa na wasiwasi .

Leo hii wakati nimeamka kufanya mazoezi asubuhi, nilikikuta kipochi cha mkononi (hand bag) kwenye njia ambayo huwa nafanya jogging, Nilichunguza mazingira vizuri na nikakifungua, nilikuta noti 132 za elf 10 pamoja na noti nyingine chache, flash, na kitambulisho.

Well, nikaibeba, nikaendelea na mazoezi yangu. Nilipofika nyumbani niliingia facebook na kumtafuta huyo mtu nikamkosa, niliingia twitter nilimkosa, Bahati ilioje niliingia Instagram nikamkuta kwa picha ile ile kama ya kwenye kitambulisho. hakika ilikuwa ni bahati kwa aliidondosha maana ingeokotwa na teja au kibaka ingekuwa ni historia.

nilimtumia meseji kwa account yangu ya pili (akaunti rapa) aniambie kama kuna shida imempata na anitumie verificaton picture (hapa nilimwambia anitumie picha kashika kikombe ili nijiridhishe ni yeye na sio picha za galley au za kudownload), baada ya lisaa hivi wakati nikiwa nakunywa chai nilipokea meseji yake ambayo alilenga moja kwa moja kwa shida iliyompata kuhusu kupoteza hio hand bag, kuhusu picha alisita mara ya kwanza ila nilipomwambia bila picha sitoi ushirikiano, ilibidi apige picha kashikilia kikombe)

Basi nilimwambia aondoe shaka, ninayo hio wallet, Nilimwambia aje kupitia wallet yake chumba cha mapokezi sehemu napofanyia kazi kwasababu mimi huwa sipo ofisi kuu muda mwingi (niliscreen shot hizo chats na kuzitunza online zije kuwa msaada likitokea la kutokea)

alikaja kuichukua wallet yake saa nne lakini huwezi amini kanisubiri mpaka nimerudi saa nane mchana huku akiwa haamini amini kwamba niliiwahi hio wallet badala ya Teja au kibaka.

Najua wengi mtaniona mjinga lakini niwaambie tu kwamba maumivu ya mtu unaemwibia, unaemdhurumu, n.k huwa yanaziba baraka zako. huwezi kujifariji kwamba umeokota wallet ambayo ina kitambulisho chenye taarifa za kumpata huyo mtu na ukapuuzia kumtafuta kwa kisingizio cha "cha kuokota si cha kuiba mwenye mali ni ....."

Anadai hio hand bag yawekezaka aliidondosha bila kujua akiwa kwenye chombo cha usafiri, Kanibembeleza sana kunipa kiasi flani kama shukrani lakini nilikataa, aliendelea kunibembeleza sana mpaka nikaanza kuona wazi wazi kukataa kwangu ni kama kunamuumiza hivi kwa kuona namdharau, ikabidi kishingo upande nichukue kiasi kidogo sana ili kumpooza roho.

Teknolojia inasaidia sana
Alikuwa wa jinsia gani na wewe ni wa jinsia gani? Isije ikawa kulikuwa na mvuto wa positive and negative charges.
 
Kuna shemeji yangu aliokota simu 2013 amekaa nayo asubiri atakayepiga smu ampe maelekezo jinsi ya kuipata!! Ilikua asubuhi kufika saa kumi jioni ikapigwa simu akatoa maelekezo waende ofisini kwake smu aliokota asubuhi wkt anaenda kazini!!mwaka 2017 akahukumiwa kunyongwa Hadi kufa Hadi Leo Yuko gerezani !!bahati nzuri ameitwa kwenye kikao Cha rufaa ya hukumu yake tareh 23 mwezi huu anasikiliza rufaa yako ,naamini Mungu atawaongoza majaji wampe haki yake
Ile smu kumbe ilikua ya mjeshi kapigwa Hadi kafa na vibaka wkt wanakimbia ndio wakaidondosha na yeye akapita hapo akaiona na kuiokota
Maaskari wapepelezi wabongo wavivu sana kufatilia kesi yaani wanakubabatiza mradi umekamatwa na kidhibiti!ukiangalia IDX ndo utajua wazungu wako makini kiasi gani

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
MUHIMU: Tahadhari inabidi zichukuliwe, Wema wako unaweza kuku gharimu! kabla hujachukua uamuzi wa kumrejeshea mtu vitu vyake ni lazima upate taarifa zake (ni mzima?, kapata tukio lipi?, nk) lasivyo unaweza kuingia mtegoni au kuhusishwa na kesi.. kama huna taarifa ni bora utafute njia ya kukirudisha ulichokiokota kisiri siri bila kuacha alama wala kujulikana au ikibidi uvipeleka polisi japo hawaaminiki, Binafsi niliridhishwa na ushirikiano wa upande wa pili hivyo sikuwa na wasiwasi .

Leo hii wakati nimeamka kufanya mazoezi asubuhi, nilikikuta kipochi cha mkononi (hand bag) kwenye njia ambayo huwa nafanya jogging, Nilichunguza mazingira vizuri na nikakifungua, nilikuta noti 132 za elf 10 pamoja na noti nyingine chache, flash, na kitambulisho.

Well, nikaibeba, nikaendelea na mazoezi yangu. Nilipofika nyumbani niliingia facebook na kumtafuta huyo mtu nikamkosa, niliingia twitter nilimkosa, Bahati ilioje niliingia Instagram nikamkuta kwa picha ile ile kama ya kwenye kitambulisho. hakika ilikuwa ni bahati kwa aliidondosha maana ingeokotwa na teja au kibaka ingekuwa ni historia.

nilimtumia meseji kwa account yangu ya pili (akaunti rapa) aniambie kama kuna shida imempata na anitumie verificaton picture (hapa nilimwambia anitumie picha kashika kikombe ili nijiridhishe ni yeye na sio picha za galley au za kudownload), baada ya lisaa hivi wakati nikiwa nakunywa chai nilipokea meseji yake ambayo alilenga moja kwa moja kwa shida iliyompata kuhusu kupoteza hio hand bag, kuhusu picha alisita mara ya kwanza ila nilipomwambia bila picha sitoi ushirikiano, ilibidi apige picha kashikilia kikombe)

Basi nilimwambia aondoe shaka, ninayo hio wallet, Nilimwambia aje kupitia wallet yake chumba cha mapokezi sehemu napofanyia kazi kwasababu mimi huwa sipo ofisi kuu muda mwingi (niliscreen shot hizo chats na kuzitunza online zije kuwa msaada likitokea la kutokea)

alikaja kuichukua wallet yake saa nne lakini huwezi amini kanisubiri mpaka nimerudi saa nane mchana huku akiwa haamini amini kwamba niliiwahi hio wallet badala ya Teja au kibaka.

Najua wengi mtaniona mjinga lakini niwaambie tu kwamba maumivu ya mtu unaemwibia, unaemdhurumu, n.k huwa yanaziba baraka zako. huwezi kujifariji kwamba umeokota wallet ambayo ina kitambulisho chenye taarifa za kumpata huyo mtu na ukapuuzia kumtafuta kwa kisingizio cha "cha kuokota si cha kuiba mwenye mali ni ....."

Anadai hio hand bag yawekezaka aliidondosha bila kujua akiwa kwenye chombo cha usafiri, Kanibembeleza sana kunipa kiasi flani kama shukrani lakini nilikataa, aliendelea kunibembeleza sana mpaka nikaanza kuona wazi wazi kukataa kwangu ni kama kunamuumiza hivi kwa kuona namdharau, ikabidi kishingo upande nichukue kiasi kidogo sana ili kumpooza roho.

Teknolojia inasaidia sana

Bwana mzehe,, hongera ssana,,, wachache kama wewe,,, acha wakuite mjinga,,, lakini wewe co mjinga,,,,
 
Umejenga msingi mzuri wa kuwaliza watu jf pindi utakapokuja na biashara ya tuma nikutumie mzigo.

Mkuu Kama una roho mbaya siyo watu wote wapo hivyo

Kuna watu wema kibao

Jana nimemuhudumia mteja wa online huko hata simfahamu nikapiga hesabu ikapungua laki Moja Yule mteja nikamtumia mzigo wake na akapokea akalipa baada ya nusu saa akanipigia akaniambia tu nimekosea hesabu
Nakurushia kiasi kilichobakia.

Nadhani ingekuwa ni wewe wala usingerudisha
 
Back
Top Bottom