Mitambo ya umeme ubungo kwanini siyo kwenye chanzo cha gasi??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mitambo ya umeme ubungo kwanini siyo kwenye chanzo cha gasi???

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mkwawa, Jun 20, 2011.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Tukipita ubungo tunaona kila mwenye nia ya kuwekeza kupitia Tanesco na serikali akijiwekea mitambo pale. Hii ilisababishwa na serikali yetu kufanya mikataba ya kitapeli ya kuvuna gasi kutoka kusini na kuisafirisha hadi Dar es salaam kwa ajili ya uzalishaji wa umeme na mambo mengine mengi.

  Nikiwa naongea na baadhi ya wataalamu wa maswala ya gasi haswa ya songo songo walisema kilichofanyika ni utapeli tu kujenga mabomba yale badala ya kufunga ile mitambo huko huko kwenye chanzo cha gasi. Gharama za kuisafirisha ile gasi kwa mabomba, kutengeneza miundo mbinu ile ingepungua sana kwa kuiweka ile mitambo kwenye chanzo. Mabomba yaliyotumika hayaendani na kinachosafirishwa. Walifikia kusema ni sawa na kutumia basi kwendea kazini.

  Kwanini mitambo isingefungwa kwenye chanzo na umeme kuingia kwenye grid ya taifa? moja kwa moja?
   
 2. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2011
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  wataalamu wa mambo ya umeme watasaidia zaidi!ila nijuavyo mm hayo mabomba yaliwekwa si kwa ajili ya umeme tu,na pia gesi inayotumika viwandan inapita kwenye bomba hilo hilo!na pia wangeweka power plant kule songosongo umeme unapotea njian kama energy lost!ni hayo tuu
   
 3. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Arusha umeme taabu tupu leo nilikuwa ofisini ilikuwa hakuna kurudi nyumbani umekatika hakuna hadi kesho asubuhi hata kuchaji simu taabu tupu.
   
 4. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Ni sababu nzuri, lakini huoni kuwa umeme ungekuwa nafuu kama tungezalishia hukohuko? hilo bomba litumike kwa matumizi ya viwanda peke yake au kuzalisha umeme wa dharula. Kiwango kinachopotea njiani naamini ni kidogo sana, kwa kuwa zipo technolojia za kuzuia hilo kama tunavyofanya kwenye umeme kutoka kidatu na mtera
   
 5. n

  ngarauo Member

  #5
  Jun 20, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  shimboni aka symbion
   
 6. lynxeffect22

  lynxeffect22 JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 625
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kama alivyosema parachichi hapo juu .... mi si mtaalam sana wa usafirishaji wa gas ila nafikiri kama inapotea ni kiasi kidogo sana kwa usafirishaji wa songosongo mpaka dar es salaam

  ila kwa upande wa umeme kama ungezalishwa huko songo songo ... usafirishaji kwenye hizo transmission lines mpaka ufike dar es salaam kama asilimia 33% au zaidi huwa inapotea tena hapo umejitahidi kusafirsiha kwenye high voltage za 220kV au zaidi, kwenye voltage levels ndogo ndio asilimia kubwa zaidi hupotea!

  nachojiuliza ni kwa nini sisi tunawekeza kwenye uzalishaji mdogo sana wa 100MW au chini ya hapo kama niliona somanga wana gas power station ambayo inazalisha 6MW, what a waste of investment and land! .... tukiwa tunawekeza tujitahidi kufanya kitu kikubwa kitakachonufaisha wengi! ... ni kama dar es salaam tunavyosikia kelele za kila mtu anapokuwa na standby generator yake umeme ukikatika badala ya kuwachangisha hao watu kuwe na standby generator kubwa at the power substation

  ni hayo tu
   
 7. Zagazaga

  Zagazaga JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 519
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  mi nna hasira sana na jk.yaani huu mgao unafanya nimchukie mbaya.huku kwetu mgao ni kila siku.si walisema mgao umeisha?yaAaani wananipa hasira kweli.dowans imewashwa lkn hamna tofauti.
  i
   
Loading...