Mitambo ya Songas yafikia kikomo kuzalisha gesi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,009
Mitambo ya Songas yafikia kikomo kuzalisha gesi


Thursday, 28 July 2011 20:59

Said Powa, aliyekuwa Kilwa
Mwananchi

KAMPUNI inayochimbaji, kusafirisha na kuzalisha umeme wa gesi ya Songas, imesema haina uwezo wa kuongeza uzalishaji wa gesi kwa sababu uwezo wa mitambo yake, umefikia kikomo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Kisiwa cha Songosongo, wilayani Kilwa juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Chris Ford, alisema uwezo wa mitambo iliyopo ni kuzalisha gesi, umefikia kiwango cha mwisho licha ya kwamba bado visima vilivyoko vina gesi ya kutosha.

"Mahitaji ya gesi ni makubwa kutokana na kuongezeka kwa matumizi yake na kwa sababu hiyo hata hiyo mitambo ya megawati 100 ambayo serikali imeinunua haitapata gesi na hakuna njia ya haraka kuweza kutatua tatizo hili," alisema Mkurugenzi huyo.

Ford alisema kwa msingi huo, serikali inapaswa kutafuta njia mbadala ya kuzalisha umeme na si kwa kutegemea gesi.Mkurugenzi huyo alisema mpango uliopo kwa sasa ni kujenga kituo kingine cha kusafisha gesi kitakachogharimu zaidi ya Dola 170 millioni za Marekani na kwamba kazi hiyo itachukuwa zaidi ya miezi 18 kukamilika.

Ford pia alisema matumizi ya gesi kwa kampuni binafsi katika Jiji la Dar es Salaam, yameongezeka hadi kufikia asilimia 35."Kutokana na matatizo yaliopo, nadhani wakati sasa umefika kwa serikali kuruhusu kampuni binafsi kuzalisha umeme (Mhhhhh!) , ili kukabiliana na upungufu uliopo katika nashati hiyo," alisema Ford.

Wakati huohuo Kaimu Meneja Mkuu wa Pan African, William Chiume, amekanusha taarifa kwamba visima vya gesi na mabomba ya kusafirishia, yamejaa kutu na hivyo kushindwa kuzalisha.Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) imesema imeleta mtambo wa kufulia umeme utakaotumia gesi na kwamba mtambo huo una uwezo wa kuzalisha megawati 100.

Chiume amesema matatizo yaliyokuwapo katika kisima kimoja kati ya visima sita vinavyozalisha gesi na kwamba hadi sasa bado kimefungwa kikisubiri kufanyiwa ukarabati maalum.




 
Haya ni matusi makubwa kwa wananchi tunayotukanwa na wataalamu wetu pamoja na viongozi wetu wakuu.. YAANI HAWAKUFANYA UTAFITI WA KUTOSHA KABLA YA KUAMUA KUNUNUA MITAMBO.. Kodi zetu zinaliwa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Haya ni matusi makubwa kwa wananchi tunayotukanwa na wataalamu wetu pamoja na viongozi wetu wakuu.. YAANI HAWAKUFANYA UTAFITI WA KUTOSHA KABLA YA KUAMUA KUNUNUA MITAMBO.. Kodi zetu zinaliwa

Mikataba imeshasainiwa na mitambo kununuliwa kumbe hakuna gas ya kutosha kutokana na uwezo mdogo wa uzalishaji wa gas hiyo!!!! Kwa kifupi hawa wanaojiita Viongozi walikurupuka bila kufanya tathmini ya kutosha matokeo yake ndio hayo....Kama huu si utaahira sijui ni kitu gani!!!
 
huu ni ufisadi na vission zisizo na uzalendo maana haingii akilini kama unafanya planing ya muda mrefu leo hii unasema inabidi ununue mtambo tena mwingine ni yaleyale maana ufisadi ndio unaowafanya wajanja wajanja kuishi mji lakini yote yana mwisho.
 
huu ni ufisadi na vission zisizo na uzalendo maana haingii akilini kama unafanya planing ya muda mrefu leo hii unasema inabidi ununue mtambo tena mwingine ni yaleyale maana ufisadi ndio unaowafanya wajanja wajanja kuishi mji lakini yote yana mwisho. 
 
Sasa wakati wanaenda kununua mitambo hiyo hawakuwasiliana na Songas na kuangalia all the possibilities and uncertainties. Hivi hawa jamaa wanafikiri kwa kina kweli?!
 
Kwani uzalishaji wa gesi pia inategemea maji kwa sababu nasikia kila kuwa kina cha maji kimepungua!
 
Tumelaaniwa, tumelogwa, tunaumwa saratani ya 10%,

Dalili zake ni
1. Kutofikiria vizuri ( kwa makusudi)
2. Kuweka mipango ya muda mfupi
3. Kutofikiria maslahi ya wananchi
4. Kujilimbikizia mali at the expense of the poor people
5. Kutoonana au kujua kuwa hayo 1-4 ni makosa
6.
 
Mikataba imeshasainiwa na mitambo kununuliwa kumbe hakuna gas ya kutosha kutokana na uwezo mdogo wa uzalishaji wa gas hiyo!!!! Kwa kifupi hawa wanaojiita Viongozi walikurupuka bila kufanya tathmini ya kutosha matokeo yake ndio hayo....Kama huu si utaahira sijui ni kitu gani!!!

Hili lilitamkwa na January Makamba (aliyekaribishwanCDM na Mbowe) wiki iliyopita baada ya "wizara ya mashati maini" kukabwa kooni kuwa hata serikali ikinunua mitambo bado inatakiwa itatue tatizo la mafuta ya kuendesha hiyo mitambo kwa sababu gesi haitoshi
 
mikataba imeshasainiwa na mitambo kununuliwa kumbe hakuna gas ya kutosha kutokana na uwezo mdogo wa uzalishaji wa gas hiyo!!!! Kwa kifupi hawa wanaojiita viongozi walikurupuka bila kufanya tathmini ya kutosha matokeo yake ndio hayo....kama huu si utaahira sijui ni kitu gani!!!
ukifikiria sana haya mambo unaweza kufa kwa presha
 

hili lilitamkwa na january makamba (aliyekaribishwancdm na mbowe) wiki iliyopita baada ya "wizara ya mashati maini" kukabwa kooni kuwa hata serikali ikinunua mitambo bado inatakiwa itatue tatizo la mafuta ya kuendesha hiyo mitambo kwa sababu gesi haitoshi
unaweza kukuta washainunua hiyo mitambo tayari
 
na watu bado wako maofisini bila wasi wasi wowote ule


the question is how would Museveni or Kagame deal with this issue?
 
.....Another 18 months or even more of mgao wa umeme or total darkness
Kila siku mtakuwa mnasikia Tanesco wameagiza mitambo wataitwa waandishi wa habari kwenda kupiga picha baada ya hapo utasikia maneno yafuatayo "Jitihada, Mipango Endelevu, Mipango ya Muda Mfupi, Mipango ya muda mrefu" baada ya hapo mtaambiwa itachukua miezi 18 mitambo kukamilika then mgao wa umeme utakuwa unaendelea kutupiga kama kawaida huku Kikwete akisema "Serikali sio Mungu haina uwezo wa kuifanya mvua inyeshe mabwawa ya mtera yajae".
 
mbona hili lilikua linajulikana. kunavitu viwili kwanza uwdzo wa kuchimba gas na pili uwezo wa kusafirisha gas. vyote inabidi viongezwe
 
Tumelaaniwa, tumelogwa, tunaumwa saratani ya 10%,

Dalili zake ni
1. Kutofikiria vizuri ( kwa makusudi)
2. Kuweka mipango ya muda mfupi
3. Kutofikiria maslahi ya wananchi
4. Kujilimbikizia mali at the expense of the poor people
5. Kutoonana au kujua kuwa hayo 1-4 ni makosa
6.
6. Hile sindano ya ndui ndio imepumbaza jamii ya kitanzania nahisi ilikuwa ni kinga thidi ya radhi la kufikiri ,lakini kichekesho zaidi ni katika bara hili la Africa, sie ndio
‪kenny rogers coward of the county‬‏ - YouTube
 
waache longolongo tunasubiri tar 31 . 08 . 2011 tupate umeme wa kutosha na tar 31 . 12 . 2011 tuwe na historia ya mgao wa umeme pasi WM aliyasema haya kwa msisitizo hizi habari zingine hazituhusu Serikali inajua kila kitu
 
Back
Top Bottom