Mitambo ya Richmond/Dowans itaifishwe - Mongela

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
824
mama mongela anaongea sasa bungeni, na amependekeza ile mitambo ya richmond/dowans itaifishwe ili itusaidie wakati wa dharura.

mimi namuunga mkono, kuwa wasiruhusiwe kuichuka hiyo mitambo, ikae hapo kama guarantee wakati tunawadai mapesa waliotuchukulia kwa mkataba feki
 
Hili la muhimu maana wametuibia na wanaendelea kutuibia hivyo basi ni muhimu kama wakazuia hiyo mitambo itusaidide ila sitashangaa nikisikia siku moja ikitaka kutumika kwamba kuna kifaa hakipo ama kuna hitilafu ndogo maana hii nchi ina makubwa hayaishi kila siku yanaongezeka.
 
Halafu Ni Hao Hao Watakuja Kununua Kwa Majina Mengine -- Mongela Ndio Anasema Sasa Hivi Lakini Mpango Huo Upo Toka Mwaka Juzi Kwamba Hizo Kampuni Zitataifishwa Watazinunua Wao Wenyewe Kisha Waje Kuuza Bidhaa Zao Kwa Watanzania
 
mmh sijui kama wataweza kwani wenye mitambo wamo humo humo Bungeni.
Ila wakikamatwa na kuwekwa Lupango itawezekana kuitaifisha mitambo yote lakini wakiendelea kupeta tu uraiani hatuwezi.
 
Hela Tulikuwa Tunawalipa Wenyewe. Hadi Sasa Tunaendelea Kuwalipa Dola 152 Milioni Kila Siku. Sasa Sio Ujinga Kusema Wanatuibia?

Macinkus
 
Halafu Ni Hao Hao Watakuja Kununua Kwa Majina Mengine -- Mongela Ndio Anasema Sasa Hivi Lakini Mpango Huo Upo Toka Mwaka Juzi Kwamba Hizo Kampuni Zitataifishwa Watazinunua Wao Wenyewe Kisha Waje Kuuza Bidhaa Zao Kwa Watanzania
Ndiyo tatizo la wanasiasia wa Bongo.Yaani huwa wanongea mambo kama wanatoka Ahera,anaweza akawa na wazo zuri ila katumwa na Flani.

Mie huwa nashangaa kipindi cha Bunge Matajiri wote wa dar e s salaam ahuwa wanakimbilia Dodoma,kuwadanganya wabunge wetu
 
Kutaifisha ni dhuluma, huwezi kupigania haki kwa kudhulumu; Nyerere alijaribu matokeo yake kila mtu anayajua. Sheria lazima itumike: mafisadi wachukue uchafu wao waondoke!!
 
nimerekebisha hvu

kwa kuwa tenesco illingia mkataba na kampuni ambayo haikuwepo kisheria, na kwa kuwa kampuni hiyo hewa imeendelea kulipwa mabilioni, na kwa kuwa sasa serikali imegundua hilo, na ikasisitsha mkataba huo. kwa kuwa kuna wanaotaka hatua kali zichukuliwe ikiwa ni pamoja na kuwashinikiza kampuni hiyo hewa irudishe hyo mabilioni

sasa, ni vema mitambo iliyoletwa na dowans mmiliki wakampuni hiyo hewa ikazuiwa na kutaifishwa ILI RICHMOND ATOKEZE TUWEZE KUMDAI
 
Katika kipindi cha kipima joto cha ITV juzi ijimaa usiku kuna bwana moja kati ya wageni waalika ambale alitokea CTI alishauri serikali ichukue mitambo ya dowans kwa nguvu iweze kuitumia katika kipindi hiki cha tatizo kubwa langao wa umeme.

Usahauri huu mimi nimeuona kama kuibaka dowans. Kinanacho mimi niwe na mashaka ni kuwa kwenye kesi ya kubambikiswa na dowans tanesco na serikali walishindwa tunalipa billion 94, hii ya kuibaka dowans si ndio nchi itauizwa kabisa ili tulipe fidia?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom