Mitambo ya dowans aigusiki-waziri ngeleja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mitambo ya dowans aigusiki-waziri ngeleja

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Feb 18, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,442
  Likes Received: 5,695
  Trophy Points: 280
  SERIKALI imesema suala la kutaifisha mitambo ya umeme ya Dowans kwa ajili ya 
kukabili hali ya mgawo wa umeme, si sera ya Serikali ya CCM, kwa kuwa hutekeleza kila jambo kwa mujibu wa sheria.
 


  Aidha, imewahadharisha viongozi na wanasiasa kuacha kutumia tatizo lililopo la 
umeme kutoa matamko ya kujitafutia sifa na badala yake wazingatie 
zaidi mustakabali wa Taifa.
 


  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, 
alipozungumza na HABARILEO katika mahojiano maalumu kuhusu hali ya umeme nchini.


  
“Kuhusu kutaifisha mitambo ya Dowans, nasema wazi na nataka ieleweke, hii si 
sera ya Serikali ya CCM, tukiendekeza mambo ya kutaifisha, leo tutataifisha 
Dowans kesho tutakwenda hadi kwenye mali za wananchi,” alisema Ngeleja.
 


  Alisema Tanzania inaongozwa kwa misingi ya utawala bora ambayo inazingatia 
utawala wa sheria.

  “Katika mazingira haya, ili utaifishe mali ya mtu lazima 
upitie mchakato wa kisheria tena kwa kuzingatia sheria za nchi zilizopo.”
 


  Alisema kwa mgawo wa umeme sasa, kumekuwa na kauli mbalimbali za 
wanasiasa ambazo hazina tija na nyingi zimejaa kujipatia umaarufu, hali ambayo 
haisaidii kutatua tatizo halisi lililopo.


  “Ombi langu, tujadili suala hili la upungufu wa umeme na juhudi za utatuzi wake 
kwa kuzingatia misingi tuliyojiwekea, naomba wananchi wapuuze kauli zinazotolewa 
na wanasiasa zenye majibu ya mkato kwa mambo mazito,” alisema.

  
Aliwataka wanasiasa kuacha mara moja kutumia nafasi hiyo ya upungufu wa umeme 
kupotosha Watanzania na ulimwengu kwa kutaka sifa au umaarufu kisiasa. 
 


  “Nasisitiza haya nikitambua kwamba katika mazingira yaliyopo ya mgawo wa umeme 
na hasira walizonazo wananchi kutokana na tatizo hilo, ni rahisi kwao kupotoshwa 
na wanasiasa wanaotaka sifa bila kuzingatia mustakabali wa nchi yetu,” alisema 
Ngeleja.


  
Pia Ngeleja aliomba wananchi waunganishe nguvu kupitia viongozi wao wa dini, ili angalau mvua zinyeshe na mabwawa yanayozalisha umeme kwa kutumia maji yajae.
 


  Akizungumzia suala la kauli yake aliyoitoa bungeni kuhusu umeme, alikanusha 
taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa hali ya umeme 
itatengemaa mwaka 2033 na kuongeza kuwa huo ni uzushi na kwamba upo mpango 
mkakati wa miradi ya umeme unaoanzia mwaka 2009 hadi 2033.
 


  Alisema mpango mkakati huo unajumuisha miradi mingi ya muda mrefu, kati na mfupi, ambayo mingine tayari imekamilika na kutoa umeme akitolea mfano mradi wa umeme wa Ubungo wa megawati 100 na wa Tegeta wa megawati 45.
 


  Alisema inasikitisha kuwa wapo baadhi ya watu wanaodhani kuwa Serikali 
haijafanya lolote kuhusu umeme ambapo alisema kama lisingekuwapo 
tatizo la umiliki katika mgodi wa Kiwira wa megawati 200 kuanzia mwaka 2005 
hadi 2010, Serikali ingekuwa na nyongeza ya umeme wa megawati 645.


  
Ngeleja alitoa kauli hiyo baada ya baadhi ya wabunge kutoa hoja ya kuikodi kwa miezi mitatu au kutaifishwa kwa mitambo ya Dowans ili kumaliza tatizo la umeme akiwamo Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, January Makamba.

  Februari 16 pia baadhi ya wanasheria waandamizi nchini walisema mitambo ya Dowans haiwezi kutaifishwa kwa sababu kampuni hiyo haikabiliwi na kesi ya uhujumu uchumi lakini pia kuingia mkataba mwingine na kampuni hiyo ni mzigo kwa Serikali.
   
 2. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hapo Kwenye Red utawala bora upo wapi hapa Tanzania? Pumbavu huyu Ngeleja
   
 3. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Si sera ya CCM, if u think again kutaifisha na maouvu ya CCM kwa wananchi wake utakua kimsingi anasema sera ya CCM ni UFISADI na hivyo hawataifisha hiyo mitambo bali KUINUA kwa bei nzuri kwa gharama tu. Stupid Ngeleja...

  Anaongelea tija while ni phase ya pili yuko wizara hiyo, madudu ndo yanazidi.... Makali ya umeme ndo yanazidi. Anafurahi kwa madudu yake inflation kupanda, bei kupanda etc? Yaani anasema he has to be a thinking limit to energy issues of this country while he has significantly failed in all his nonsensical endeavors/solutions..... Kiongozi mzuri ni yule anaesikiliza mawazo ya wengi au ya wengine wawe wengi au wachache.... they have to be considered in making decisions.
   
 4. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 621
  Trophy Points: 280
  Tanzania vituko tupu!!
  1.Tunaingia mkataba na DOWANS
  2. Tunavunja mkataba na DOWANS
  3.Tunaingia Gharama za kuilipa fidia DOWANS kwa kuvunja mkataba
  4.Tunataka kuwasha mitambo ya Dowans kwasababu tunaihitaji kwasasa
  5.Nafikiri tunaelekea point No.1
   
 5. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Anaogopa kusema ukweli kuwa mitambo ile iliwekwa rehani na Dowans wakati ilipokopa milioni 100 Barclays.
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkuu, naona umeliona hili!
  Lakini unapokuwa na kiongozi wa aina ya Ngeleja anayesema wananchi kupitia kwa dini zao waombe Mungu Mvua inyeshe, anatuambia yeye na CCm wenzake wamefikia kikomo katika kufikiri, na kutoa suluhisho la matatizo ya umeme kwa miaka takribani 14 sasa!

  This is a big joke, sasa kama tutegemee Mungu, si waondoke tu madarakani, wanalipya ili sisi tusali mvua inyeshe?

  ...On the second thought, hivi hii kamati ya nishati ilivyoanza kazi kwa kutembelea Mtera kujionea jinsi kina cha maji kilivyopungua; Wakishaona halafu inakuwaje? wanafanya dua au?......This is nonsense!!!
   
 7. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkuu, ile mitambo imeshauzwa kwa kampuni moja ya Korea.......Hawa jamaa ni wahuni!
   
 8. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mbona hawajalipa deni la Barclays?
   
Loading...