Mitambo chakavu tatizo la umeme Z’bar

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,736
155,419
SERIKALI imekiri kuwa tatizo la umeme visiwani Zanzibar linatokana na uchakavu wa mitambo ambayo ni ya muda mrefu na inahitaji marekebisho na gharama kubwa.

Katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda leo asubuhi, Mbunge wa Chambani, Salim Hemd Khamisi (CUF), ameuliza Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania ina mpango gani wa kuisaidia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuhusu giza totoro lililodumu kwa muda mrefu.

Mbunge huyo alisema kero ya giza visiwani humo ilianza tangu Desemba 10, mwaka jana, na hadi sasa bado inaendelea na kusababisha shughuli za maendeleo kukwama.

“Tumeambiwa kuwa tataizo hilo linaweza kumalizika ifikapo Februari 10, mwaka huu, je Serikali ya Jamhuri ina mpango wa kuisadia SMZ kwani undugu si kufaana bali ni kusaidiana?” amehoji mbunge huyo.

Akijibu swali hilo, Waziri Pinda amesema ni kweli kabisa tatizo hilo ni kubwa na linahitaji nguvu zaidi ya kuisaidia SMZ.

Waziri Pinda amesema Serikali ya Tanzania imefanya jitihada za kuhakikisha kuwa tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi. Hata hivyo Waziri Kiongozi amemwandikia barua ya kuomba msaada.

“Waziri Kiongozi Zanzibar ameniandikia barua kuhusiana na namna ya kuweza kusaidia tatizo hilo kwani linahitaji gharama kubwa na mbinu ili kuweza kulitatua,” amesema Pinda.

Amesema katika kuhakikisha kuwa wananchi wa Zanzibar wanaondoka na kero hiyo haraka tayari amemwandikia barua Waziri wa Fedha kuangalia namna ya kuweza kulitatua tatizo hilo.

Amesema ni kweli nyaya za umeme zimechakaa sana na zinahitaji marekebisho kutokana na kuwa ni za muda mrefu.
 
Back
Top Bottom