Mitaala na mfumo mpya wa elimu bila MASLAHI mapya kwa Walimu ni kufeli kabla ya utekelezwaji wa mfumo

Mwl Athumani Ramadhani

JF-Expert Member
Sep 10, 2022
1,282
2,506
Prof. Mkenda

Wewe ni Mwalimu kwa ueledi,changamoto za walimu huku field huzijui!?

Kama changamoto za watekelezaji wa mtaala mpya na mfumo wake zitakuwa zile zile na matokeo yaweza yakawa yale yale!

Mfumo mpya wa elimu ungeweka wazi Kuwa ili mtaala huu ufanikiwe utekelezwaji wake maslahi mapya ya walimu kama haya yatekelezwe:-

1. POSHO YA UTEKELEZAJI MTAALA.
Walimu wapewe posho maalumu kuendana na Kasi ya utekelezwaji wa mtaala husika ili malengo ya mtaala huo yafikiwe haraka na kuleta matokeo chanya.

2. MAZINGIRA WEZESHI YA KUFUNDISHIA MITAALA MIPYA.

Majengo ya vyumba vya Madarasa pekee havitoshi Kuwa wezeshi kwa walimu,makazi na umbali kutoka wanapoishi Hadi kituo cha kazi ni la kuangaliwa upya,walimu wengi wanaishi mbali na vituo vya kazi kwa kukosa nyumba za kuishi na wengine wanaishi kwa kubanana nyumba moja familia mbili hadi tatu HII inashusha morali ya utekelezwaji wa mtaala uliopo,ITASABABISHA kufeli kwa utekelezwaji wa mtaala mpya.

3. MIKOPO YA ASSET (KAMA NYUMBA) KWA WALIMU.

Shirika la nyumba la Taifa lianze rasmi kukopesha watumishi wa umma (walimu) nyumba za kuishi KWA watumishi watakapostaafu. Tena KWA MIKOA watakayo chagua wenyewe na FEDHA kukatwa pole pole Hadi deni linapoisha,ili kuondoa msongo wa mawazo kuhusu maisha baada ya kustaafu. Wadau mbali mbali wawekeze kwenye hilo pamoja na asset nyinginezo ambazo ni mtambuka KWA watumishi KWA nyakati zijazo za maisha baada ya utumishi!!!!

4. KUPANDA CHEO (MADARAJA) IWE SEHEMU YA MTAALA MPYA,KULIKO KUTEGEMEA UTASHI WA ALIESHIKA HATAMU.

Kama tulivoona KWA miaka takriban sita hivi, kwamba upandaji cheo na Madaraja ni utashi wa ALIESHIKA HATAMU, akiamua lolote ndilo litakalofanyika, ni bora mambo haya yakajumuishwa kwenye mitaala na mfumo mpya wa elimu Ili iwe SEHEMU ya utekelezwaji wake vikaendana sambamba KULIKO ilivyo Sasa!

KUTEGEMEA CWT na TUCTA kama mtetezi mkuu wa walimu ni kujipa matumaini hewa,kwani tangu tupate uhuru hakuna cha maana HASA kilichotetewa na vyama hivi zaidi ya kuwanyonya walimu KWA kuzikata FEDHA zao za mishahara. Ni utashi wa aliye shika hatamu pekee ndio limebaki kuwa tumaini pekee la walimu nchini wala SIO juhudi za Chama chochote cha wafanyakazi nchini.

Haya ni Kati ya mengi Sana yaliyopaswa kujumuishwa kwenye mtaala mpya na mfumo wake Ili kuwezesha utekelezwaji wake. Mafunzo PEKEE ya semina elekezi hayawezi kutosheleza matakwa ya utekelezwaji wa mfumo huu mpya wa elimu

Mungu AWABARIKI walimu. KWA uvumilivu na utendaji wao tangu tupate uhuru.

Mungu aibariki wizara ya elimu iendelee kuwa na maono mapya kuhusu mstakabali wa kesho ya elimu itakayolikomboa Taifa letu dhidi ya ujinga, maradhi na umaskini.

Mungu aibariki nchi yangu Tanzania niipendayo.

Mimi Mwl Ramadhani Athumani.
Nikiendelea kulitumikia Taifa langu sasa.
 
Mitaala bora ya elimu hasa kwa kizazi cha SAsa ni ule uliotumika enzi ya ukoloni. Ule ulifundisha skills na sio academy.

Watu wafunzwe stadi za Kazi Ili wazione fursa wazitumie kuzalisha na sio kurundika watu vyuo vikuu waishie kupata academy, sababu awajaandaliwa wakimaliza uishia kutembeza vyeti mitaani miaka na miaka,then ukata tamaa na kurudi kutafuta skills Ili waweze kumudu maisha.

Maisha ya SAsa sio vyeti bali ni ujanja wako wa kumudu kupata taarifa na kuzibadili ziwe pesa. Kuwa na vyuo vikuu vingi katika nchi ni kuongeza idadi ya masikini nchini.
 
Back
Top Bottom