Mita ya umeme kwa ajili ya wapangaji inaingiza Units na kukata umeme pale units zikiisha,pia inakopesha units

XOXOQY

Senior Member
Feb 7, 2011
172
36
iMarkup_20210429_081400.jpg

-Inatumia line (mtandao wowote),line kwa ajili ya kuwasiliana na system,kutuma na kupokea taarifa.

-Mpangaji atanunua umeme kama kawaida na kujaza mita kubwa ya tanesco,akisha jaza..system
zetu zitaditect na zitaijaza mita yake ndogo UNIT zile zile alizo nunua,kwenye mita kubwa,unit za
mita ndogo zikiisha umeme unakatika kwake tu.

-Ukikatika ananunua tena anajaza katika mita ya Tanesco.

-Zina mfumo wa kukopesha UNIT,kama mpangaji atakua na dharura,anaweza kukopa UNIT kwa
kuwasiliana na sisi,atakopeshwa....akija kuweka atakatwa kile kiasi Cha UNIT alicho kopa.

-Mita ni automatic,anajaza umeme mita kubwa tu ya Tanesco,hizi ndogo zinapokea taarifa
automatic.

-Bei ya mita complete ni 180,000/- per PC.

MAELEZO ZAIDI.

-JINSI YA KUNUNUA UMEME

Nunua umeme kawaida Kupitia namba ya mita ya Tanesco,kama unavyonunua siku zote,ukipokea
token Jaza katika mita ya tanesco.

Mfano umenunua UNIT 3,ukiingiza katika mita ya Tanesco,token zikakubali,mita yako ndogo pia
itasoma UNIT 3,zile to ulizo nunua.

Zikiisha hizo UNIT 3 katika mita yako ndogo Basi,umeme utakatika kwako tu,hata Kama mita kubwa
ya Tanesco inaumeme.

-ITAKUWAJE KAMA NI MIMI PEKE YANGU NIMEFUNGA MITA HIYO NA WAPANGAJI WENGINE
WANAENDELEA KUTUMIA MFUMO WA KAWAIDA.

Ukifunga mita hii,peke yako,mfano nyumba in wapangaji watatu,wewe peke yako ukafunga mita hii.

Wale wapangaji wengine Kuna uwezekano wakatumia UNIT zako,hivyo umeme unaweza Isha katika
mita kubwa kabla haujaisha mita yako ndogo.

Ikitokea hivyo,wewe hauhusiki na ununuaji wa umeme,sababu mita yako bado itakua na
umeme,wewe unanunua umeme pale tu mita yako ndogo inapoisha umeme.

Hivyo mita kubwa ikiisha umeme na wakati mita ndogo bado ina umeme,itawalazimu wale ambao
hawajafunga mita ndogo,wanunue umeme,wakiweka umeme mita kubwa,mita yako ndogo itasoma
kiasi kilichobaki baki na utaendelea kutumia Hadi uishe.Ukiisha katika mita ndogo wewe ndo
utanunua,wakwako tu ambao unaona utakutosha.Ukisha nunua unaenda ingiza mita kubwa token
zako.

-SOLUTION YA KUISHA UMEME MITA KUBWA WAKATI MITA NDOGO BADO INAIDADI YA UNITS.

Tatizo la kuisha umeme mita kubwa na mita ndogo bado ikiwa na UNITS zake litaisha pale tu
wapangaji wote watafungiwa mita hizi ndogo.

Kila mpangaji akifungiwa mita yake umeme mita kubwa utakua hauishi,sababu Kila mtu anachukua
kiasi chake Cha UNITS alicho weka katika mita kubwa bila kuzidisha,labda itokee mita zote ndogo
UNIT ziwe Zero,ndo mita kubwa nayo itaenda Zero UNIT.

-JE KIFAA HIKI KINA UHUSIANO NA TANESCO.

Hapana mita hizi,hazifungwi na Tanesco ni mita zinazo uzwa madukani,ni kifaa kinachosaidia
kuratibu na kusimamia matumizi yako binafsi,hakihusianina Tanesco,ni Kama vile unavyonunua
TV,au simu.

Ili uweze fungiwa mita hizi lazima uwe tayari umefungiwa umeme na Tanesco,ambapo mita hizi
zinachukua umeme kutokea katika Main switch (distribution board),kwenda chumbani kwako.

Na Kama ulinunu UNIT 3,na mita kubwa umeme ukaisha kabla umeme was mita ndogo haujaisha

-JE NAWEZA KUHAMA NAYO MITA NDOGO.

Ndiyo Kama mita hii umenunua wewe mpangaji,unaweza kuhamanayo,ila Kama ni mwenyewe
nyumba kanunua,lain yako tu ndiyo itakayo tolewa katika mita,na utakabidhiwa.

-JE NI VIPIMO GANI INATUMIA KATIKA KUKADILIA MATUMIZI YA UMEME.

Vipimo vya mita hizi ndogo ni sawa na vipimo vya mita kubwa za Tanesco kipimo chake ni 1kilowatt
hour=1Unit

Ambapo mita hizi zunahesabia pulse(kile kitaa chekundu kinachowaka katika mita) 1600 kwa Kila
kwh 1.

Kile kitaa chekundu,huwaka kulingana na matumizi yako ukiwa unatumia umeme mwingi kinawaka
haraka haraka,ukiwa unatumia umeme kidogo kinawaka taratibu.

Hivyo Kila kikiwaka mara 1600 ni sawa na umetumia UNIT

1.

-NI JINSI GANI NAWEZA KOPA UMEME.

Utakacho fanya ni kuwasiliana nasi,Sisi tutanunua umeme na tutakutumia Token za kiasi cha unit
unachotaka kukopa.

Token tulizo kutumia utaingiza katika mita ya Tanesco,baada ya kuingiza na ukakubali mita yako
ndogo itasoma hizo Unit ndani ya dakika 3.

Ukija kununua umeme baadae utakatwa kile kiasi Cha token ulichokopa,katika mita yako ndogo.

-GHARAMA ZA MITA HII.

Mita hizi zinauzwa 180,000/-,Bei hii haina mahusiano na matayarisho ya wiring kwa ajili ya kufunga.

Unatakiwa kuweka Oda kupata mita hii(sababu tunaagiza),na malipo ni baada ya kufungiwa.

Tupo Dar mtaa wa Lindi

Tucheki 0744233350
 
Swali:

Mfano, meter ndogo zipo 3,

Nimenunua umeme Tanesco nikaweka Meter kubwa, Je itajuaje umeme ni wangu, uende kwa meter yangu ndogo badala ya kwenda kwa meter ndogo no.2 au no.3? Kuna kitu natakiwa kufanya kwenye meter kubwa?

Je Tanesco wameruhusu hili jambo?
 
Haijatatua changamoto bado.
Kutatua changamoto ni umeme kwangu Usikate hata unit za wapangaji wengine zikiisha endapo bado unit nilizonunua mimi hazijaisha.

Sasa hiyo umeme utaisha ukawaombe wanunue ili wewe upate zile unit zako unazodai.Hii inatatua changamoto ya kulipa zaidi ya matumizi yako tu,haina tofauti na zile za kuhesabu unit
 
Mita zinatumia line (line za simu)hii ndiyo inatoa utambulisho wa mita yako, pia mita zenyewe zina amba zake (kama zilivyo tu za Tanesco, kila mteja anakuwa na data base yake ukinunua umeme mteja wa mita namba 1, umeme utaingizwa kwako wewe wa namba 1, uhakiki wa ukweli wa units na mita gani uingizwe ni kazi ya kimfumo ya mita zenyewe.

Tanesco hawahusiani na mita hizi ila kununua umeme utalazimika kukunua kupitia mita yao kama kawaida.
 
Kuondoa changamoto hiyo nimesha sema wote mnafunga....kama wengine hawana uwezo utakua umepunguza changamoto ya kulipia usicho tumia.
 
Nimenunua umeme Tanesco nikaweka Meter kubwa, Je itajuaje umeme ni wangu, uende kwa meter yangu ndogo badala ya kwenda kwa meter ndogo no.2 au no.3?
Kwa maelezo yaliyotolewa hapo juu, Ni simcard yako itakayokuwa kwenye meter, na kukutambua wewe kama mnunuzi wa umeme.
Ndiyo Kama mita hii umenunua wewe mpangaji,unaweza kuhamanayo,ila Kama ni mwenyewe
nyumba kanunua,lain yako tu ndiyo itakayo tolewa katika mita,na utakabidhiwa.
 
kuondoa changamoto hiyo nimesha sema wote mnafunga....kama wengine hawana uwezo utakua umepunguza changamoto ya kulipia usicho tumia.
Ukishaanza kujumuisha Wengine hiyo ni changamoto tayari mkuu. Sasa Kwanini ninunue hiyo yako kwa ajili ya kuhesabia unit tu kwa gharama ya 180000 badala ya kufunga zile manual za 30,000-50,000?
 
Ukishaanza kujumuisha Wengine hiyo ni changamoto tayari mkuu.Sasa Kwanini ninunue hiyo yako kwa ajili ya kuhesabia unit tu kwa gharama ya 180000 badala ya kufunga zile manual za 30000-50000?
Ni sawa pia itategemeana na unataka kutatua tatizo katika njia ipi zote solution mkuu.
 
kuondoa changamoto hiyo nimesha sema wote mnafunga....kama wengine hawana uwezo utakua umepunguza changamoto ya kulipia usicho tumia.
Bado soln.ya tatizo hili hamjalipata!!inshu mizozo mingi kwenye nyumba za watumiaji wengi wa umeme, ni kujaza umeme kwenye mita kubwa, hata kama wote mna hizo mita, kwani sehemu nyingi kwa sasa wanatumia hizi mita ndogo ambayo kila mtu anajifungia, kwake, kuweza kujua matumizi yake, sasa kuna wengine bado ni shida, umeme unaisha kwenye mita kubwa, mkienda kwenye mita yake, mnakuta umeme wake umekwisha na ameshatumia na wa wengine, jibu analiwapa kwa sasa sina pesa , labda kesho, haya, hapo mkubali kulala giza au mtu ajitolee kununua tu!!hapa hadi tanesco watakapoamua wao kama wao watengeneza hizo mita ndogo, ina maana mtu akinunua umeme uingie moja kwa moja kwenye hiyo mita yake ndogo, tu, ukiisha inazimika tu.Waswahili ni tabu sana, mimi kuna sehemu hadi nilionekana adui kwani tulikuwa tunatumia mita hizo, kwenye fremu za biashara, daaa, wakiniona tu nimebeba daftari tayari wanajua kimewaka, watu kununua umeme wao ni tabu mtu anatumia hadi units 30, za mwenzake?!!ukimkatia anaenda kwa mjumbe, hahaaa!!
 
Mita hizi huwezi tumia umeme wa wengine,UNIT zako zikiisha unakatika kwako tu.
 
Mita hizi huwezi tumia umeme wa wengine,UNIT zako zikiisha unakatika kwako tu.
Pia kuna sababu inayowafanya Tanesco wasifunge mita nyingi zinazo jitegemea sehemu moja...si sababu za kiufundi zaidi ni sababu za kimapato,biashara ya uuzaji umeme sio kama biashara ya watu wa maji mfano dawasco.

Umeme unakitu kinaitwa Tariff,hicho ndo kinaleta changamoto ya kufunga mita nyingi eneo moja.
 
Mita hizi huwezi tumia umeme wa wengine,UNIT zako zikiisha unakatika kwako tu.
tatizo ni pale bado nina umeme wangu kwenye kimita hicho, lakini kwenye mita kubwa hakuna, watu wametumia umeme wote na wanasema hawana pesa kwa muda huo!!huoni bado shida iko pale pale?!!kwani itabidi uingie mfukoni tena ununue lasivyo utalala giza na bado una units zako
 
Mita zinatumia line (line za simu)hii ndiyo inatoa utambulisho wa mita yako, pia mita zenyewe zina amba zake (kama zilivyo tu za Tanesco, kila mteja anakuwa na data base yake ukinunua umeme mteja wa mita namba 1, umeme utaingizwa kwako wewe wa namba 1, uhakiki wa ukweli wa units na mita gani uingizwe ni kazi ya kimfumo ya mita zenyewe.

Tanesco hawahusiani na mita hizi ila kununua umeme utalazimika kukunua kupitia mita yao kama kawaida.
Kwa maana hiyo umeme ni lazima ninunue kwa kutumia simu yangu ndio uingie kwangu peke yake?Nachotaka kujua ni hiyo processs ya kununua umeme,unanunuaje kwa kutumia hiyo line yangu,ili nitakapoweka kwenye mita kubwa iweze kujua kuwa ni mimi ndio nilieweka umeme na sio mpangaji mwingine...?
 
Back
Top Bottom