Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 746
- 3,058
Walimu wawili wa shule za msingi Mwagimagi na Kifune wilayani Misungwi mkoani Mwanza, wamefikishwa mahakama ya wilaya hiyo kwa tuhuma za kubaka na kuwapa ujauzito wanafunzi wawili.
Walimu hao ni Telepholy Revocatus (32) wa Shule ya Msingi Mwagimagi na Peter Ferdinand (35) wa Shule ya Msingi Kifune.
Akisoma hati ya mashitaka mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi, Erick Marley, mwendesha mashitaka wa polisi Ramsoney Salehe kwa kesi namba 117/ 2018 amedai mshtakiwa mwalimu Revocatus alitenda kosa hilo kati ya Januari na Februari, 2018.
Amedai mshtakiwa alimbaka na kumtia mimba mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwenye umri wa miaka 17 katika Sekondari ya Ilujamate wilayani hapo kinyume na kifungu cha 130(1) 2(e) na 131sura ya adhabu 16 iliyorekebishwa mwaka 2002.
Salehe alimsomea tena kesi ya jinai namba 107 /2018 Peter Ferdinand kwa kosa kama hilo la kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la saba wa Shule ya Msingi Kifune.
Watuhumiwa wote wako nje kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ambayo yalikuwa kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya shilingi milini moja kila mmoja.
Hakimu Marley aliziahirisha kesi hizo hadi Septemba 26,2018
Chanzo: Mwananchi