MISUKULE inayodaiwa kutolewa na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwaj | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MISUKULE inayodaiwa kutolewa na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwaj

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Apr 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280

  MISUKULE inayodaiwa kutolewa na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima imemuumbua baada ya kuandikiwa barua na taasisi moja inayotetea watu hasa wanyonge ya Liberty International Foundation (LIF) ikimtaka kiongozi huyo wa kiroho kuomba radhi kwa Bw. Faustin George Kahabi kwa madai ya kumdhalilisha mtoto wake, Happiness Kahabi ambaye anadaiwa kutangazwa kuwa ni mmoja wa misukule waliookolewa katika kanisa hilo.

  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa barua hiyo inayojulikana kisheria kama Demand note ya Aprili 7, mwaka huu, iliyoandikwa na taasisi hiyo inasema, Bw. Kahabi anadai kuwa Mchungaji Gwajima aliutangazia umma kuwa mtoto wake Happiness ambaye ni mke wa Isaya Ndambo alichukuliwa Msukule na yeye (baba) na kupelekwa chini ya Ziwa Victoria baada ya kufariki dunia mwaka 2008 katika Hospitali ya Bugando na kwamba kutokana na maombi yake (Gwajima) alifanikiwa kumtoa kuzimu katika kundi la Misukule.

  Waraka huo (nakala tunayo) unazidi kueleza kuwa tukio hilo la kutolewa kama Msukule Happiness, lilirekodiwa na kuwekwa katika kanda (DVD) na kusambazwa sehemu mbalimbali za dunia hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa Bw. Kahabi.

  “Umesababisha Bw. Kahabi agombane na mkewe Edda Faustine Kahabi na ndugu na kumsababishia hatari katika jamii na pia kupandikiza unyanyapaa,” imesema sehemu ya waraka huo.
  Aidha, barua hiyo imesema upo ushahidi kutoka kwa jamaa wa Bw. Kahabi, marafiki na majirani kuwa katika familia hiyo (ya Kahabi) hapajawahi kutokea msiba wa Happiness na wala hawajawahi kuwa na Msukule na kwamba aliyetajwa kuwa Msukule hajawahi kutoweka nyumbani hata kwa wiki moja.

  [​IMG]
  Mchungaji Mtikila
  Barua hiyo imemtahadharisha Mchungaji Gwajima kuwa kuzusha habari za Msukule ni kosa la jinai kama litafikishwa katika vyombo vya sheria, hivyo taasisi ya LIF imemtaka amuombe radhi Bw. Kahabi ndani ya siku saba kuanzia siku iliyoandikwa barua hiyo Aprili 7, mwaka huu.

  Aidha, pamoja na radhi hiyo, Mchungaji Gwajima ametakiwa kuambatanisha shilingi bilioni moja kama fidia ya kuikashifu familia hiyo na pia kuhakikisha mke wa Bw. Kahabi anarudi kwa mumewe akiwa na watoto wao George pamoja na Amos.
  Taasisi hiyo imemuonya Mchungaji Gwajima kuwa bila kufanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria bila kupewa taarifa ya ziada.

  Uchunguzi wetu umegundua kuwa aliyepewa kusimamia shauri hilo ni Mchungaji Christopher Mtikila ambaye anaaminika kwa kufuatilia kesi mahakamani. Chanzo chetu cha habari kilisema kigezo kilichotumika kumchagua ni kutokana na uhodari wake wa kushughulikia kesi ngumu, wakatoa mfano wa kesi ya mgombea binafsi ambayo imelazimu Mahakama ya Rufaa nchini kuisikiliza ikiwa na majaji saba.
  [​IMG]
  Demand Note aliyopelekewa Mchungaji Gwajima
  Aidha, Mtikila anatajwa kuwa amekuwa na historia nzuri ya kushinda kesi na wakatolea mfano wa kesi ya vyama vya siasa kuomba kibali cha kufanya mikutano ya hadhara ambapo kiongozi huyo wa Chama cha Democratic Party aliishitaki serikali na kuishinda.
  Gazeti hili liliwasiliana na Mchungaji Mtikila na kumuuliza kama kweli amepewa jukumu la kuisimamia kesi ya Bw. Kahabi akasema kwa sasa hawezi kusema chochote kwa kuwa Mchungaji Gwajima kapewa masharti ya kutimiza na atakuwa tayari kusema iwapo aliyoandikiwa katika barua atashindwa kutekeleza.

  “Mimi kwa sasa siwezi kunena chochote kwa sababu kuna barua kapelekewa, sasa kama atashindwa kutekeleza alichoambiwa na siku saba alizopewa zikaisha, nitazungumza,” alisema Mtikila. Siku saba hizo zinaisha leo.
  Mchungaji Gwajima hakuweza kupatikana licha ya waandishi wetu kufika katika kanisa lake Ubungo.

  Hivi karibuni Mchungaji Gwajima amejizolea umaarufu kwa madai ya kutoa Misukule. Hata hivyo, watu wana hamu kubwa kuona kama atafanikiwa kumrejesha aliyekuwa Mbunge wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amina Chifupa ambaye aliwahi kudai kuwa ni msukule na wiki iliyopita gazeti hili lilibeba habari inayodai kuwa aliwahi kutoa misukule 70.
   

  Attached Files:

 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  tunaweza kuona idadi ya makoso ya udhalilishaji kwa kutumia maneno yanapungua iwapo watu wawili watatu watafunguliwa kesi ya madai

  way to go
   
 3. H

  HUBERT MLIGO Member

  #3
  Apr 14, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kama udaku vile...
   
 4. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  No comment.
   
 5. T

  Tall JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.KWENYE MSAFARA WA MAMBA KENGE HAKOSI. KUNA UWEZEKANO WA KUMCHOMEKEA MLALAMIKIWA?

  FIKIRI SANA:
  2. Kwa mfano mimi siku zote nipo nyumbani,nalala hapo,anakuja mtu anamweleza mke wangu kuwa jana,sijalala hapo nyumbani na mke WANGU ghafla tunagombana weee mimi na wife mwisho anaondoka kurudi kwao.UTASEMAJE HAPO?nililala home sikulala?kama nililala HOME ugomvi wanini na wife? au mke wangu ni chizi? AKILI YANGU INANIAMBIA KUWA? MTOTO ALIPOTEA NA NDIO MAANA WAKAGOMBANA MUME NA MKE NA MKE ANAAMINI MMEWE SI MTU SAFI. OTHERWISE WAGOMBANIE NINI? HAYO NDIO MAWAZO YANGU.
   
 6. k

  kijanaa New Member

  #6
  Apr 14, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii habari haija kamilika kwani ni ngetegemea alie rudishwa msukule nae ahojiwe yeye anesemaje kwa jinsi ninavyo faham mchungaji hawezi kumuita mtu msukule kama yeye sio hapo kuna tatizo
   
 7. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ...? duh...
   
 8. m

  make Member

  #8
  Apr 14, 2010
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Ukweli juu ya jambo hili analo aliyechukuliwa msukule, maana maamini ndiye aliyetoa habari nzima, alikuwa wapi na alichukuliwa na nani. Naunga mkono mchangiaji aliyepita kwamba mchungaji haiti mtu tuu aseme ila mtu anakuja halafu anasema mwenyewe.
   
 9. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #9
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hawa wachungaji nao wamezidi utapeli, hizi dini zingine zitawapeleka pabaya. Kuidharilisha familia ya mtu mpaka kuwatenganisha mtu na mkewe ni kosa kubwa sana.
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Binafsi sina comment hadi kesi itakapoamuliwa na mahakama na ukweli kufahamika.
   
 11. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  huu ndo utakuwa mwisho wa mtikila, kwasababu amechezea sana siasa, sasa akijaribu kuanza kuchezea na makanisa, ataishia pabaya sana, aibu yake itaonekana na kila mtu. ni ajabu sana kwamba, baadhii yetu sisi tumeshuhudia kabisa kwa macho yetu misukule mingi, si pale kwa gwajima tu, na sehemu zingine, hili jambo lipo, kuna watu wanachukua na kuchukuliwa misukule, MUNGU ANAO UWEZO WA KURUDISHA MTU ALIYECHUKULIWA MSUKULE, kwasababu anakuwa hajafa bali amefanyiwa manjonjo ya kichawi tu. robo ya watz ni wachawi wanaojua na kuamini kuwa jambo hili lipo, si geni, toka tumezaliwa tumekuwa tukilijua, sasa mtu anayetaka kuja kuleta upinzani na kujidai kuwa jambo la misukule duniani halipo, ni mnafiki, au haelewe na anahitaji kueleweshwa. HAKIKA, NAMTAKIA MTIKILA ANGUKO JEMA, kwasababu, gusa kitu chochote, ila ukijaribu kumgusa mtu wa Mungu, unagusa mboni ya jicho la Mungu mwenyewe, na utaona reaction yake toka kwake aliye juu.

  kwa kifupi, hili si tukio la kwanza kwa gwajima kufuatwa namna hiyo, wengi wamekuwa wakimuwinda sana, kwasababu biashara yao kuu ni ya kutumia misukule. kuna watu wanamiliki mamia na maelfu ya misukule, mingine inatengeneza lambalamba kwenye viwanda vya wahindi mjinii hapa, mingine inalima na kutunza mashamba ya watu kibaha na bagamoyo na tz nzima, kwa wale ambao walishawahi kuwa wachawi kipindi cha nyuma wanalielewa hili, kwenu ninyi ambao hamjawahi kuwa wachawi msiongee lolote kwasababu hamjui lolote. WACHA Mungu afanye kazi yake, kuna watu wanateseka mashimoni, tz inamilikiwa na watu wanaomiliki wenzao...hebu n yamazeni kwanza. Mungu ataonekana.
   
 12. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  wewe ndo usiongee kabisaaa, kwasababu nyie ndo mnaongoza kununua,kutunza na kuchukua misukule. nenda kamwulize shehe wako, atakwambia. siku zenu zimekaribia kwisha, mtaaibika hadi mchoke.
   
 13. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #13
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Anaye amini mambo ya uchawi na misukule naye mchawi kama si msukule!
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Apr 15, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  No comment mmh!
   
 15. S

  Sinag Man Member

  #15
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi sasa umefika wakati tuwe tunatumia fikra mungu alizotupa. Tuwe tunajenga hoja kwa hawa viongozi wetu wa dini wasiwe wanatupeleka tu. tuache akili kushikiwa. Kwa wenzetu waislamu wana uhuru wa kuhoji. kwanini kwetu ukihoji jambo ambalo lina utata unajengewa mazingira ya kutengwa, kwa kuambiwa n shetani amekuingia,hapa ndiyo hawa viongozi wetu wa dini yetu wanapata kutushika akili zetu na kutudanganya mambo mengi. Tuamkeni na sisi, mbona wenzetu wanahoji pale peye utata. "Bwana asifwe".
   
 16. father-xmas

  father-xmas JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 530
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  tehetehe mi sisemi kitu maana hukawii kuitwa mpinga kristo.
   
 17. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #17
  Apr 15, 2010
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 670
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 80
  Heri mimi sijasema!! Shiii Shii!!!!
   
 18. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #18
  Apr 15, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  always base on point, kwa sheria ipi hapo mpaka liwe kosa kubwa, naona unawatetea wanao chukua watu misukule siyo?
   
 19. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #19
  Apr 15, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  bwana yupi, bwana shamba au? hebu nyoosha lugha kwanza,
   
 20. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #20
  Apr 15, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  as well as i
   
Loading...