Misukosuko na changamoto niliyokutana nazo kipindi nimepanga Mbagala na Mwembechai

Dawa nikumiliki siraha ya moto tu.
Kuna mishale inafanana na bastola ambayo haina complication ktk kuipata kwake inauzwa Tanganyika arms na sehem nyingine zinazouzwa silaha sijajua kwa sasa kama wamebadili masharti ya upatikanaji wake. Ukiwa nayo inasaidia sana mm kuna sehem nakaa kuna siku wakajichanganya nilitoka kwa siri nikamuachia mshale mmoja wa mgongoni maana alivamia jirani yetu na mapanga hakuna aliyethubutu kusogelea yule alivyopiga kelele wote walitimka. Lakini inauwezo wa kuuwa ila yule nilimlenga kiunoni makusudi.
 
Wakati nimefika Dar mwaka 2005, nilikuwa naishi Magomeni Kagera.
Basi ajali ikitokea (Moro rd) vijana walikuwa kwanza wanafanya zoezi la uokozi. Baada ya hapo mwenye kuondoka na tairi, jeki, chochote kinachoweza kubebeka ilikuwa ni halali yao!
 
Nakumbuka 2017 nilienda kuishi maeneo ya mwembe chai karibu na mburahati eneo hilo ilikuwa ni kati kwa kati,siku niliyohamia nikiwa napanga vitu hata pazia sijaweka ile naangalia dirishani naona kundi kubwa la vijana wapatao 30 wakiwa wakitembea wengi wamevaa pensi za jins ,kofia za pama au bagalashia na silaha viunoni watu walikuwa wanakimbizana wakijifungia ndani mule ndani akina dada walingia ndani uwepesi na kufunga mlango..nikajisemea mwenyewe leo nimeingia choo cha kike kweli nimekaribishwa kitaani na kodi huwezi kudai ,nikapiga moyo konde nikasema tutapambana hivyo hivyo


E bwana siku nyingine hio kuna rafiki yangu tuliyekuwa tunapiga kazi pamoja na rafiki yangu wa muda tu tokea udogoni alikuja kunitembelea sasa yeye akawa anachezea simu yangu kaketi kibarazani na pembeni walikuwa wamekaa akina mama na alikuwa amevaa kanzu siku hio,mara ghafla kundi la wahuni likawa linapita kwa bahati nzuri ndugu yangu yule alijiongezea fasta akatoka spidi kutafuta njia ya kuelekea chini na aliruka mfereji na kanzu yale wale wahuni wakawa wanamkimbiza huku wanamrushia mawe lakini bahati nzuri aliweza ku escape na alirudi baadae wale akina mama hawakuamini kwa tukio lile wakasema ustazi hatukutegemea kama ungeweza kuruka mfereji ule kwa kanzu ile ,

Sasa hio siku nyingine kuna jamaa alikuwa mgeni bila shaka alimfuata demu wakawa wanaegemea ukuta huku wanaongea hewala mara paap kundi la wahuni wapatao 40 likawa linapita sasa kwenye kundi lile waliokuwa wamekaa mbele ni wenyeji na yule demu walikuwa wanamjua wakawakaushia sasa wale waliokaa nyuma wakawa wamemshika yule njemba wanaondoka nae kwa kumbuluza yule demu akawa anapiga kelele fasta wengine wakamfuata yule demu na kumzaba makofi yule njemba alichukuliwa kila kitu tukio hilo linafanyika mchana nashuhudia kupitia dirisha.

Sasa kuna mchaga mmoja masikini ya Mungu alihamia sasa wakati anashusha mizigo kwenye canter kumbe kuna watoto walikuwa wanachora rada yule Mangi kutoka tu kundi la watu likaingia mule ndani na kusafisha kila kitu yule Mangi kurudi e bwana alishika kichwa na kusema yerewiii akawa anapiga biti anaenda kumshitaki mwenye nyumba lkn mwenye nyumba akasema ningefanya nn na kundi la watu wamekuja na silaha nisingefanya chochote ,mangi alichoka


Mitaa ile kwa chini kuna uwanja wa mpira huko ndio wanakutana watoto wa mburahati,mwembe chai,kagera ,manzese na kuvuta bangi wanakuwa wengi mno sasa wakitoka huko inakuwa amani hakuna

Binafsi ilikuwa siku nimeenda sehemu nikachelewa usiku mkubwa nilikuwa naenda kupumzika kwa washikaji narudi asubuhi nilipokuwa ninaishi kuna siku mpemba na mwenzake walirudi usiku mnene ile wanakatiza uchochoro kumbe na wezi walikuwa wanatokeza yule mwenzake mpemba alikimbia lkn yule mpemba alitaka kupambana nao mwisho wa siku alitobolewa na bisibisi watu walivyotoka kwenda kumsaidia alifia njiani kiukweli mitaa ile ilikuwa hatari kuna dada alikuwa anaolewa sasa ile kitchen party sijui sherehe yake alikuwa anapokea zawadi za kuanzia maisha kama Tv flat,friji,kitanda nk usiku ule wahuni walivamia sherehe na kubeba vitu vyote na kupakiza kwenye toyo na kutoweka nazo

Uwanja wa gine ulikuwa makao makuu ya wahuni ilikuwa kawaida kuona jalamba la panya road kupita ukienda hapo uwanjani ndio utapata jibu la panya road ni akina nani haswa hakuna mechi au ligi itakayoisha salama


Kuna kipindi nilikuwa nakaa mbagala kiburugwa na kipindi hicho nilikuwa nightmare narudi usiku siku ya kwanza nilivyokuwa mshamba nilitaka nipite pekee yangu kwa miguu kuna viwanja vya mpira na michanga ni mingi na pembezoni mwa barabara kulikuwa na miti miti na ofisi za fundi fenicha sasa wakati napita kama Mungu ananionyesha nikamuona mtu kajibanza pembeni ya mti ikabidi nisimame nitizame kwa makini mara ghafla naona kajitokeza lakini akitumia ujanja wa kuficha panga uzuri nilifahamu kuwa alishika panga maana hakuna mkono mrefu wa kiasi kile akawa ananiambia oya fresh pita tu mara naona mtu mwingine akitokezea upande wa pili wa barabara akija upande wetu mara wanatokea wengune nikawa narudi nyuma sasa wakawa wananiongelesha aah sasa yule aliyekuwa ananikaribia nikapata wazo wa kumumwagia mchanga maana sehemu yenyewe ina michanga mingi nilivyomwagia akaachia panga akawa anashika uso sasa hapohapo nikageuza chap na kuanza kufungua mbio maana mita kama 200 kulikuwa kumechangamka na watu wapo wakanikimbiza ila walivyoona nakaribia wakazuga na kutafuta njia wakakunja nilivyofika nikaona kundi la watu mbele wameshukana mikono binafsi sikuwaamini wakanituliza nilivyowaeleza wakaniambia una akili kweli unawezaje kupita hapo pekee yako sisi wenyewe unavyotuona tumesubiriana na kujikusanya ili tupite hapo tuelekee makwetu na ndivyo tunavyofanya hvyo kila siku nikawaambia mm mgeni nilikuwa sifahamu

Siku nyingine narudi usiku nakatiza kichochoro nakutana na watu 3 wamebana pembeni ilinipite kati nilikuwa ninavuta sigara ilikuwa ni style yangu mida ya usiku nikirudi lazima nitembee na sigara sasa kuna mmoja akanipa ishara anataka sigara hapohapo nikamrukia teke akaenda chini kwenye upande wake ndipo nilipopita wakanikimbiza lkn bahati ikawa kwangu lkn nilipokuwa naishi walioajua wakapiga mikwara lkn hawakufanya chochote ila kuna siku pale stendi ya mtongani kuna mpumbavu aliniibia kofia yangu kali,aliruka na kunipiga kichwani na kudaka kofia na kuondoka nayo mithili ya eagle anavyobeba samaki au mdudu..


Kiukweli kipindi nakaa mbagala nilipata misukosuko sana sababu mishe zangu nilikuwa nafanyia mbali na kurudi nilikuwa naweza kurudi saa sita usiku ,mishale mibovu lakini nashukuru Mungu ndio kipindi nilikuwa nafanya mazoezi ya kukimbia nilikuwa fit kwa kiasi chake nilishakimbizwa karibia mita 100 na walikoma wenyewe na kule mwembe chai karibu na mburahati vijana walikuwa wamepinda na mara nyingi walikuwa wanatembea kwa makundi
aisee pole mkuu mm ntaweka yangu si mda inachekesha lkn inauzunisha pia
 
Duh aiseee japo sipendi mauaji laikini natamani akodiwe sniper wa kuwapukutisha hao
 
Mimi wahuni hawanisumbui Mimi mwenyewe muhuni hardcore product ya Manzese mimi shida ilikuwa nilikuwa sisalimii wapangaji wenzangu niko na mambo yangu siku hiyo nikawafuma wananisema sisalimii


Niliwaashia moto nikawaambia salamu hailazimishwi


Hawatakaa wasahau
 
Mimi mweyewe nnahamu nao sana hao panya. kila siku narudi gheto usiku ili nikutane nao ila wapi.
Hahaa Vibaka Wana uwezo mkubwa Sana wa ku scan Ni mtu gani wa kumvamia, nimepita Sana mitaa ya deviscorner tandika mida mibaya Nilikua naishia kuombwa Ela ya fegi tu!😂😂😂😂😂
 
Miliki mguu wa kuku tu, au hata vile vibaruti sijui huwa vinapatikana wapi na ni bei gani.!??
Watu wengi hawajuiilio halisi ya bunduki, ukiwa na lile toy tu lenye baruti ni ulinzi tosha.
 
Kuna mishale inafanana na bastola ambayo haina complication ktk kuipata kwake inauzwa Tanganyika arms na sehem nyingine zinazouzwa silaha sijajua kwa sasa kama wamebadili masharti ya upatikanaji wake. Ukiwa nayo inasaidia sana mm kuna sehem nakaa kuna siku wakajichanganya nilitoka kwa siri nikamuachia mshale mmoja wa mgongoni maana alivamia jirani yetu na mapanga hakuna aliyethubutu kusogelea yule alivyopiga kelele wote walitimka. Lakini inauwezo wa kuuwa ila yule nilimlenga kiunoni makusudi.
Mkuu hakuna hata ka picha ka huo mshale ili hata tukitaka kununua unajua unaanzia wapi kuulizia
 
Back
Top Bottom