Tina
JF-Expert Member
- Jul 9, 2007
- 572
- 579
Misuguano ya ulaji yaibuka bandarini
MSUGUANO umeibuka ndani ya Bandari Tanzania (TPA) kutokana na kuwepo tuhuma za maandalizi ya manunuzi ya kifisadi kupitia kitengo cha manunuzi cha mamlaka hiyo, imefahamika.
Tuhuma hizo zimeibuka baada ya kuwapo kwa hatua za kufanya mabadiliko katika kitengo hicho na kuingizwa kwa watu ambao waliingia TPA katika mazingira tata, wakitokea maeneo alikotokea mmoja wa viongozi wa mamlaka hiyo.
Kabla ya kuingia kwa uongozi mpya chini ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Madeni Kipande, ziliibuka tuhuma za kuunda kitengo cha manunuzi (Management Procurement Unit-PMU) kwa ajili ya maslahi binafsi.
Kilichofuata ni Kipande akiungwa mkono na wizara kuvunja PMU na Bodi za Ununuzi Bandari ya Dar es Salaam na Makao Makuu na kuunda Bodi Kuu ya Zabuni (CTB) wakidai uamuzi huo utakuwa muarobaini wa rushwa na ufisadi na hakutakuwepo athari zozote kiutendaji. Wahenga husema mtoto akililia wembe mpe ajikate na sasa mambo yamebadilika, anasema ofisa mwandamizi wa TPA.
Imeelezwa kwamba ndani ya mwaka mmoja sasa Kipande ameanza kulaumu kuwa Bodi ya Zabuni ya TPA inakwamisha ununuzi na hivyo kukwamisha ufanisi ndani ya TPA.
Lawama hizo hata hivyo hazikuwa za ukweli kwa vile sheria ya ununuzi iko wazi, na CTB ilikuwa inaeleza wazi kuwa inaongozwa na sheria hiyo.
Kipande na watu wake wakashindwa kufanya wanachotaka wao na sasa wanazirudisha zile bodi zilizovunjwa na kuweka watu wao, anasema ofisa huyo ambaye yuko karibu na Kipande kiutendaji.
Habari ndani ya TPA na nyaraka ambazo Tanzania Daima imeziona zinaeleza kwamba Kipande ameunda bodi hizo zikisheheni watu kutoka TANROADS alikotokea.
Bodi mpya ya Ununuzi ya Bandari ya Dar es Salaam inaongozwa na Alois Matei, ambaye ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA (Miundombinu) kutoka Makao Makuu alitokea TANROAD S alikokuwa akifanya kazi na Kipande kabla ya TPA huku Bodi Kuu (CTB) ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu ambaye kwa muundo uliopo anafanya kazi chini ya Matei.
Kwa muundo huu Matei atawajibika kwa CTB ambayo iko chini ya mfanyakazi wake!
Mbali na hayo, Kipande pia kamteua ofisa mwingine kwenye Bodi ya Ununuzi ya Bandari ya Dar es Salaam ambaye ni William Shila, Kaimu Mkurugenzi wa Uhandisi ambaye naye aliletwa TPA akitokea TANROADS .
Hivi hawa viongozi walioko makao makuu wanaingia vipi Bodi ya Ununuzi ya Bandari ya Dar es Salaam kama sio kwa lengo la kufanya ufisadi?
Maajabu mengine ni kuwa mtumishi mmoja kateuliwa kuajiriwa bila usaili wowote pamoja na ukweli ambao umedhihirika kuwa hana uzoefu katika fani ya ununuzi jambo ambalo sheria ya manunuzi inakataza.
Isitoshe mtumishi huyo pamoja na kutokuwa na sifa za kazi hiyo, ndiye kateuliwa na kuwa Katibu wa Bodi ya Ununuzi ya Bandari ya Dar es Salaam na kuwaacha wafanyakazi wazoefu na wenye uwezo wa kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia sheria ya ununuzi, anasema ofisa huyo akisema ni vyema serikali kuu ikafuatilia.
Tayari TPA imeingia kwenye misuguano ya muda mrefu toka kuingia kwa uongozi mpya kiasi cha bodi ya mamlaka hiyo kutaka kumsimamisha Kipande kabla ya Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kuivunja na kuunda mpya.
moja ya tuhuma ambazo bodi iliyovunjwa iliuhusisha uongozi wa Kipande ni pamoja na kuingiza kinyemela mradi wa tozo ya ufuatiliaji wa mizigo kwa mtandao (Eletronic Cargo Tracking Note, e-CTN) bila kufuata sheria na kanuni.
Tayari Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Majini na Nchi Kavu (Sumatra) ilishazuia mradi huo wa e-CTN usitishwe hadi taratibu zitakapofuatwa lakini habari sasa zinaeleza kwamba TPA iko kwenye mkakati wa kubadilisha baadhi ya vipengele kwenye sheria ya TPA ili iweze kutekeleza miradi yake bila udhibiti wowote.
.....
Source: http://www.freemedia.co.tz/daima/misuguano-ya-ulaji-yaibuka-bandarini/