MissTz 2010: Mrembo kakosa umiss kwa kujibu vibaya

ULICHOKISEMA hapo kwenye bold ni sahihi kabisa ila kwangu mimi bado nitasimamia maoni yangu kuwa lile swali halikuwa zuri kwa vigezo vyovyote vile kwenye yale mashindano. Binafsi nilisikitika pale walipomzomea binti wa watu...na hata baadhi ya watu walihisi hivyo hivyo. Kile kitendo cha kuzomewa huenda ..nasema huenda kiliathiri hata maoni ya majaji. Mzoemeo ule haukuwa mdogo eti!Utadhanii ukumbi mzima ulizomea.

WoS hiki ni Kipindi very sensitive and waandaaji should have know that before, sasa pale walihisi ni muendelezo wa ccm kutumia kila mkusanyiko kupiga Kampeni, Umesahau ya Londa na Swala ya Eid?
 
Jamani tafadhali sana mnaweza kututumie hiyo clip hapa, pls waungwana tunaomba huo msaada tunahamu kubwa ya kuona hiyo zomea zomea kwani kama kweli ni baada ya kutaja JK ndo zomea ikatokea basi hiyo ni issue kubwa sana na hiyo ni act of rejection kwa CCM na JK, TUNAOMBA CLIP mliofanikiwa kunyonya tafadhali
 
Lile swali lilikuwa unfair na halikustahili kuwepo kwenye orodha ya maswali.Mabinti wale huenda hata hawazijui vizuri siasa za upinzani na hivyo ilikuwa rahisi sana kwa binti kujikuta akiingia kwenye mtego wa kumshabikia "rais wake aliyeko madarakani".

Hapo! Hawa ndio baadae wanawekwa kwenye ndege wanakwenda kutangaza taifa nje, sasa kama hata current affairs za humu ndani hazijui, si aibu tu huko nje! Ni kama wale vijana wanaojiita 'sisi ni kioo cha jamii' huku suruali zimedondoka, nguo za ndani zinaonekana, manywele utadhani mfungwa, wakiimba sauti zinazokwaruza, na maneno ya kingono ngono tu! Hatuwezi kuwa na nchi namna hii, na kweli tunahitaji mabadiliko, mabadiliko yatakarejesha nchi katika maadili na uadilifu. Ufisadi sio tu kuiba hela serikalini, pia kuishi bila kujali wengine ( awareness of needs of others), kuheshimu utu wa binadamu (kuvaa kitanashati, bila kuonyesha visivyoonekana hadharani). Niseme zaidi?
 
Uporoto ni mpotoshaji mkubwa, wote tulikuwepo na tuliona kilichotokea! Sisiem wataendelea kujiimanisha lakini ukweli utabakia. "Watz wameichoka ccm, wamemchoka Kikwete. Swali lenyewe lilikuwa la kisiasa na watu hawakuzomea wakati akiulizwa. Walimsikiliza kwa makini na sifa alizokuwa akizitaja ni kama alikuwa akimsema Dk Slaa maana alisema anataka Kiongozi makini, Kiongozi mchapakazi na jasiri, anamtaka kiongozi mzalendo anayependa nchi yake, wakati huo watu kimyaa wakimsikiliza. Akaendelea, " ninamtaka kiongozi atakayetuletea maendeleo kama rais Jakaya Kikwete! hapo watu wakaanza kuzomea na kuonyesha kukerwa na mrembo huyo. hayo yametokea mbele ya Ridhwan mwanaye Kikwete, Rostam Azizi mshirika wake kwenye ufisadi na watu wengine wengi ambao wamekuwa wakimsaidia!!! Looool, CCM inapoteza umaarufu kwa kasi ya ajabu. Hivi star TV hawakukata kweli matangazo kuwa wapenda sanaa ya urembo, wametukana???
Kama hili lilionekana kwenye TV nchi nzima, basi sisiem wameipata aibu ya mwaka

Star TV hawawezi kukata matangazo kwani bosi wao alishapigwa chini kwenye uwaziri. Si mnakumbuka alikuwa waziri kisha akatemwa na JK kwenye mojawapo ya mabadiliko ya mawaziri aliyofanya?
 
Hapo! Hawa ndio baadae wanawekwa kwenye ndege wanakwenda kutangaza taifa nje, sasa kama hata current affairs za humu ndani hazijui, si aibu tu huko nje! Ni kama wale vijana wanaojiita 'sisi ni kioo cha jamii' huku suruali zimedondoka, nguo za ndani zinaonekana, manywele utadhani mfungwa, wakiimba sauti zinazokwaruza, na maneno ya kingono ngono tu! Hatuwezi kuwa na nchi namna hii, na kweli tunahitaji mabadiliko, mabadiliko yatakarejesha nchi katika maadili na uadilifu. Ufisadi sio tu kuiba hela serikalini, pia kuishi bila kujali wengine ( awareness of needs of others), kuheshimu utu wa binadamu (kuvaa kitanashati, bila kuonyesha visivyoonekana hadharani). Niseme zaidi?

Sema, sema
 
Kwani contract ya Miss Tanzania inasema nini kuhusu maswali yanayoweza kuwa ya kisiasa na majibu yake? Kuna clause za kukataza ushabiki wa wazi wa kisiasa ?

Na kama kuna clause kama hiyo kwa nini kuwe na swali lililo bordeline kwenye violation ya clause hii kama hilo? Na kama kuna swali bordeline for some reason kwa nini hamna hata reminder kwamba hawaruhusiwi kumtaja mtu? Au ndio mtihani wenyewe? Kwamba kuna kifungu cha kutomtaja mtu katika swali la kisiasa halafu wanakuuliza swali la kisiasa na kukuangalia kama una akili ya kufuatisha sheria? Kama ni hivyo, strategy hii mbona inataka kufumua matatizo makubwa kuliko scope ya Miss Tanzania ?

Vipi kuhusu uhuru wa kujieleza wa mtu binafsi? Au ukitaka kuwa Miss Tanzania ni kama unagombea uongozi, unatupa ubinafsi na kukumbatia uTanzania (with the exclusion of party politics) ?

Nakumbuka Miss California alipata tabu kwa habari ya gay marriage lakini kwa sababu Marekani inaheshimu freedom of speech hawakumnyang'anya ushindi kwa sababu hiyo.

Kwa wanaosema swali lilikuwa ni sifa na sio jina la mtu, mtu anaweza kusema ili kueleweka vizuri zaidi ni muhimu kutoa mifano.Kwamba mtu anaweza kukuuliza sifa za vimiminika, ukasema vinachukua umbo la container lolote vitakavyowekwa ndani yake etc lakini mchanga nao una tabia hii, na ili kukuelimisha zaidi kwamba kimiminika ni kipi anaweza kukutajia mfano wa maji.

Kwangu mimi swala kubwa ni contract na kama imekuwa violated.
 
Join Date Fri Aug 2010

Wanahaha kuja humu kumjengea hoja JK. Lakini wana-JF ni WATU MAKINI. Wamechelewa. Wamechelewa sana.

Ujumbe umefika LIVE BILA CHENGA kwa kambi ya JK. Hata wapenda burudani HAWAKUKUBALI. Huyo kimwana uliyemtuma kazomewa KWA NIABA YAKO! Umemkosesha ushindi binti wa watu! LOL
 
CCM is a bIG Party, chama cha mapinduzi

Mapinduzi ya kiuchumi

Mapinduzi ya kifkra

Mapinduzi ya Elimu

Mapinduzi ya Kilimo

Mapinduzi ya Afya

Mapinduzi ya kidemokrasia

Mapinduzi ya Utamaduni na Michezo

Mapinduzi ya Viwanda

Mapinduzi ......



na Katu si Chama cha kuwaweka watanzania kwenye DEMA, si chama cha mitego
when gays speak!!!!!!!!
 
Jamani tafadhali sana mnaweza kututumie hiyo clip hapa, pls waungwana tunaomba huo msaada tunahamu kubwa ya kuona hiyo zomea zomea kwani kama kweli ni baada ya kutaja JK ndo zomea ikatokea basi hiyo ni issue kubwa sana na hiyo ni act of rejection kwa CCM na JK, TUNAOMBA CLIP mliofanikiwa kunyonya tafadhali
rido kule uka-edit ile font yako ya kipuuzi na ma-blue, bol and sh!t
 
She was completely insane. She didn't speak from her heart. It looked like officials had already prepared them with questions and how are they going to answer them. The whole thing was completely crap MC Taji Liundi manipulated the whole event leaving Jokate hanging you can even see her face that he bored her. It was a crap I saw it. There are no changes other than different stage design as they bluff. I mean its nothing we ain't going no where believe me.
 
shindano gani hilo??? ni hilo la miss tz au kuna la start TV pekee?

wanawake wenzetu hutumiwa kama vyombo vya starehe na hawa wakubw so msishangae mwenzetu alivyosema mchapakazi alikuwa na maana nyingine (alitumia tafsida kidogo)
 
kosa lake labda lilikuwa ni kukosa kusoma alama za nyakati na kujibu suala kwa namna anavyoamini yeye na sio kwa kuwaridhisha mashabiki.

vigezo vya majaji hatuvijui wala havipo wazi, manake kwa hali ya yoyote ile kungelikuwa na vigezo vya kueleweka tusingechagulia mshindi yule aliyechaguliwa!
 
akina nani? mbona hujawa specific na swali lako, walio mzomea? ama waliompa swali la namna hiyo?

NB: uhuru wa maoni haina maana kukubariana na kila kitu eti kwa sababu ya kuheshimu uhuru huo,
maana mpaka hapo wewe pia hujaheshimu uhuru wa maoni ya kuzomewa kwa bi dada huyo, kipofu wa nyakati

Na wewe unawaonea wazomeaji bure kwani Hata Kuzomea ni maoni ya watu na ni Lazima Kuheshimiwe vile

Inwezekana ni kweli ila hii inaitwa ustaarabu. Watu waliostaarabika kamwe hawazomeani pindi wakipingana. Umati ule haukuwa na ustaarabu kwa kumzomea binti yule kisa alimtaja ndugu Kikwete katika jawabu lake.
 
Katika kile kinachoonyesha joto la Dr. Slaa kupanda sana, kwenye shindano la urembo lililoendeshwa na Star TV, mrembo mmoja alizomewa na ukumbi mzima katika mahojiano yafuatayo:

Swali: Utamchagua Rais wa aina...?

Utamchagua Rais wa aina gani? Mgombea wa miss Tanzania ajibu: Nitamchagua Rais anayechapa kazi kama mheshimiwa Jakaya Kikwete.. Watazamaji wazomea: Booooooo!

My Take: Nani kasema kajibu vibaya? Kujibu vizuri au vibaya na kuzomewa ni vitu viwili tofauti. nafikiri tunahitaji tafakari zaidi katika kuchangia. Binafsi sioni ubaya kwa yeye kujimtaja JK (ama hata kama angekuwa mwingine yeyote) kama mchapakazi kwa kadri anavyoona yeye. Tatizo naona watu tumeanza kuhamanika na siasa na kuacha kutafakari
 
Inwezekana ni kweli ila hii inaitwa ustaarabu. Watu waliostaarabika kamwe hawazomeani pindi wakipingana. Umati ule haukuwa na ustaarabu kwa kumzomea binti yule kisa alimtaja ndugu Kikwete katika jawabu lake.

Mkuu, tangu lini watu wanaoenda kungalia mabinti wanaopita mbele za watu huku wamevaa nusu uchi wakawa wastaarabu? Wastaarabu na mambo yao ni ya kiustaraabu na hawaendi huko.
 
..na anavyopenda kupendwa...lazima alikuwa anaangalia LIVE maana kabla hajawa rais alikuwa hakosagi kuhudhuria......,nadhani ka presha kalimpanda baada ya tukio la jana......unajuwa they are really miscalculating where to make there PR..Watu wana hasira...yet kila wanapopita ni mabango tu yanaytokana na PAYE zetu...tukiyaona tunazidi kupata hasira..yet watu wanaingia ukumbini kwa kiingilio chao...unawaletea mambo ya kujitangaza ....shwine!!
kula kumi mkubwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom